Pages

KAPIPI TV

Saturday, August 23, 2014

VIFAA VYA KUBAINI DALILI ZA AWALI ZA UGONJWA WA EBOLA KUPITIA JOTO LA MWILI VYAWASILI NCHINI, KUANZA KUTUMIKA VIWANJA VYA NDEGE.


???????????????????????????????
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Steven Kebwe (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi Dkt. Elias Chinamo moja ya kifaa (kamera) itakayotumika kupima dalili za ugonjwa wa Ebola kwa wasafiri wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege ili kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama kwa kuuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.
???????????????????????????????
Mkurugenzi wa Ugavi wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD),Heri Mchunga (kushoto)  akimpima Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi Dkt. Elias Chinamo (kulia) kuonyesha namna moja ya kifaa cha kupimia joto la mwili wa Binadamu kinavyofanya kazi kwa kubaini dalili za Ugonjwa wa Ebola eneo la uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 
???????????????????????????????
Moja ya kifaa (kamera) nne zilizoagizwa na Serikali kupimia dalili za ugonjwa wa Ebola maeneo ya viwanja vya ndege. Kifaa  hicho kina uwezo wa kutunza picha na kumbukumbu za msafiri, muda , joto la msafiri, tarehe aliyoingia nchini pia uwezo wa kupata takwimu kutoka kwenye hali ya majimaji au jasho la Binadamu pindi kinapoelekezwa kwake.
???????????????????????????????
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Steven Kebwe akiongea na waandishi wa habari eneo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa kupokea na kukabidhi vifaa vya kupima dalili za ugonjwa wa Ebola. Wengine ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Dharula na Maafa (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifani.
???????????????????????????????
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Steven Kebwe akiangalia kwa karibu taarifa zilizorekodiwa na moja ya kifaa (kamera) nne zilizoagizwa na Serikali kupimia dalili za ugonjwa wa Ebola maeneo ya viwanja vya ndege.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
………………………………………………………………………………….
 
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
 Dar es salaam.
 
 Sehemu ya vifaa vya kubaini hatua za awali za ugonjwa wa Ebola kwa kupima hali ya joto la mwili kwa wasafiri kutoka nje nchi wanaotumia viwanja vya ndege  vilivyokuwa vimeagizwa na Serikali vimewasili jijini Dar es salaam.
 
Vifaa hivyo vinavyohusisha kamera 4 zenye uwezo wa kubaini joto la mwili wa msafiri kwa umbali wa mita 100 bila  kumgusa muhusika vimewasili leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam kutoka nchini Afrika ya Kusini vilikonunuliwa.
 
Akikabidhi vifaa hivyo kwa wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Steven Kebwe amesema kuwa kuwasili kwa vifaa hivyo ni moja ya juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama kwa kuuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.
 
Amesema vifaa hivyo vitapelekwa katika maeneo ya viwanja vya ndege na maeneo yanayotumiwa na raia wa kigeni kuingia nchini vikiwemo vya Dar es salaam, Zanzibar, Kilimanjaro,Mbeya na Mwanza.
 
Ameongeza kuwa Serikali inaendelea na mpango wa kuagiza vifaa zaidi vya kuwezesha shughuli ya upimaji wa afya kwa wasafiri wanaotembea (scanners) zitakazowezesha kubaini afya za wasafiri wengi zaidi kwa wakati mmoja bila kulazimu kuwasimamisha.
 
Aidha, amewataka wataalam hao wa afya kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa kwa kuhakikisha wanawapima abiria wote wanaotoka nje ya nchi bila kujali hadhi walizonazo ili kuweza kubaini kama wana maabukizi au dalili za ugonjwa wa Ebola.
 
“Nataka mfanye kazi yenu kwa kuzingatia weledi wa taaluma yenu na kwa kuzingatia yale mliyojifunza,mvitumie vifaa hivyo kupima kila abiria ili kubaini joto lake bila kujali cheo wala hadhi yake maana janga hili ni kubwa” Amesema Dkt. Kebwe.

 
Kuhusu utunzaji wa vifaa hivyo amewataka wataalam hao kuhakikisha wanavitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu na kutimiza malengo yaliyokusudiwa ya kuwasaidia wananchi kutokana na vifaa hivyo kugharimu fedha nyingi kila kimoja.
 
Katika hatua nyingine Mh. Kebwe amefafanua kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaendelea na shughuli ya utoaji wa Elimu ya Afya kuhusu ugonjwa wa Ebaola ili kuwawezesha wananchi kuchukua tahadhari na kuzielewa dalili za ugonjwa huo na namna ya kujingika endapo utagundulika nchini.
 
Amesema tayari  kamati mbalimbali za wataalam zimeshaundwa ili kuwezesha zoezi la utoaji wa elimu na mafunzo kwa wataalam wa ndani ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na janga hilo.
 
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), Cosmas Mwaifwani ambaye ofisi yake imehusika katika uagizaji wa vifaa hivyo nchini Afrika ya Kusini  amesema kuwa mahitaji ya vifaa hivyo kwa sasa yameongezeka kutokana na umuhimu wake na jinsi vinavyofanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
 
Amesema upimaji kwa kutumia vifaa hivyo unatumia teknolojia ya kubaini mionzi ya joto kutoka katika mwili wa binadamu pindi vinapoelekezwa katika maeneo ya macho na masikio ya mwili wa binadamu.
 
Amefafanua kuwa vifaa hivyo vinauwezo wa kutunza picha na kumbukumbu za msafiri, muda , joto la msafiri na tarehe aliyoingia nchini na kuongeza kuwa vifaa hivyo vina uwezo wa kupata takwimu kutoka kwenye hali ya majimaji au jasho la Binadamu pindi kinapoelekezwa kwake.
 
Mwaifwani ameeleza kuwa MSD inaendelea kuimarisha uwezo wake kwa kuongeza vifaa zaidi kutoka Ubelgiji na China na kufafanua kuwa Bohari hiyo imejiandaa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kwa kujenga uwezo wa kuwa na dawa za kutibu hali ya magonjwa yanayoambatana na homa hiyo.
 
Naye Mkurugenzi wa Viwanja vya ndege nchini, Moses Malaki akizungumza kwa niaba ya Viwanja vya ndege nchini ameielezea hali hiyo ya upatikanaji wa vifaa  katika maeneo hayo kuwa itaongeza ufanisi wa uchunguzi wa afya kwa wasafiri na kuondoa usumbufu kutokana na uwezo wa vifaa hivyo kumpima msafiri akiwa mbali

MISS TEMEKE 2014 APATIKANA TCC CLUB CHANG'OMBE JIJINI DAR


MMGM3002
Mshindi wa taji la Miss Temeke 2014,Sitti Mtemvu akipungia mkono mara tu baada ya kutangazwa rasmi kuwa ndie aliestahili kupata taji hilo katika shindano lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa TCC Club,Chang’ombe jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mshindi wa pili,Salama Saleh na kulia ni Mshindi wa tatu,Neema Mollely.PICHA KWA HISANI YA MICHUZIBLOG
MMGM2844
Mwanalibeneke Othman Michuzi akimvisha taji la Michuzi Blog Miss Photogenic 2014 Mrembo Lilian Loth (9) kwa niaba ya Ankal,baada ya kuonekana ndie Mrembo pekee mwenye mvuto wa picha katika shindano la Miss Temeke 2014,lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa TCC Club,Chang’ombe jijini Dar es salaam
MMGM2906
Baadhi ya Warembo wa Miss Temeke 2014 wakiongozwa na Michuzi Blog Miss Photogenic,Lilian Loth wakiwa kwenye picha ya pamoja kusubiria kutangazwa mshindi wa jumla wa shindano hilo.

DIWANI ATAKA WATUMISHI IDARA YA ARDHI KIGOMA WANAOTOA HATI FEKI KUCHUKULIWA HATUA

Na Magreth Magosso,Kigoma

DIWANI  wa  kata ya Businde  Said Makala Mkoa wa hapa, ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji  iwachukulie hatua  za  kisheria na nidhamu  kwa  watumishi  wa  idara  ya  Ardhi wanaowahujumu  wananchi  kwa  kuwapa  hati feki  za umiliki  wa ardhi .
 
Akizungumza na gazeti hili  kigoma Ujiji  jana Makala alisema, watumishi wa idara husika wanachangamoto ya kuwachonganisha wananchi na serikali iliyopo madarakani kutokana na sintofahamu ya  hati sahihi ,ambapo  inachangiwa  na madiwani wa hapa kutokuwa wazalendo na adha zinazowakabili raia husika.
 
“watendaji na uongozi wa manispaa upo kimya wakati wananchi wanajenga  hatimaye huwatumia mgambo na kubomoa kwa kuvizia kwa madai wapo kinyume cha sheria, wanahujumu raia wasio na hatia ,utawala wanaujua ukweli  na jamii  inafuata taratibu za kupata hati na kulipia kodi za jengo wahusika     si  wazalendo” alibainisha Makala.
 
Zena Tuza ni miongoni mwa wachache waliothubutu kumfuata diwani huyo  na kumpatia hati feki aliyomilikishwa na manispaa hiyo sanjari na kubomolewa kwa madai amejenga katika eneo la awali la msitu wa masanga ambapo kwa  sasa  kaya zinaendelea kujengwa  .
 
Alishauri kuwa, ili kuondoa adha hizo idara husika watumie mikutano ya hadhara kwa kuwashirikisha madiwani wa manispaa hiyo kwa lengo la kutoa elimu sahihi na vigezo vya kupatiwa hati miliki iliyo halali na si kutumia utashi wa kisiasa kuharibu malengo ya jamii na kuitupia lawama serikali tawala.
 
Akijibia  hilo  Mwenyekiti  wa  kamati  ya  Fedha  na Mazingira  Adam  Mussa  alisema wananchi wataendelea kuvunjiwa  makazi  kwa uzembe wa kushindwa  kubaini maeneo tengwa  kwa  ajili ya makazi ya watu.
 
Alisema kutokana na hati aliyotoa muhanga huyo akili ni feki na kuwataka wananchi wasikubali kuuziwa  viwanjwa katika maeneo tengefu na mapori ya hifadhi wakati huohuo Kaimu meya wa mnispaa hiyo Rashid Yunus alidai watumishi watakaobainika kufanya hivyo watawajibika.
 
Yunus  alishauri  idara  ya  ardhi  iwe  wazi  katika  uwajibikaji  wake  kwa  mujibu wa  sheria,kanuni na taratibu  zilizopo  kwa  lengo la  kuwaondoa  walengwa  katika  changamoto  ya  kubomolewa  makazi sambamba  na  kutoa  elimu sahihi  kwa  kuzingatia  wiazara  husika  na  isiwe chanzo cha kuwachonganisha  umma  na viongozi.

KIKONGWE WA MIAKA 76 AAMUA KUJITENGENEZEA JENEZA LAKE MWENYEWE KWA SABABU YA UGUMU WA MAISHA

Bi
Scholastika Mhagama akiwa katika mlango wa nyumba yake.
 ———————
 
Na Oswald Ngonyani wa demashonews
– Peramiho.
 
Wahenga walisema ‘Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni;’ Jamii inazidi kujawa na chuki naukatili ndani yake, imekuwa kawaida siku hizi kusikia fulani kamuua fulani kwakisa kisichokuwa na maana.Maalbino wanakatwa viungo vyao kwa visingizio vya
kupata utajiri kwa watu wasiokuwa na huruma, watoto wadogo wananyimwa haki zao na kuwekwa ndani ya maboksi na wengine kuishi maisha yao katika uvunguza
kitanda yote haya ni mambo ya kutisha yanayotendeka katika jamii zetu.
Hali imekuwa tete amani na upendo vinazidi kuyeyuka
kama barafu, watu hawana utu tena, wamejivika ngozi za kondoo wakati mioyo yao ni ya Simba, hakuna tena roho ya huruma kwa wanadamu wa dunia ya leo.
Choo cha bibi Scholastika Mhagama
Jeneza la bibi likitolewa ndani kwake na wanachama wa Kombination Camp
 Jeneza la Bi Scholastika Mhagama
 
Akielezea historia ya maisha yake Bi Scholastika
anasema alizaliwa akiwa na miguu yote lakini alipata bahati mbaya ya kugongwa
na nyoka alipokuwa darasa la pili hali iliyomfanya kukatwa mguu ili kuepusha
madhara mengine kama vile kifo. Hivyo maisha yake yalibadilika na tangu hapo
akawa mlemavu.
 
 Hali hiyo ya ulemavu lakini pia uzee alionao vimemfanya ashindwe kujihudumia kwa lolote zaidi ya kupika tu. 
 
Hata hivyo anakosa mahitaji muhimu kama vile maji na chakula
hali inayomfanya alale na njaa kwa baadhi ya siku.
Kwa hali aliyo nayo ni wazi kuwa Bi Scholastika anahitaji baiskeli ya miguu mitatu (wheel chair) ambaye itamwezesha  kutembea kwa kuwa hivi sasa anatambaa na kupata maumivu makali kutokana na nyama
iliyobakia kwenye nyonga baada ya kukatwa mguu.
 
Bi Scholastika anazidi kueleza kuwa kuna watu waliwahi kufika kumuandikisha jina lake na kumuingiza katika orodha ya watu wanaostahili kupata msaada lakini anasikia misaada inafika kwa jina lake lakini yeye mwenyewe hajawahi kuipata.
 
Vipi kuhusu Sera ya Wazee?Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003
inaweka bayana kuwa suala la uzee na kuzeeka limekuwa lenye umuhimu mkubwa
ambapo karne ya ishirini imeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya wazee.
 
Kwa kurejelea takwimu zilizopo ni kwamba, ifikapo mwaka 2050 idadi ya wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 nchini hapa itaongezeka na kufikia wazee milioni 8.3 (Sawa na asilimia 10 ya watanzania wote)
 
Kama hiyo haitoshi, Taarifa ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 1999 inaeleza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wazee duniani na kwamba ongezeko hilo linaonekana zaidi katika nchi zinazoendelea (Tanzania ikiwepo) ambapo viwango vya ongezeko hilo havilingani na uwezo wa rasilimali zilizopo za kuwahudumia.
 
Rasilimali hizo zinajikita zaidi katika Nyanja za
msingi katika makuzi ya binadamu yoyote zikiwemo Nyanja za afya, lishe na
huduma nyingine za msingi zisizoweza kuepukwa na binadamu yeyote.

MFANYAKAZI WA HOSPITALI YA PERAMIHO SONGEA AJINYONGA

Mwili wa Fredrick Mgaya (60) ukiwa unaning’inia katika mtu aliojinyongea , Tunaomba radhi kwa picha hii.
————————–
 
Mwanaume mmoja Fredrick Mgaya(60), mkazi wa Peramiho, Songea mkoani Ruvuma amejinyonga usiku wa kuamkia leo katika maeneo yaliyo karibu na viwanja vya michezo vya Abasia kijijini Peramiho. 
 
 Mwanaume huyo aliyekuwa akifanya kazi kitengo cha maabara katika Hospitali ya Peramiho na kustaafu mnamo mwezi aprili mwaka huu amekutwa amejinyonga majira ya asubuhi ya leo.
 
Marehemu Fredrick Mgaya amekutwa na ujumbe katika mfuko wa shati lake, ulioelezea chanzo kilichopelekea yeye  kujitoa uhai.
 
Afande Allen Urio ambaye alikuwa mmoja wa mashuhuda wa kwanza,anasema “ Nilikuwa natoka lindo asubuhi ndipo nikakuta kundi la wanafunzi wa shule ya msingi wakiwa njiani, nikawauliza kwanini wamesimama badala ya kwenda shule muda ule, ndipo waliponiambia kuna mtu ananing’inia kwenye mti pale. Nilipofika kwenye mti huu ndipo nilipomkuta mzee wetu Fredrick Mgaya akiwa ameshapoteza maisha.
 
Ni tukio la kusikitisha sana kwani ni mzee wetu katika jamii ambaye tulikuwa tunaishi naye vizuri. 
 
Mbali na migogoro yake na mkewe lakini uamuzi aliouchukuwa unasikitisha na si mzuri
kabisa. Kama mlinda amani katika jamii napenda kuwaasa wananchi wajaribu
kutafuta suluhu ya matatizo kwa namna nyingine na sio kwa kujitoa uhai”
 
Akiongea  Hakimu wa mahakama ya mwanzo kijijini Peramiho bi Maria Sambo amesema, ameshaletewa na kusuluhisha migogoro ya ndoa hiyo ya marehemu mara mbili na hadi sasa kuna kesi inayoendelea katika mahakama ya Hakimu mkazi, lakini  kwa hali ya
kawaida hakudhani kwamba marehemu Fredrick Mgaya angefikia hatua hiyo ya
kujitoa uhai. 
 
Nao mashuhuda wa tukio hilo wakiongea kwa masikitiko, wengi wamelaani uamuzi uliofikiwa na mzee Mgaya kwani ni dhahiri alikuwa ni mtu wa watu na pia alikuwa ni tegemeo la familia yake ambayo amewaacha ghafla. 
 
Uamuzi ambao umesababisha maumivu kwa wanajamii hususan ndugu, jamaa pamoja na marafiki wengi waliokuwa wakimpenda na kushirikiana naye
kwa mambo mengi ya kimaisha.
 
 
 Mwenyekiti wa kijiji cha Peramiho A Bwana Joseph Ngonyani ameonesha masikitiko yake ya dhati kwa kuondokewa na moja ya wazee aliokuwa akiwategemea kwa ushauri katika kijiji chake. 
 
“Tukio hili linagusa sana unajua, kwasababu linahusu mtu wa karibu sana na ambaye
tunashinda nae siku zote bila kujua nini kinamsibu na nini anakipanga katika akili yake”. 
 
Ndoa nyingi sana zinasumbuliwa na migogoro ya hapa na pale, hivyo ni vizuri watu wa ustawi wa jamii na asasi zinazohusiana na jamii kujaribu kutoa mafunzo na maelekezo ya jinsi ya kutatua migogoro hiyo ili kuepusha adha kama hii isijitokeze tena ndani ya jamii
yetu.Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo bwana Ignasi Kapinga.
 
Winfried Thadei Mgaya, mdogo wa marehemu anasema, amepokea tukio hilo kwa mshtuko na kwa majonzi sana. 
 
Anapata uchungu sana juu ya msiba wa kaka yake kwani marehemu ameacha watoto wanne ambao bado ni tegemezi pamoja na mjane. Pia amesema mazishi yatafanyika tarehe 7 jumamosi  kijijini kwao Madaba, Songea
mkoani Ruvuma.
Habari kwa hisani ya Demashonews

ACT WADAI KUMLINDA ZITTO KABWE -KIGOMA

Baadhi ya wanachama wapya wakivamia jukwaa la ACT  katika kiwanja cha cine atlasi  manispaa ya kigoma ujiji wakitaka wapewe kadi za chama hicho .
kaimu mwenyekiti akihutubu madhira yaliyochangia kukihama chama cha chadema katika kiwanja cha cine atlas manispaa ya kigoma ujiji.

walioshika bendera za chama katikati aliyevaa flana ya bluu na njano ni katibu ACT wilaya ya kigoma Anzoluni Kibela akiwa ameshika bendera za chadema kutoka kwa wanachama wapya pembeni yake ambao wamekihama Chadema jana katika kiwanja cha cine atlas manispaa ya  kigoma ujiji na hapo chini ni baadhi ya kadi za chadema.

Na Magreth Magosso,Kigoma

Chama  cha  Alliance Transiparency For Change(Act) Mkoa wa Kigoma, kimeahidi kumlinda  Mbunge  wa  Jimbo la Kigoma Kaskazini  Zitto Kabwe kwa gharama zote kutokana na hila zinazofanywa na mahasimu wachache wa chama cha chadema za kutaka kumwangusha kisiasa.
 
Pia wamemshauri afute kesi yake dhidi ya uongozi wa Chadema na kumtaka arudi Kigoma aungane na ACT kwa ajili ya kukusanya  wanachama katika vijiji   vilivyopo hapa kwa lengo la kukuza demokrasia  ya uwazi,uwajibikaji  wenye tija kwa wananchi .
 
Akitoa kauli hiyo kigoma ujiji jana  Mjumbe  Kamati  Kuu  Taifa  Jaffar Kasisiko   katika mkutano wa hadhara uliofanyika  kiwanja cha Cine Atlas uliokuwa ukiwakabidhi  kadi wanachama  wapya  kutoka  vyama mbalimbali  ambapo   wanachama hao  walichana kadi ,bendera na katiba ya chadema wakidai  wameshindwa kukihudumia chadema mkoani hapa.
 
Alisema uongozi wa chadema una hila ya kusambaza maneno hasi dhidi ya Zitto Kabwe  kwa umma kwa lengo la kulinda maslai yao binafsi ,badala ya kutetea haki za wanyonge ili kuboresha changamoto zilizopo kwa tija ya kuondoa fujo na vurugu zinazolinyemelea  taifa husika.
 
“Zitto ni wa hapa,tutamlinda kwa njia zote na huyu Sabrina Sungura achunge ndimi yake,ni mwanetu lakini aache fitna asome alama za nyakati ,akumbuke aliyemuweka katika kiti alichokalia” alibainisha  Kasisiko.
 
Mjumbe halmashauri kuu Taifa Msafiri Wamalwa alisema ,Mbunge huyo asipoteze muda wa kulumbana na uongozi wa chadema,badala yake akaifute kesi katika mahakama husika na aje hapa ili kukijenga chama  hicho.
 
Katibu mwenezi wilaya ya kigoma Anzoluni Kibela alisema hadi sasa kadi  ya kiongozi huyo ipo tayari na kuna wabunge wapatao 18 wapo tayari kujiunga na chama kwenye uzinduzi ,ambao utafanyika mkoani hapo mwanzoni mwa mwezi ujao.
 
Kwa upande wa Kaimu mwenyekiti Taifa Shaban Mambo aliwasihi wananchi wamuunge mkono mbunge huyo atakapojiunga na chama hicho, ili aboreshe adha ya usafiri wa njia ya reli ya kati kwa kuwaletea treni inayotumia umeme kwa gharama zake.
 
Baadhi ya wanachama wapya wa ACT aliyekuwa mweka hazina  Chadema kigoma ujiji, Hamidu Hamis na Katibu wilaya Haji  Idd  kwa nyakati tofauti walisema wamejiunga na ACT kwa nia ya kuleta mabadiliko  ya umoja,uwazi na uwajibikaji kwa mujibu wa dira ya chama hicho.
 

Sunday, August 17, 2014

KIGOGO CCM AKATALIWA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU

Na Allan Ntana,Tabora

WAJUMBE zaidi ya 130 wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi
Tabora mjini wamemkataa Katibu wa Chama hicho wilaya ya Tabora mjini
Bakar Luasa kwa madai ya kukigawa na kukichafua.

Hatua hiyo ilifikiwa Agosti 12 mwaka huu baada ya wajumbe hao
kuamua kutoka nje ya ukumbi wa Ali Hassan Mwinyi kwa madai ya kutokuwa
na imani na Katibu huyo wa CCM wilaya.

Chanzo cha taarifa toka kwa wajumbe wa halmashuri kuu ya CCM ndani ya
kikao hicho ambao hawakutaka majina yatajwe walisema kufuatia hali
hiyo kikao kiliahirishwa na kufanyika tena mwezi Agosti 13 mwaka huu.

Wajumbe hao walisema baada ya kuingia ukumbini walitoka
nje na kuongea kwa nyakati tofauti wakidai hawamtaki Katibu wao Bakar
Luasa kwa madai kuwa hawana imani naye na anakigawa chama.

“Huyu Katibu wetu ana kama miezi sita au saba hivi na toka amehamia hapa Tabora
lakini tokea afike amekuwa akikivuruga chama kwa migogoro
isiyoisha…….kwa kujifanya yeye anajua ilani na taratibu za chama kila
kukicha anagombana na Mwenyekiti wake”, waliongeza.

Walisema Mwenyekiti wa CCM Tabora mjini Abrahman Nkonkota aligombea
vipindi viwili na
akashinda kwa kura nyingi hivyo kama Mwenyekiti wetu ana tatizo wapo zaidi
ya Makatibu wanne ambao wamepita hatukuona wanakwaruzana naye.

Walisema Katibu huyo wana taarifa anapokea fedha kila mwisho wa mwezi
ili aendeleze fujo na kugawa chama kwa maslahi yake na kamwe
hawataweza fanya kazi na Katibu Bakar Luasa kutokana na kuendeleza
majungu na fitina.

Walisema alipeleka taarifa Makao Makuu ya chama kuwa hakuna
watendaji, sasa wanachama na wajumbe ambao hawamtaki tunatamka wazi
kuwa tunatoka nje ya ukumbi, hatumtaki.
 
Mwandishi wet alimtafuta Katibu wa CCM Bakar Luasa kuhusiana na madai
hayo ambapo alisema yeye hana tatizo, mwenye tatizo ni Mwenyekiti wake
kwani ndiye anaratibu hayo.

“Mimi nafikiri kila kitu kiko wazi kama mimi ni tatizo kwani katibu
mkuu wa CCM Abdurahaman Kinana alikuja akaelezwa na makamu
mwenyekiti wa CCM Philip Mangula naye alielezwa tunasubiri maamuzi ya
kamati kuu ya CCM” alisema.

Alisema kwa kuwa kamati kuu inataka kuchukua maamuzi dhidi yangu na
Mwenyekiti, sina cha kueleza zaidi tusubiri.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini Abdulrahaman Moshi Nkonkota
alijibu kuwa tuhuma hizo si za kweli yeye hana matatizo kwani kila kitu kiko
wazi,..... mimi siwezi kushawishi wajumbe zaidi ya 140 wamkatae Katibu wangu
ili iweje, aliongeza.

Alisema, ukweli ni kwamba anagawa chama,  hapa ofisini haelewani na
watendaji, wanachama na mimi mwenyewe kwani hataki kufanya kazi na mimi.

MAJAJI WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENT (TMT) WAKIFUATILIA FILAMU FUPI ILIYOCHEZWA NA BAADHI YA WASHIRIKI WA SHINDANO HILO

Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakifuatilia Filamu fupi iliyochezwa na baadhi ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie talents (TMT) wakati ilipokua ikionyeshwa kwenye runinga kubwa katika Ukumbi wa Makumbusho. Kutoka Kulia ni Single Mtambalike au Rich Rich katikati ni Vyonne Cherry au Monalisa na Kushoto ni Jaji Mkuu wa Shindano hilo Roy Sarungi.
 Mahosti wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwajibika katika Jukwaa la Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea alhamisi iliyopita.
 Mmoja kati ya Washindi kutoka Kanda ya Pwani, Mkoa wa Dar Es Salaam katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Shiraz Ngassa (wa Kwanza Kushoto) akiongea na Msanii Joti mara baada ya Kuaga rasmi shindano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya alhamisi.
 Fredy Kiluswa ambae pia alikuwa mmoja kati ya Washindi watano kutoka Kanda ya Pwani katika Hatua ya kuwatafuta washindi wa Kanda akitoa maneno ya Shukrani mara baada ya kuaga shindano hilo kutokana na uchache wa kura alizopata.
 Baadhi ya washiriki wa kundi la Kwanza wakiwa mbele ya Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) mara baada ya Filamu yao fupi kuonyeshwa.
Mwinshehe Mohamed ambae alikua mmoja kati ya Washindi wa Tatu kutoka Kanda ya Kati mkoa wa Dodoma akitoa pongezi na Maneno ya Shukrani kwa Timu nzima ya TMT mara baada ya kuaga shindano alhamisi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
 Baadhi ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) waliofanikiwa kuingia hatua ya Fainali ambapo mshindi wa Shindano hilo linalotarajiwa kufikia Tamati Mnamo mwisho wa Mwezi wa Nane kwa Mshindi Kukabidhiwa Kitita Cha Shilingi Milioni hamsini za Kitanzani.Picha Zote na Josephat Lukaza - Proin Promotions ltd

Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limefikia hatua ya Mwisho kabisa mara baada ya washiriki kumi bora kupatikana katika Show ya Mchujo iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya Alhamisi.

Show hiyo ya Mwisho katika katika Hatua ya mchujo ilifanyika siku ya Alhamisi na kupelekea Washiriki watatu kutoka Kanda Mbili za Tanzania yaani Kanda ya Kati na Kanda ya Pwani kuondolewa katika Kinyanganyiro hiko na Kupelekea Shindano hilo kubaki na washiriki 10 tu ambao wameingia hatua ya fainali ambapo mshindi mmoja ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika Fainali Kubwa inayotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City siku ya Tarehe 30 Mwezi huu wa Nane.

Washiriki waliondolewa katika Kinyanganyiro Hiko ni Mwinshehe Mohamed ambae alikuwa mmoja kati ya Washindi watatu kutoka Kanda ya Kati ambapo anafanya Idadi ya washiriki wawili kutoka Kanda ya Kati kuondolewa na Kuifanya Kanda ya Kati kuwakilishwa na Mshindi Mmoja katika Fainali hiyo.

 Wengine waliotoka ni Shiraz Ngassa na Fredy Kiluswa ambao wote ni Washindi kutoka kanda ya Pwani Mkoa wa Dar Es Salaam. Kanda ya Pwani walichukuliwa washindi watano huku Shiraz na Fredy wakitimiza idadi ya Washiriki wanne kuondolewa katika kinyanganyiro hiko kwa Kanda ya Pwani, Tishi Abdallah ndie Mshindi mmoja kati ya washindi watano kutoka kanda ya Pwani ambae anaiwakilisha Kanda ya Pwani katika Fainali kubwa ya Shindao la Kwanza na la Kipekee kufanyika Afrika Mashariki na Kati la Tanzania Movie Talents (TMT).

Mpaka Sasa Ni Kanda Moja tu ambayo washindi wake wote watatu ndio wanaiwakilisha Kanda hiyo katika Fainali kubwa itakayofanyika Mwishoni Mwa Mwezi wa Nane katika Ukumbi wa Mlimani city ambapo mshindi mmoja ataondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania huku washindi wote kumi waliofanikiwa kuingia Katika hatua ya Fainali watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions limited ambapo watacheza filamu ya pamoja na Hatimaye kuanza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo inayotarajiwa kutoka Hivi Karibu.

Vipindi vya Shindano hili la Tanzania Movie Talents (TMT) vitaendelea kurushwa katika Kituo cha Runinga cha ITV siku ya Jumamosi Saa 4 Usiku huku marudio yake yakiwa siku ya Jumapili Saa 10 Jioni na Siku ya Jumatano saa 5 usiku.

Ili Kuendelea kumuwezesha Mshiriki wako kuibuka mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kwa Mwaka 2014 unachotakiwa ni kuendelea kumpigia kura kwa wingi kadri uwezavyo kwa Kuandika Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS) Neno TMT acha nafasi ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 halafu tuma kwenda 15678 au unaweza kupiga kura pia kupitia Ukurasa wetu wa Facebook kwa kufungua kiunganishi hiki https://www.facebook.com/tztmt/app_316963748468949

CHADEMA YAKUBALI KUSHIRIKIANA NA ACT-KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

CHAMA  cha  Demokrasia  na  Maendeleo (Chadema) mkoani hapa,kimekubali kushirikiana na vyama vya upinzani kikiwemo chama kipya cha ACT  kwa lengo la kukiondoa madarakani  chama Tawala ambacho ni chachu ya kudumaza huduma za jamii zishio vijijini.
 
Kauli hiyo ni moja ya harakati ya uongozi mpya wa chama hicho kukiri mabadiliko ya mfumo wa vyama vya upinzani  vinahitaji dhati ya mshikamano,uwazi,uwajibikaji  na utoaji wa elimu sahihi ya uraia kwa tija ya umma kubaini uhalisia wa mambo hatimaye kukiondoa chama tawala madarakani 2015.
 
Mwenyekiti wa chadema Mkoa huo  Ally Kisala alisema kukaidi kuviunga mkono vyama vipya ni moja ya mapungufu ya vyama kutokukubali alama za nyakati  ambazo huchangia baadhi ya viongozi wa vyama husika kutumia muda mwingi  kuponda uongozi wa chama kingine ambapo wote wana nia ya kushika dola kwa mujibu wa katiba zao.
 
Kisala alitoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya mwanga center kigoma ujiji,uliokuwa ukitambulisha safu ya uongozi mpya wa chadema na kuelezea wananchi uhai wa chama mkoani hapo na  lengo la  vyama vya upinzani ni kukiondoa ccm kwenye mfumo wa utawala wa miaka kenda usiorasimisha mabadiliko ya  utawala mpya kwa kushindwa  kuwajibikaji kwa viongozi wazembe.
 
“hatunahaja  ya kulumbana,tunataka tuungane ili kukitoa ccm katika madaraka,waliotoka chadema tufanye kazi pamoja ya kuelimisha umma,ili wakati wa uchaguzi mkuu vyama vya upinzani tushike majimbo yote na si kubomoana wenyewe” alianisha Kisala.
 
Katibu wa Chadema wa hapa Shaban Madede aliwataka wakazi wa hapo watumie fursa kwa kuchukua  fomu za  chama hicho kwa  kuomba  nafasi ya kada mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya kitongozi hadi taifa kwa maslai ya kukijenga chama ili kufanikisha ndoto za kuingia ikulu mwakani.
 
Mkurugenzi  wa  Mipango Taifa  Benson  Kigaila alisema chadema taifa  inathamini nguvu za wakazi wa kigoma kwa kujitolea mali na jasho lao katika kukiimarisha chama tangu kuanzishwa kwake ndio maana inatoa nafasi nyingi  kwa wazawa wa hapo kwenye safu ya uongozi taifa na kuwasihi wanachama wazingatie maadili na falsafa ya katiba yao.
 
Pia ,imependekeza kuwa suala la kujadili rasimu ya katiba ifutwe kwa sasa ili fedha mtambukwa zisaidie huhudumia  jamii na kushawishi wananchi ifikapo 2015 wakipe kura chadema ili ishike dola na rasimu ya katiba ifanyike katika mfumo wa utawala wao.
 
Jamboleo liliwahoji  Katibu mwenezi  wilaya ACT wa hapa Anzoluni Kibela    na Katibu wa NRA Taifa Hamis Kiswaga ni kweli wapo tayari kushirikiana kukiondoa madarakani ccm 2015 na kuacha kudoboana majukwaani  kwa nyakati tofauti walisema  ni ndoto  kwa vyama hivyo ,kutokana na sera,itikadi ,utashi na ubinafsi uliopo miongoni mwa  viongozi wa vyama vilivyopo.
 
Walisema baadhi ya viongozi katika vyama wanautashi binafsi na kushawishi jambo Fulani kwa wakati maalum na linapokuja suala la umoja,mshikamano wa kusimika mgombea mmoja katika kiti cha urais ili kukiondoa ccm madarakani huibuka hisia za utashi na  ubinafsi kwa kusalitiana hatimaye ccm inaendelea kuhodhi madaraka  na kushauri wasafiane nia na uwazi wa malengo ili kutimiza hilo.
 
Kwa upande wa Katibu mwenezi CCM wa hapa Kalembe Masudi alisema vyama vya upinzani hawana dhati ya umoja,mshikamano ,kutokana na kushindwa kuwa  na uwazi wa uwajibikaji kwa wanachama wake kwa mujibu wa katiba zao na kudai  ccm itaendela kutawala kutokana na vyama hivyo kuwa na umoja wa mashaka kwa kutawaliwa na ubinafsi na si tija kwa wananchi.

Thursday, August 14, 2014

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA KWANZA WA DIASPORA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

di1
di3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuzindua tovuti rasmi ya Diaspora wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014.
Pamoja naye ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Mwenyekiti wa Taasisi ya Diaspora Bw. Emmanuel Mwachullah (wa pili kulia), Mwana-Diaspora Dennis Londa (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Diaspora Bi. Rose Jairo