Na Magreth Magosso,Kigoma
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani hapa,kimekubali
kushirikiana na vyama vya upinzani kikiwemo chama kipya cha ACT kwa lengo la kukiondoa madarakani chama Tawala ambacho ni chachu ya kudumaza
huduma za jamii zishio vijijini.
Kauli hiyo ni moja ya harakati ya uongozi mpya wa chama
hicho kukiri mabadiliko ya mfumo wa vyama vya upinzani vinahitaji dhati ya
mshikamano,uwazi,uwajibikaji na utoaji
wa elimu sahihi ya uraia kwa tija ya umma kubaini uhalisia wa mambo hatimaye
kukiondoa chama tawala madarakani 2015.
Mwenyekiti wa chadema Mkoa huo Ally Kisala alisema kukaidi kuviunga mkono
vyama vipya ni moja ya mapungufu ya vyama kutokukubali alama za nyakati ambazo huchangia baadhi ya viongozi wa vyama
husika kutumia muda mwingi kuponda uongozi
wa chama kingine ambapo wote wana nia ya kushika dola kwa mujibu wa katiba zao.
Kisala alitoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa hadhara
katika viwanja vya mwanga center kigoma ujiji,uliokuwa ukitambulisha safu ya
uongozi mpya wa chadema na kuelezea wananchi uhai wa chama mkoani hapo na lengo la vyama vya upinzani ni kukiondoa ccm kwenye
mfumo wa utawala wa miaka kenda usiorasimisha mabadiliko ya utawala mpya kwa kushindwa kuwajibikaji kwa viongozi wazembe.
“hatunahaja ya
kulumbana,tunataka tuungane ili kukitoa ccm katika madaraka,waliotoka chadema
tufanye kazi pamoja ya kuelimisha umma,ili wakati wa uchaguzi mkuu vyama vya
upinzani tushike majimbo yote na si kubomoana wenyewe” alianisha Kisala.
Katibu wa Chadema wa hapa Shaban Madede aliwataka wakazi wa
hapo watumie fursa kwa kuchukua fomu za chama hicho kwa kuomba nafasi ya kada mbalimbali za uongozi kuanzia
ngazi ya kitongozi hadi taifa kwa maslai ya kukijenga chama ili kufanikisha
ndoto za kuingia ikulu mwakani.
Mkurugenzi wa Mipango Taifa Benson Kigaila
alisema chadema taifa inathamini nguvu
za wakazi wa kigoma kwa kujitolea mali na jasho lao katika kukiimarisha chama
tangu kuanzishwa kwake ndio maana inatoa nafasi nyingi kwa wazawa wa hapo kwenye safu ya uongozi taifa
na kuwasihi wanachama wazingatie maadili na falsafa ya katiba yao.
Pia ,imependekeza kuwa suala la kujadili rasimu ya katiba
ifutwe kwa sasa ili fedha mtambukwa zisaidie huhudumia jamii na kushawishi wananchi ifikapo 2015
wakipe kura chadema ili ishike dola na rasimu ya katiba ifanyike katika mfumo
wa utawala wao.
Jamboleo liliwahoji Katibu mwenezi wilaya ACT wa hapa Anzoluni Kibela
na Katibu wa NRA Taifa Hamis
Kiswaga ni kweli wapo tayari kushirikiana kukiondoa madarakani ccm 2015 na
kuacha kudoboana majukwaani kwa nyakati
tofauti walisema ni ndoto kwa vyama hivyo ,kutokana na sera,itikadi
,utashi na ubinafsi uliopo miongoni mwa viongozi wa vyama vilivyopo.
Walisema baadhi ya viongozi katika vyama wanautashi binafsi
na kushawishi jambo Fulani kwa wakati maalum na linapokuja suala la
umoja,mshikamano wa kusimika mgombea mmoja katika kiti cha urais ili kukiondoa
ccm madarakani huibuka hisia za utashi na
ubinafsi kwa kusalitiana hatimaye ccm inaendelea kuhodhi madaraka na kushauri wasafiane nia na uwazi wa malengo
ili kutimiza hilo.
Kwa upande wa Katibu mwenezi CCM wa hapa Kalembe Masudi
alisema vyama vya upinzani hawana dhati ya umoja,mshikamano ,kutokana na
kushindwa kuwa na uwazi wa uwajibikaji
kwa wanachama wake kwa mujibu wa katiba zao na kudai ccm itaendela kutawala kutokana na vyama hivyo
kuwa na umoja wa mashaka kwa kutawaliwa na ubinafsi na si tija kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment