DIWANI wa kata ya Businde Said Makala Mkoa wa hapa, ameitaka Halmashauri
ya Manispaa ya Kigoma Ujiji iwachukulie
hatua za kisheria na nidhamu kwa watumishi wa idara ya
Ardhi wanaowahujumu wananchi kwa kuwapa
hati feki za umiliki wa ardhi .
Akizungumza na gazeti hili kigoma Ujiji jana Makala alisema, watumishi wa idara husika
wanachangamoto ya kuwachonganisha wananchi na serikali iliyopo madarakani
kutokana na sintofahamu ya hati sahihi ,ambapo
inachangiwa na madiwani wa hapa kutokuwa wazalendo na adha
zinazowakabili raia husika.
“watendaji na uongozi wa manispaa upo kimya wakati wananchi
wanajenga hatimaye huwatumia mgambo na kubomoa
kwa kuvizia kwa madai wapo kinyume cha sheria, wanahujumu raia wasio na hatia ,utawala
wanaujua ukweli na jamii inafuata taratibu za kupata hati na kulipia
kodi za jengo wahusika si wazalendo” alibainisha Makala.
Zena Tuza ni miongoni mwa wachache waliothubutu kumfuata
diwani huyo na kumpatia hati feki
aliyomilikishwa na manispaa hiyo sanjari na kubomolewa kwa madai amejenga
katika eneo la awali la msitu wa masanga ambapo kwa sasa kaya zinaendelea kujengwa .
Alishauri kuwa, ili kuondoa adha hizo idara husika watumie
mikutano ya hadhara kwa kuwashirikisha madiwani wa manispaa hiyo kwa lengo la
kutoa elimu sahihi na vigezo vya kupatiwa hati miliki iliyo halali na si
kutumia utashi wa kisiasa kuharibu malengo ya jamii na kuitupia lawama serikali
tawala.
Akijibia hilo Mwenyekiti wa kamati ya Fedha
na Mazingira Adam Mussa
alisema wananchi wataendelea
kuvunjiwa makazi kwa uzembe wa kushindwa kubaini maeneo tengwa kwa ajili ya makazi ya watu.
Alisema kutokana na hati aliyotoa muhanga huyo akili ni feki
na kuwataka wananchi wasikubali kuuziwa viwanjwa katika maeneo tengefu na mapori ya
hifadhi wakati huohuo Kaimu meya wa mnispaa hiyo Rashid Yunus alidai watumishi
watakaobainika kufanya hivyo watawajibika.
Yunus alishauri idara ya
ardhi iwe wazi katika uwajibikaji
wake kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu zilizopo kwa lengo
la kuwaondoa walengwa katika changamoto ya kubomolewa makazi sambamba na kutoa elimu
sahihi kwa kuzingatia wiazara husika na
isiwe chanzo cha kuwachonganisha umma na
viongozi.
No comments:
Post a Comment