Pages

KAPIPI TV

Monday, September 1, 2014

RAIS KIKWETE ATEMBELEA WILAYA YA CHAMWINO KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA DODOMA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Fatma S. Ally alipowasili wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi
 Rais Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wilayani humo
  Rais Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wilayani humo
 Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde “Kibajaji”
 Ujumbe toka kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Msanga
 Kikundi cha utamaduni cha Shule ya Msingi ya Msanga kikitumbuiza
 Rais Kikwete akiangalia ngoma ya Kigogo ikichezwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Msanga
 Rais Kiwkete akiwapongeza wacheza ngoma wa Shule ya Msingi ya Msanga
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi akishauriana jambo na Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe Fatma S. Ally
 Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe Fatma S. Ally akitoa taarifa ya Wilaya
 Watendaji wa Wilaya ya Chamwino wakiwa katika kikao na Rais Kikwete
 Rais Kikwete akitoa ushauri na maagizo kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali
 Watendaji wa Wilaya wakisikiliza kwa makini
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Chamwino akifafanua jambo
 Mwalimu Silvanus Hosea wa shule ya Bwigiri ambaye ni mwalimu mwenye ulemavu wa macho akitoa maoni yake
 Mwakilishi wa shirika la kimataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) akifafanua juu ya mradi wa chakula kwa wanafunzi mashuleni
 Rais Kikwete akitoa ushauri wa njia bora za kuendeleza mradi wa chakula kwa wanafunzi mashuleni
 Vijana waliomaliza elimu ya juu na kuamua kujishuhghulisha na mradi wa kilimo wilayani Chamwino wakitambulishwa. Rais Kikwete ameahidi kuwapatia trekta ili kuongeza tija
 Mmoja wa wataalamu wa miradi akitambulishwa 
 Rais Kikwete akisalimiana na Mwalimu Silvanus Hosea wa shule ya Bwigiri
 Rais Kikwete akisalimiana na wahandisi wa mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
 Sehemu ya mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashuari ya wilaya ya Chwamwino
 Wananchi wakifurahia katika sherehe za uwekaji wa jiwwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Chamwino
Continue reading →

PONGEZI KWA JWTZ KWA KUTIMIZA MIAKA 50 TOKEA KUANZISHWA

 Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa kwenye maonyesho Katika Uwanja wa Taifa.Picha na Maktaba.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa mazoezini.


Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog. 

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo limetimiza Miaka 50 toka Kuanzishwa kwake mnamo tarehe 1/09/1964. 

JWTZ ni moja ya Jeshi lililotajwa na Mtandao mmoja hivi karibuni kuwa Ni Jeshi lenye weredi wa hali juu Duniani kutokana na Operesheni ambazo wamewahi kuzifanya na linalotumia Silaha za Kisasa. 

Baadhi ya Operesheni zilizowahi kufanywa na Jeshi la Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) ni Ile ya Kuwasambaratisha Waasi Wa M23 nchini Congo, Operesheni ya Comoro, Operesheni nyingine ni Ile ya Kulinda Amani Sudan wakiwa wameungana na Majeshi Mengine Kutoka Umoja wa Mataifa (UN)

Jeshi la Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) limejipatia Umaarufu na sifa kutokana na Kuwa na Askari wenye Nidhamu ya Hali ya Juu na Kuwachukulia Hatua kwa Haraka Askari wake ambao wameonyesha utovu wa Nidhamu kwa Wananchi na Jamii kwa Ujumla lakini Pia Sifa Hiyo Kubwa Imekuja Kutokana na uwezo mkubwa wa Kivita na Kuweza Kuwasambaratisha Waasi wa Kikundi cha M23 nchini Congo.

Jukumu kubwa la Kazi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Wavamizi na Vile vile Kushiriki katika kulinda Amani Katika Ngazi ya Kimataifa lakini Pia Pamoja na Majukumu hayo vilevile Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa Mstari wa Mbele katika Kujitoa kwenye shughuli za Kijamii kama Vile Matibabu, Elimu nk na Wamekuwa Mstari wa Mbele katika Kusaidia Jamii katika shughuli mbalimbali kama Vile za Uokoaji katika Maafa yanayotokea Nchini.

Kwa kifupi Sahivi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa jeshi la Kisasa na wasomi ambao wanalisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo yake kama Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujitoa katika shughuli nyingine za kijamii. Hongera ya Kutimiza Miaka 50 Tokea Kuanzishwa 

TAMASHA LA FIESTA 2014 LILIVYOSAMBAZA UPENDO KWA WAKAZI WA MJI WA MOSHI MWISHONI MWA WIKI

 Mmoja wa mashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 pichani akitazama kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Rachael akiimba kwa hisia jukwaani.
 Mashabikii wakishangilia jambo wakati wasanii mbalimbali wa tamasha la Fiesta 2014 wakiendelea kutumbuiza jukwaani.
 Mwanadada Feza Kessy akiimba jukwaani wakati wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyka mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Majengo mjini Moshi.
 Sehemu ya umati wa watu waliofika kushuhudia tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.
 MKali wa kusugua ngoma,kutoka Clouds FM,Dj Zero akiwa kwenye mashine yake ya kazi
 Mashabiki wakisambaza upendo wa kutosha kabisa kwa wasanii wao waliokuwa wakitumbuiza jukwaani.
 Sehemu ya umati wa mashabiki wa tamasha la fiesta wakiwa wamemezwa vilivyo na jicho la samaki
 Wakazi wa jiji la Moshi walisambaza upendo wa kutosha ndani ya tamasha hilo ambalo hukusanyisha watu kutoka vitongoji mbalimbali ndani na nje ya mji wa Moshi.
 Mkali mwingine wa muziki wa Bongofleva,Ali Kiba akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani.PICHA NA MICHUZIJR-FIESTA MOSHI

MRADI WA MAJARIBIO WA KUFUNDISHA MASOMO YA SAYANSI WA UNESCO WANEEMESHA TANZANIA

DSC_0018Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisoma risala ya kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs) kwa wadau wa elimu, wakuu wa shule mbalimbali, maafisa elimu na maofisa wa serikali kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za shirika hilo jijini Dar.

Na Mwandishi wetu
MRADI wa miaka minne wa kusaidia ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa kufanikisha majaribio ya maabara uliokuwa ukifadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na sayansi na utamaduni (UNESCO) na kuendeshwa na wizara ya elimu nchini katika shule 180 zilizopo katika wilaya 34 umemalizika kwa mafanikio huku wito ukitolewa kutafutwa njia ya kuendeleza mradi huo.

Tangu awali mradi huo haukuelezwa kinaga ubaga unakuaje endelevu kama utaonekana kuwa na manufaa kwa taifa.

Akitoa maelezo ya kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs) kwa wadau wa elimu,wataalamu na maofisa wa serikali, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues aliwataka wadau hao kuzingatia mafanikio yaliyokuwapo,kuangalia changamoto zake na kuona namna ya kuendeleza mazuri ya mradi.

Mradi huo wa majaribio ulifanyika katika shule za mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Kagera, Morogoro, Kigoma na Tanga kwa upande wa Tanzania Bara.

Aidha ilielezwa katika kikao hicho kilichofanyika ofisi za Unesco kwa lengo la kuufunga rasmi pamoja na malengo yake ya kuboresha elimu Tanzania kwa kuhakikisha masomo ya sayansi yanafundishwa kwa namna inavyotakiwa, tathmini ilionesha udhaifu wa kutokuwepo na mpango madhubuti wa kuendelezwa kwake.
DSC_0015Mradi huu wa majaribio wa MSK ulilenga kukuza uwezo wa kufundisha masomo ya sayansi (baiolojia,kemia na fizikia) kwa shule ambazo hazina maabara kwakuzipatia visanduku vya majaribio pia uliendesha warsha mbalimbali ili kukuza uwezo wa matumizi ya zana zilizo katika mradi wa MSK pamoja na vitabu vya kufundishia.

Aidha mradi huo ulizingatia pia kuongeza upendo wa masomo ya sayansi kwa jamii na kuwafanya wanafunzi wapende na wawe na hamu na masomo ya sayansi.

Mradi huo ambao umefanyika kwa kuzingatia pia mahitaji ya taifa na kimataifa chini ya dhana ya kuendeleza masomo ya sayansi duniani unaendeshwa na UNESCO kwa kujenga uwezo wa shule za sekondari na msingi kufanya mazoezi ya utambuzi wa nadharia mbalimbali kimaabara hutoa masanduku maalumu ambayo yanakuwa ni kama maabara ndogo zinazotembea.

Maabara hizi hutoa uwezo wa kufanyika kwa majaribio ya msingi na yale makubwa kwa kuzingatia madaraja mbalimbali ya mafunzo kuanzia ngazi za chini kati na juu.

Katika ufungaji wa mradi huo uliofanyika mwishoni mwa mwezi Agosti washiriki walielezwa maendeleo ya mradi hadi mwisho wake na changamoto zilizokuwa zinakabiliwa.

Unesco imesema kutanuka kwa kasi kwa elimu ya msingi kumesababisha changamoto za ubora wa elimu katika mfumo wa elimu nchini na mradi wa majaribio ulionesha kwamba ubora unaweza kurejeshwa kwa kuwa na mpango kama MSKs.
DSC_0021Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau wa elimu, wakuu wa shule mbalimbali, maafisa elimu na maofisa wa serikali waliohudhuria mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa juma.

Kutokana na changamoto za raslimali kushindwa kuhakikisha kwamba kila darasa, mwalimu na mwanafunzi wanakuwa na zana zinazotakiwa kufundisha na kujifunza,walimu na wanafunzi walielemewa na hivyo kuathiri ufundishaji wa masomo ya sayansi ya baiolojia, kemia na fizikia.

Mathalani matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2011 wastani wa matokeo ya masomo ya sayansi kitaifa uliporomnoka chini ya asilimia 50.

Fizikia ilikuwa aislimia 43.2, kemia 43.3 na baiolojia 43.4 na katika takwimu hizo zilionesha kwamba wasichana walifanya vibaya zaidi.

Utafiti ulionesha wazi kwamba udhaifu huo umetokana na kukosekana kwa maabara, vifaa vya kufundishia na upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi.

Pamoja na kuwepo kwa changamoto za uhaba wa masanduku haya ya maabara, tathmini iliyiofanywa ilionesha kwamba mradi ungeliweza kuunganishwa na miradi kama ya JICA na pia kutengenezewa mfumoi wa wa kuweza kuwa endelevu kutokana na umuhimu wake na ufanisi.

Changamoto kama za masanduku machache kuliko yalivyokusudiwa katika mradi , muda mfupi wa kufunza walimu na pia kutekeleza yote yaliyopangwa na suala la ukaguzi bado mradi huu kutokana na asili yake ungelikuwa na maana zaidi kuendelezwa ili kufikia zaidi shule zilizo pembezoni.
DSC_0009Aidha ili kuendelea na mradi huo tathmini iliyofanywa na kuelezwa na Ellen Binagi katika kikao cha wadau ilishauriwa serikali kufikiria kuanzisha vituo na taasisi za kutengeneza maabara hizo ndogo nchini badala ya kuagiza kutoka nje kutokana na gharama zake na hasa ikizingatiwa kwamba Tanzania ni nchi kubwa na yenye shule nyingi.

Binagi alisema kwamba kuanzishwa kwa mtindo huo kumeleta muonekano mpya katika upenzi wa masomo ya sayansi na katika shule za majaribio ufanisi wake ulikuwa mkubwa na ipo haja ya kuangalia namna ya kuendeleza.

Mtathmini huyo pia amesema ipo haja kwa UNESCO na serikali ya Tanzania pamoja na mradi kumalizika kuona namna ya kuuendeleza na kuondoa changamoto zilizoonekana wakati wa utekelezaji wake.
DSC_0012

JOPO LA MAJAJI TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI LATUA KANDA YA KASKAZINI

Picha Na 2Jaji Constancia Gabusa (wa sita kutoka kushoto) akizungumza na mtoto Abdalah Suleman (kulia) aliyefika kisimani kuchota maji katika kijiji cha Chanjagaa wilayani Same. Mradi wa kisima hicho unafadhiliwa na kampuni ya uchimbaji wa madini aina ya bauxite ya Willy Enterprises Ltd
C360_2014-08-27-23-58-06-465Timu ya majaji na sekretarieti ikiangalia bidhaa za urembo zinazotengenezwa na kikundi cha wakinamama wa kimasai cha Ebeneza mara walipotembelea kikundi hicho huko Mirerani. Kikundi hicho kinafadhiliwa na kampuni ya TanzaniteOne ikiwa ni pamoja na kutangaza bidhaa zake nchini Marekani.
Picha Na 3Muuguzi wa zahanati ya Mteke iliyopo wilayani Same Bi. Winfrida Momoya (kulia) akizungumza na majaji Bw. Venance Bahati ( wa pili kutoka kushoto) na Bi Constancia Gabusa (wa tatu kutoka kushoto) mara walipotembelea zahanati hiyo inayofadhiliwa na kampuni ya uchimbaji wa madini aina ya bauxite ya Willy Enterprises Ltd
Picha Na 4Mkurugenzi wa mgodi wa madini ya vito wa TanzaniteOne Bw. Farai Manyemba akisisitiza jambo katika kikao hicho
Picha Na 5Mkurugenzi wa mgodi wa madini ya vito wa TanzaniteOne Bw. Farai Manyemba akielezea mchango wa kampuni hiyo katika huduma za jamii mara timu ya majaji na sekretarieti ilipofanya ziara kwenye mgodi huo
Picha Na 7Jaji Constancia Gabusa (kushoto) akioneshwa urembo na kupewa maelezo na mama wa kimasai ambaye jina lake halikupatikana mara moja juu ya shughuli zinazofanywa na kikundi cha wakinamama wa kimasai cha Ebeneza kinachofadhiliwa na kampuni ya TanzaniteOne.
Picha Na. 8Mkazi wa kijiji cha Kolila, King’ori Bw. Petro Losina akitoa maelezo kuhusu kisima cha maji kilichofadhiliwa na kampuni ya usagaji wa kokoto na utengenezaji wa matofali ya Arusha Aggregates Ltd. mbele ya majaji.

POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA

huu ndio ukumbi uliharibiwa na washabiki mjini stuttgart,ujerumani-1Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,Ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri onyesho lake,washabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi kwa  Euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa onyesho  lingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
 
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,
Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki
Ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.
 
moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa na mshtuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatalini .
 
Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea,kwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
 
mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa
wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promota huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwani inasemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
 
Magazeti ya Stuttgart; yameandika kwa kijerumani  “Washabiki wana hasira nawewe DIAMOND”  kwenye link hii hapa:

Sunday, August 31, 2014

WATANZANIA WAASWA KUPANDA MITI KUTUNZA MAZINGIRA


01Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akipanda mti wa pili aina ya mtiki ikiwa ni ishara ya kuthamini, kuhifadhi na kutunza mazingira nchini wakati wabunge wa bunge hilo walipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana mjini Bagamoyo.02Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Dkt. Margaret Zziwa akipanda mti aina ya mtiki ikiwa ni ishara ya kuthamini, kuhifadhi na kutunza mazingira nchini wakati wabunge wa bunge hilo walipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana mjini Bagamoyo.
……………………………………………………
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
 
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Dkt. Margaret Zziwa ameipa heshima Tanzania kwa kupanda mti aina ya mtiki ikiwa ni ishara ya kuthamini, kuhifadhi na kutunza mazingira nchini.
 
Spika Dkt.  Zziwa alipanda  mti huo wakati wa ziara yake pamoja na wabunge wa EALA walipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana mjini Bagamoyo.
 
 “Huu ni utaratibu wetu na ni azimio tuliojiwekea kama EALA kupanda miti kila tunapoenda kufanya mkutano katika nchi washirika ndani ya jumuiya yetu ili kuwasisitiza wananchi umuhimu wa kutunza mazingira” alisema Dkt.  Zziwa.
 
Dkt.  Zziwa alisema kuwa imekuwa desturi ambayo pia ni utaratibu waliojiwekea bunge hilo kupanda miti kila wanapokuwa na mkutano kila mwaka katika nchi washirika ambapo mikutano hiyo hufanyika kwa mzunguko ndani ya jumuiya.
 
Dkt. Zziwa alieleza kuwa zoezi la kupanda miti hiyo lilikuwa lifanyike Dar es Salaam lakini yeye na wabunge wa EALA waliamua lifanyike Bagamoyo ambapo pamoja na kutembelea Taasisi ya TaSUBa wamepata kujionea hazina ya historia Afrika Mashariki iliyopo katika mji mkongwe wa Bagamoyo.
 
Aidha, Dkt. Zziwa amempa jukumu la Mbunge wa EALA kutoka Tanzania ShyRose Bhanji kutembelea taasisi hiyo na kujionea hali ya miti waliyoipanda wakati wa ziara yao inavyoendelea kumea na kutoa taarifa mara kwa mara katika bunge hilo.
 
Kwa upande wake Mbunge wa EALA kutoka Tanzania Makongoro Nyerere ametoa wito kwa Watanzania wa kutunza mazingira kwa kupanda miti mingi iwezekanavyo ili kutunza mazingira.
 
Makongoro amesema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi ahamasike, kila mwananchi mmoja mmoja apande mti mmoja autunze hadi ukue.
 
Makongoro alisisitiza kwa kusema, “Miti ina umuhimu mkubwa sana katika jamii yetu, inasaidia kutunza uso wa ardhi yetu na rutuba kwa manufaa ya kilimo bora katika nchi yetu’’.
 
“Miti ni uchumi katika nchi, inatumika kujengea, kutengenezea samani za maofisini na majumbani, viwandani kutengeneza vitu mbalimbali ikiwamo viberiti na vyombo vya kusafiria vya baharini” alisema Makongoro.
 
Aidha, Makongoro alisema kuwa kutokana na hatari ya mabadiliko hali ya tabia nchi yanavyoendelea, ni wajibu wa kila Mtanzania kutunza mazingira na kuzingatia usemi wa “Kata mti, Panda miti” ili kuboresha hali ya hewa nchini na mazingira yawe rafiki kwa viumbe vyote vilivyopo kwenye maji na nchi kavu wakiwemo wanyama, mimea, samaki na viumbe wengine wanaoishi kwenye maji.
 
Katika tukio la upandaji miti, ilipandwa jumla ya miti mitatu katika taasisi ya TaSUBa ikiwa ni juhudi zinazofanywa na bunge la EALA katika kutunza mazingira kwa vitendo.
Mti wa pili ulipandwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara na wa tatu ulipandwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki, Dkt. Abdala Juma Abdulla Saadalla.

WATANZANIA WAASWA KUTUNZA MAZINGIRA.


Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
31/8/2014
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Dkt. Margaret Zziwa ameipa heshima Tanzania kwa kupanda mti aina ya mtiki ikiwa ni ishara ya kuthamini, kuhifadhi na kutunza mazingira nchini.
 
Spika Dkt.  Zziwa ualipanda  mti huo wakati wa ziara yake pamoja na wabunge wa EALA walipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana mjini Bagamoyo.
 
“Huu ni utaratibu wetu na ni azimio tuliojiwekea kama EALA kupanda miti kila tunapoenda kufanya mkutano katika nchi washirika ndani ya jumuiya yetu ili kuwasisitiza wananchi umuhimu wa kutunza mazingira” alisema Dkt.  Zziwa.
 
Dkt.  Zziwa alisema kuwa imekuwa desturi ambayo pia ni utaratibu waliojiwekea bunge hilo kupanda miti kila wanapokuwa na mkutano kila mwaka katika nchi washirika ambapo mikutano hiyo hufanyika kwa mzunguko ndani ya jumuiya.
 
Dkt. Zziwa alieleza kuwa zoezi la kupanda miti hiyo lilikuwa lifanyike Dar es Salaam lakini yeye na wabunge wa EALA waliamua lifanyike Bagamoyo ambapo pamoja na kutembelea Taasisi ya TaSUBa wamepata kujionea hazina ya historia Afrika Mashariki iliyopo katika mji mkongwe wa Bagamoyo.
 
Aidha, Dkt. Zziwa amempa jukumu la Mbunge wa EALA kutoka Tanzania ShyRose Bhanji kutembelea taasisi hiyo na kujionea hali ya miti waliyoipanda wakati wa ziara yao inavyoendelea kumea na kutoa taarifa mara kwa mara katika bunge hilo.
 
Kwa upande wake Mbunge wa EALA kutoka Tanzania Makongoro Nyerere ametoa wito kwa Watanzania wa kutunza mazingira kwa kupanda miti mingi iwezekanavyo ili kutunza mazingira.
 
Makongoro amesema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi ahamasike, kila mwananchi mmoja mmoja apande mti mmoja autunze hadi ukue.
 
Makongoro alisisitiza kwa kusema, “Miti ina umuhimu mkubwa sana katika jamii yetu, inasaidia kutunza uso wa ardhi yetu na rutuba kwa manufaa ya kilimo bora katika nchi yetu’’.
 
“Miti ni uchumi katika nchi, inatumika kujengea, kutengenezea samani za maofisini na majumbani, viwandani kutengeneza vitu mbalimbali ikiwamo viberiti na vyombo vya kusafiria vya baharini” alisema Makongoro.
 
Aidha, Makongoro alisema kuwa kutokana na hatari ya mabadiliko hali ya tabia nchi yanavyoendelea, ni wajibu wa kila Mtanzania kutunza mazingira na kuzingatia usemi wa “Kata mti, Panda miti” ili kuboresha hali ya hewa nchini na mazingira yawe rafiki kwa viumbe vyote vilivyopo kwenye maji na nchi kavu wakiwemo wanyama, mimea, samaki na viumbe wengine wanaoishi kwenye maji.
 
Katika tukio la upandaji miti, ilipandwa jumla ya miti mitatu katika taasisi ya TaSUBa ikiwa ni juhudi zinazofanywa na bunge la EALA katika kutunza mazingira kwa vitendo.
 
Mti wa pili ulipandwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara na wa tatu ulipandwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki, Dkt. Abdala Juma Abdulla Saadalla.