Baadhi ya wanachama wapya wakivamia jukwaa la ACT katika kiwanja cha cine atlasi manispaa ya kigoma ujiji wakitaka wapewe kadi za chama hicho . |
kaimu mwenyekiti akihutubu madhira yaliyochangia kukihama chama cha chadema katika kiwanja cha cine atlas manispaa ya kigoma ujiji. |
Na Magreth
Magosso,Kigoma
Chama cha Alliance
Transiparency For Change(Act) Mkoa wa Kigoma, kimeahidi kumlinda Mbunge wa Jimbo
la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kwa
gharama zote kutokana na hila zinazofanywa na mahasimu wachache wa chama cha
chadema za kutaka kumwangusha kisiasa.
Pia
wamemshauri afute kesi yake dhidi ya uongozi wa Chadema na kumtaka arudi Kigoma
aungane na ACT kwa ajili ya kukusanya
wanachama katika vijiji vilivyopo hapa kwa lengo la kukuza demokrasia ya uwazi,uwajibikaji wenye tija kwa wananchi .
Akitoa kauli
hiyo kigoma ujiji jana Mjumbe Kamati Kuu Taifa Jaffar Kasisiko katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kiwanja
cha Cine Atlas uliokuwa ukiwakabidhi kadi wanachama wapya kutoka vyama mbalimbali ambapo wanachama hao walichana kadi ,bendera na katiba ya chadema wakidai wameshindwa kukihudumia chadema mkoani hapa.
Alisema
uongozi wa chadema una hila ya kusambaza maneno hasi dhidi ya Zitto Kabwe kwa umma kwa lengo la kulinda maslai yao
binafsi ,badala ya kutetea haki za wanyonge ili kuboresha changamoto zilizopo
kwa tija ya kuondoa fujo na vurugu zinazolinyemelea taifa husika.
“Zitto ni wa
hapa,tutamlinda kwa njia zote na huyu Sabrina Sungura achunge ndimi yake,ni mwanetu
lakini aache fitna asome alama za nyakati ,akumbuke aliyemuweka katika kiti
alichokalia” alibainisha Kasisiko.
Mjumbe
halmashauri kuu Taifa Msafiri Wamalwa alisema ,Mbunge huyo asipoteze muda wa
kulumbana na uongozi wa chadema,badala yake akaifute kesi katika mahakama
husika na aje hapa ili kukijenga chama hicho.
Katibu
mwenezi wilaya ya kigoma Anzoluni Kibela alisema hadi sasa kadi ya kiongozi huyo ipo tayari na kuna wabunge
wapatao 18 wapo tayari kujiunga na chama kwenye uzinduzi ,ambao utafanyika
mkoani hapo mwanzoni mwa mwezi ujao.
Kwa upande
wa Kaimu mwenyekiti Taifa Shaban Mambo aliwasihi wananchi wamuunge mkono mbunge
huyo atakapojiunga na chama hicho, ili aboreshe adha ya usafiri wa njia ya reli
ya kati kwa kuwaletea treni inayotumia umeme kwa gharama zake.
Baadhi ya
wanachama wapya wa ACT aliyekuwa mweka hazina Chadema kigoma ujiji, Hamidu Hamis na Katibu
wilaya Haji Idd kwa nyakati tofauti walisema wamejiunga na ACT
kwa nia ya kuleta mabadiliko ya
umoja,uwazi na uwajibikaji kwa mujibu wa dira ya chama hicho.
No comments:
Post a Comment