Friday, March 21, 2014
Thursday, March 20, 2014
MASHINDANO YA REDD'S MISS TANZANIA KUZINDULIWA
Meneja wa kinywaji cha Redd's Original
Victoria kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam
juu ya kuzinduliwa kwa mashindano ya Redd,s Miss Tanzania 2014kulia ni
mkurugenzi wa kamåuni ya LINO International Hashi Lundenga ambao ni
waandaaji wa mashindano hayo na kushoto ni Meneja Masoko wa kinywaji
cha Redd's Original Vimal Vaghmaria.
Mkurugenzi wa kampuni ya LINO International Hashi Lundenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kuzinduliwa kwa mashindano ya Redd's Miss Tanzania 2014 katikakati ni meneja wa kinywaji cha Redd's Original Victoria Kimaro na mwisho ni Meneja Masoko wa kinywaji cha Redd's Original Vimal Vaghmaria.
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria kwenye uzinduzi jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya LINO International Hashi Lundenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kuzinduliwa kwa mashindano ya Redd's Miss Tanzania 2014 katikakati ni meneja wa kinywaji cha Redd's Original Victoria Kimaro na mwisho ni Meneja Masoko wa kinywaji cha Redd's Original Vimal Vaghmaria.
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria kwenye uzinduzi jijini Dar Es Salaam.
MAWESE KUPANDA BEI KIGOMA!!!
Bidhaa ya Mafuta ya mawese Mkoa wa Kigoma itapanda bei,kutokana
na Halmashauri ya wilaya hiyo, kukabidhiwa mradi wa Kiwanda kidogo cha kisasa cha uchakataji wa mafuta hayo.
Pia kujengwa kwa kiwanda hicho ni shabaha ya kupunguza changamoto ya uchakataji wa awali
ambao ulikuwa ukitumia nguvu na muda mrefu katika uchakataji wake, sambamba na
ubora usio na kiwango cha kuteka soko la
nje.
Akikabidhi mradi kwa Halmashauri,Meneja wa Mradi wa
uhifadhi Ziwa Tanganyika Seleboni Mushi alisema bidhaa hiyo itazidishwa
ubora na hivyo kuweka ushindani wa soko la nje na nchi za Bara la Asia,huku
akitaka halmashauri hiyo watumie sheria,kanuni na taratibu ili kiwanda hicho kiwe endelevu leo na siku zijazo.
Kwa Upande wa wachakataji wa zao hilo Fatuma Hamis na Rajabu Hassan
alisema kiwanda hicho ni tija kwao kutokana na ubora wa jengo na zana za kisasa
ambapo itasaidia kuongeza ujazo wa lita pamoja na ufungaji wa kisasa hali
itakayoongeza kipato kuanzia ngazi ya mkulima na mchuuzi wa mafuta hayo.
“hivi sasa bei ya soko la ndani tunauza dumu la lita 20 kwa
sh.21,000 lakini kupitia hii itapanda zaidi ya hapa kutokana na ubora wake na
kuongezeka kwa lita kutokana na kukamua makapi sahihi” alisema Hamisi
Naye Mgeni rasmi Katibu
tawala wa Mkoa Eng.John Ndunguru alisema ili kulinda mazingira maofisa kilimo
wa wilaya hiyo watumie mabaki ya mawese kwenye mfumo wa mbolea ambayo italeta tija
kwa wakulima wa kijiji hicho .
Mradi huo umefadhiliwa na GEF ,UNDP huku kiasi cha milioni 247.55 kimegharimu ujenzi
wa kiwanda hicho, wakilenga kupunguza changamoto ya uharibifu wa mazingira
katika mfumo wa ucheketaji wa kienyeji ambao hauna tija kwa wakulima na
wacheketaji wa mafuta hayo.
MILIONI 47 ZATUMIKA KUWAPA MOTISHA WALIMU KIGOMA
Na Magreth Magosso,Kigoma
Halmashauri ya Wialaya ya Kigoma vijijini inatarajia kutumia zaidi ya milioni 47 kwa ajili ya motisha kwa Walimu
430 watakaokwenda kufundisha shule zilizopo mwambao wa ziwa Tanganyika na kaskazini kwa tija ya kuboresha viwango vya
ufaulu wa wanafunzi .
Hayo yalisemwa katika kikao
maalum cha wadau wa tasisi za mabenki na
mifuko ya hifadhi ya jamii lengo likiwa
ni kupata maoni ili kuhakikisha changamoto ya walimu kukataa kuishi vijijini ilipungua
na kuboresha ufaulu wa wanafunzi wa
shule za msingi na sekondari ambapo kwa miongo kadhaa imekuwa sintofahamu.
Akizungumzia hilo Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo Miriam Mmbaga alisema katika maeneo ya vijijini kunachangamoto
ya ukosefu wa walimu ambapo wilaya hiyo imepangiwa walimu 300 wa shule za
msingi na walimu 130 shule za Sekondari tatizo hilo litapungua kwa asilimia 50.
Mmbaga alisema kuwa maeneo ya
mwambao wa ziwa walimu 102 watapelekwa katika shule za msingi na walimu 37
sekondari nao watapelekwa huko ambapo waliobaki watapelekwa katika vijiji vya
wilaya hiyo na kueleza kuwa licha ya kupungua kwa changamoto hiyo lakini bado
kunatatizo la ukosefu wa walimu wa masomo ya mchepuo wa Sayansi.
“ Kwa ukanda wa ziwa motisha yao
itakuwa godoro ,taa za sola na redio ya kuchaji ,ukanda wa kaskazini watapewa
taa za solar na redio ili waweze kupata m,awasiliano na jamaa zao sanjari na nyumba bora ya makazi “ alisema Mbaga.
Aidha aliwataka wakuu wa idara
kuondoa urasimu katika maeneo yao ya kazi ili kuweka uwazi na uwajibikaji jambo
litakalowafanya walimu na watumishi waliopo katika maeneo ambayo mazingira ni
magumu waweze kuishi na kufanya kazi kama inavyotakiwa ikiwa ni pamoja na kuwanao
karibu na kuwazungukia mara kwa mara
kujua hali halisi ya maendeleo ya ufundishaji.
Kwa upende wa wadau walichangia kiasi cha
milioni 21 ambapo kila tasisi husika itatoa milioni tatu ili kufanikisha
motisha kwa walimu hao,wakati huohuo halmashauri itatoa milioni 25 ikiwemo usafiri,chakula
na malazi kwa siku tatu ikiwa ni sehemu ya kuwafariji na
kuzoea mazingira halisi ya mkoa huo.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kigalya Husein Kasala alisema changamoto
kubwa inayokabili wakazi wa vijijini ni uhaba wa walimu ukilinganisha na idadi
ya wanafunzi sambamba na ukosefu wa
nyumba bora za walimu hali inayochangia walimu wanaopangiwa kuishi huko
kukimbia.
Alisema ili kudhibiti hali hiyo wananchi wa kijiji chake wamejitolea
nyumba bora nne kwa ajili ya walimu watakaopangiwa kufundisha huko ,wakati vijiji vya Pamila ,Kalya na Kalema wameweka
utaratibu wa kuwachangia walimu mahitaji mbalimbali ikiwemo mchele,samaki,gunia
za mkaa na maharage ili wafundishe vyema.
Aidha tasisi zilizoshiriki
kuchangia ni pamoja na CRDB,NMB,Benki ya Posta,Exim Bank,LAPF,NSSF,PSPF,NHIF,na
kuahidi kukamilisha michango machi,25,2014,ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma
za jamii,huku wadau wakishauri walimu kuzingatia maadili na kuipenda kazi kwa kufuata
kanuni,sheria na taratibu zilizopo.
Tuesday, March 18, 2014
MADINI YA MAGADI SODA KUIINGIZIA TANZANIA SHILINGI BILIONI 480
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa
Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO.
Katikati ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah
Mandwanga, na Mwisho ni ofisa Habari wa Idara
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akifafanua kwa waandishi umuhimu wa mradi wa uchimbaji magadi soda katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Kushoto ni Mhandisi wa mradi Godfrey Mahundi na Kulia ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga. Picha na Georgina Misama – Maelezo.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akifafanua kwa waandishi umuhimu wa mradi wa uchimbaji magadi soda katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Kushoto ni Mhandisi wa mradi Godfrey Mahundi na Kulia ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga. Picha na Georgina Misama – Maelezo.
IMEELEZWA kuwa Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa magadi soda yatakayoingizia taifa Shilingi Bilioni 480 kwa mwaka. Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano na Mawsiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Abel Ngapemba akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Ngapemba alisema hatua hiyo inatokana na kugunduliwa kwa kwa kiasi kikubwa cha madini hayo katika Bonde la Engaruka Wilayani Monduli mkoani Arusha. Alizitaja faida za kugundulika kwa madini ya magadi soda kuwa ni ajira zaidi ya 500 na fedha za kigeni kutokana na mauzo ya madini hayo nje ya nchi.
Alisema kuwa viwanda vinavyotegemea magadi soda kama malighafi ya uzalishaji hali itakayochochea kukua kwa sekta ya viwanda hapa nchini. Ngapemba alibainisha kuwa madini ya magadi soda yanatumika viwandani katika utengenezaji wa bidhaa kama vioo, sabuni, dawa za meno, dawa za hosipitali, uoakaji mikate, kutengeneza karatasi, nguo, na usafishaji wa maji.
Alifafanua kuwa utafiti uliofanywa na wataalamu wazalendo kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 na ulifanyika kwa awamu tatu yakwanza ikiwa ni uchunguzi wa awali na kutafuta maeneo ya kufanyia uchorongaji ili kubaini wingi na ubora wa magadi soda. Alisema kuwa kazi iliyofanywa na kampuni ya OC, ambapo awamu iliyofuata ni kuangalia njia ya uvunaji wa magadi soda hayo iliyofanywa na JSC Service.
"Matokeo ya utafiti huo yameonyesha kuwapo kwa magadi soda kiasi cha mita za ujazo bilioni 4.7 na inakadiriwa kila mwaka wastani wa mita za ujazo milioni 1.9 zinaongezeka katika eneo hilo," alisema Ngapemba na kuongeza: Alisema kuwa NDC itahakikisha kuwa katika utekelezaji wa miradi hii mazingira hayataathiriwa na tunu za taifa zitalindwa ambapo mtazamo wa shirika hilo ni kuwapo kwa mradi wa uvunaji magadi, utalii, na ufugaji.
CHANZO:The Habari.com
MALINZI USIKUBALI TENA KULIPA MILIONI 15 UWANJA WA TAIFA, KUNJUA MAKUCHA KWA WAHARIBIFU WA VITI!!
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
0712461967 au 0764302956
Ligi
kuu soka Tanzania bara inatarajia kuendelea kesho machi 19 mwaka huu
kwa mechi kali ya vuta ni kuvute kati ya mabingwa watetezi, Young
Africans dhidi ya makamu bingwa Azam fc , itakayochezwa Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.
Shirikisho
la soka Tanzania kupitia kwa Afisa habari wake, Boniface Wambura Mgoyo
limesema tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa saa 2 asubuhi
katika magari maalumu .
Vituo
vilivyotajwa ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Ubungo Terminal,
mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Samora/Ohio, OilCom Ubungo, Buguruni
Shell, Dar Live- Mbagala, kituo cha daladala Mwenge na Uwanja wa Taifa.
Wambura
aliongeza kuwa baada ya saa 6 mchana mauzo yote yatahamia Uwanja wa
Taifa ambapo milango kwa ajili ya mechi itakuwa wazi kuanzia saa 7.30
mchana.
Pia
afisa habari huyo alibainisha viingilio katika mechi hiyo kuwa ni sh.
30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati viti vya rangi ya
chungwa, bluu na kijani kiingilio ni sh. 7,000.
Wambura
alimtaja mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam kuwa ndiye
atakayechezesha mechi hiyo, huku akisaidiwa na Anold Bugado (Singida),
Florentina Zablon (Dodoma) na Lulu Mushi (Dar es Salaam).
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa ni Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathimini wa waamuzi ni Alfred Rwiza wa Mwanza.
Rais
wa TFF, Jamal Emil Malinzi kesho utakubali kuingia mfukoni na kulipa
milioni 15 zingine endapo uharibifu utatokea uwanja wa Taifa?
Wakati mechi hiyo ikisubiriwa kwa hamu, kuna baadhi ya mambo yanatakiwa kuangaliwa kwa jicho la tatu.
Siku
za karibuni mashabiki wa klabu za Simba na Yanga wamekuwa wakifanya
vurugu ndani ya uwanja wa Taifa, huku wengine waking`oa viti kuashiria
kupinga baadhi ya mambo yakiwemo maamuzzi ya waamuzi.
Mashabiki wa timu hizi kubwa wamekuwa wakikosa ustaraabu na uvumilivu pale timu zao zinaposhindwa kupata matokeo.
Pia maamuzi ya waamuzi yamekuwa chanzo cha vurugu hizi ambapo mashabiki huwa wanawalaamu marefa kuvurunda.
Kuna wakati kweli waamuzi wanakosea kwa sababu za kibinadamu, kwani hakuna aliyeumbwa mkamilifu.
Linapokuja suala la baadhi yao kufanya maamuzi nje ya sheria 17 za soka, hapo inakuwa ngumu kutafsiri kwanini inakuwa hivyo.
TFF wanatakiwa kuwakumbusha waamuzi kuwa mechi ya kesho ina uzito mkubwa mno katika harakati za ubingwa wa Tanzania bara.
Yanga wanahitaji kushinda ili kupunguza pengo la pointi baina yao na vinara Azam fc.
Mpaka sasa Yanga wao nafasi ya pili kwa pointi 39 nyuma ya Azam waliopo kileleni kwa pointi 43.
Kama Azam fc atashinda kesho
inawezekana ikawa mguu ndani- nje kutafuta ubingwa wake wa kwanza tangu
kuingia ligi kuu msimu wa 2008/2009.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA CHINI
MWENDESHA BODABODA AMGONGA MTU NA KUMVUNJA MGUU,ATIMUA MBIO NA KUTELEKEZA PIKIPIKI
Heri Idd akiwa amelazwa wadi ya majeruhi hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete.(Picha zote na Mpiga picha wetu Mrisho Juma) |
MKUTANO WA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA KUKABILIANA NA MARADHI YASIOAMBUKIZA ZANZIBAR WAFUNGULIWA
Mkurugenzi
wa Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk Mohd J,Dahoma akifungua mkutano
wa Mpango mkakati wa Miaka mitano 2014 hadi 2019 juu ya kukabiliana na
magonjwa yasioambukiza Zanzibar hafla iliofanyika katika Hoteli ya
Zanzibar Ocean View Zanzibar.
Mkuu
wa Kitengo cha maradhi yasio ambukiza Dk,Omar Mwalim akiwasilisha mada
kuhusu Mpango mkakati wa Miaka mitano 2014 hadi 2019 juu ya kukabiliana
na magonjwa yasioambukiza Zanzibar hafla iliofanyika katika Hoteli ya
Zanzibar Ocean View Zanzibar.
Mwakilishi
kutoka Danida tawi la Zanzibar Dr.Jutta katikati akichangia mada kuhusu
kukabiliana na magonjwa yasioambukiza Zanzibar hafla iliofanyika katika
Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar.
Meneja
wa Mradi wa Kumaliza Malaria Zanzibar Abdulla Suleiman wapili kulia
akichangia mada kuhusu kukabiliana na magonjwa yasioambukiza Zanzibar
hafla iliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
Wasiriki
wa Mkutano wa kukabiliana na magonjwa yasioambukiza Zanzibar
wakijadiliana kuhusiana na maswali mbalimbali yaliojitokeza katika
mkutano huo,hafla iliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
Wasiriki wa Mkutano wa
kukabiliana na magonjwa yasioambukiza Zanzibar wakijadiliana kuhusiana
na maswali mbalimbali yaliojitokeza katika mkutano huo,hafla iliofanyika
katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View .(PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO
ZANZIBAR).
THRD YAKUTANA NA WABUNGE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA DODOMA
Mbunge wa Bunge Maalumu la Katiba Bw.James Mbatia akizungumza katika mkutano huo wa Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba na Sekretarieti ya Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu THRD. |
Mbunge wa Bunge Maalumu la Katiba Bw. Tundu Lissu |
Baadhi ya Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba wakisikiliza kwa makini kuhusu Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu namna unavyoweza kufanya kazi hapa nchini. |
Mbunge wa Bunge Maalumu la Katiba Bi.Magdalena Sakaya ambaye kwa nafasi yake alipongeza kuwepo kwa mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu nchini |
Mtandao
wa Watetezi wa Binadamu Wakutana na Waandishi wa habari na Wabunge wa Bunge
Maalumu la Katiba Dodoma.
Sekretariati ya THRDC
Jumapili ya tarehe 16 Machi ilikutana na waandishi wa habari za Bunge Maalumu
la Katiba mjini Dodomakwa ajili ya semina ya uandishi wa habari za watetezi wa
haki za binadamu na pia juu ya masuala kadhaa ambayo watetezi wanataka yawekwe
katika katiba mpya.
Matukio yote mawili
yaliyoandaliwa mjini Dodoma kati ya THRDC na waandishi na lile la wabunge na
Mtandao, yote yaliratibiwa na Bw. Ali Uki ambaye ni mhadhiri wa sheria,
mwandishi wa habari wa zamani.
Mratibu wa Mtandao wa
Watetezi wa Haki za Binadamu Bw. Onesmo Olengurumwa alisema kwamba watetezi wa
haki za binadamu wana haki ya kutambuliwa kikatiba na kulindwa. Alisema kuna
umuhimu wa wanahabari kutoa taarifa nyingi za watetezi kwa umma.
Mgeni
Rasmi Bi Samia Suluhu, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba
Aliishukuru
sekretariati ya THRDC kwa mualiko huo na kusema kwamba kutambuliwa kwa watetezi
wa haki za binadamu kutaisaidia serikali katika utendaji wake. Na pia akaongeza
kwamba majadiliano ni njia yenye nguvu kuliko silaha yoyote.
Aliongeza kwamba
watetezi wa haki za binadamu wanatambuliwa kimataifa kupitia Azimio la Umoja wa
Mataifa lwa Mwaka 1998 juu ya Watetezi wa Haki za Binadamu. Na akasema
kutambuliwa kwao kutaongeza ufanisi katika utawala bora kwa kushirikiana na
taasisi nyingine kama vile mahakama na kwa kuheshimu mikataba mingine ya
kimataifa.
Mkutano
wa Mchana na Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.
Hotuba
ya Mratibu Bw. Onesmo Olengurumwa
Alisema kwamba watetezi
wa haki za binadamu wanakutana na changamoto nyingi katika shughuli zao. Pia
akaongeza kwamba watetezi huongozwa na miito kwa kazi hiyo na wala siyo kwa
vigezo vya vyeti vya kitaaluma. Aliongeza kwamba mkutano huo ulilenga
kuwafahamisha wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba juu ya shughuli za watetezi na
namna ya kuyaingiza masuala yao katika katiba mpya.
Mhe.
Tundu Lissu mtetezi, mwanasheria na mjumbe wa Bunge la Katiba
Aliwashukuru watetezi
kwa kuandaa semina hii lakini akasema waongeze jitiahada zaidi katika mashirika
yao ya haki za biandamu na hata kurekebisha lugha inayotumika katika katiba
yenyewe.
Bw.
James Mbatia Mbunge, Bunge Maalumu la Katiba
Alikosoa kwa kiwango
kikubwa uendeshaji wa haki za baindamu nchini Tanznaia na kuadai kwamba hata
sasa hali hiyo ya ukiukwaju wa hakai za biandamu inajonyesha hata katika Bunge
Maalumu la Katiba lenyewe kwa viongozi kukiuka kanuni zilizotungwa na wabunge
wa Baunge hilo.
Mhe.
Samia Suluhu-Makamu Mwenyekiti Bunge Maalumu la Katiba
Alisema katika kipindi
hiki tayari Taifa la Tanzania limepiga hatua kubwa ya haki za baindamu
ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya mwaka 1992.
Alisema kuwapo kwa
mashirika ya watetezi kama vile HakiElimu, Sikika, HakiArdhi n.k. ni kiashiria
tosha kwa kwamba taifa hili linaziheshimu na kuzitambua haki za binadamu. Alisisitiza kwamba katiba
mpya iwe yenye kuleta baraka kwa sababu imeundwa katika kipindi cha amani.
Prof
Ibrahim Lipumba mjumbe Bunge Maalumu la Katiba
Wakati akifunga mkutano
huo alisema kwamba masuala ya haki za binadamu yasiishie mijini bali yaende
hadi vijijini ambako kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Alishauri kwamba
makundi yanayotetea haki za binadamu yawe na umoja madhubuti kwa sababu Jeshi
la Polisi limekuwa likiwabambikizia kesi wapinzani na watu wengine (wakiwamo
watetezi) ambao kwa kulia au matendo yao huwaudhi watawala.
Sunday, March 16, 2014
ALBINO MBARONI KWA KUMCHUNA NGOZI MTOTO SEHEMU YAKE YA SIRI
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida SACP, Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
MKULIMA
mkazi wa kijiji cha Nkalankala kata ya Mwanga,tarafa ya Nduguti wilaya
ya Mkalama mkoani Singida ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) ,Hidaya
Omari (20),anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumnyonga hadi
kufa, mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka moja na nusu,na kisha
kumchuna ngozi katika sehemu yake ya siri.
Mtoto
aliyenyongwa na kuchunwa ngozi ya sehemu yake ya siri na kutupwa
kwenye kisima cha maji chenye kina cha mita moja,ni Richard Paulo.
Imedaiwa
pia mama yake mzazi na mtuhumiwa Hidaya,Neema Paulo (35), naye
anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kuhusika kumnyonga Daudi Richard
na kumsababishia kifo.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoani Singida,SACP,Geofrey Kamwela,alisema tukio
hilo la kusikitisha,limetokea machi 13 mwaka huu saa moja na nusu
asubuhi huko katika kijiji cha Nkalankala wilayani Mkalama.
Alisema mtoto huyo Daudi,aliokotwa akiwa anaelea juu ya maji ya kisima chenye urefu wa mita moja.
Kamwela
alisema uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi,umebaini kuwa Daudi
(marehemu) aliuawa na kuchunwa ngozi yake na kutumbukizwa katika kisima
hicho.
Alisema
mwili wa marehemu ulipofanyiwa uchunguzi na daktari katika eneo la
tukio na kubaini kuwa kabla ya mauaji jhayo,mtoto huyo alinyongwa shingo
yake.Chanzo cha mauaji hayo,inasadikiwa kuwa ni imani ya kishirikina.
Kamanda
Kamwela alisema mara upelelezi utakapokamilika,watuhumiwa mtu na mama
yake,watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
MISS TABORA 2012 ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO NA KUFURAHIA SIKU YAKE YA KUZALIWA
Mrembo Sarah Paul aliposhiriki furaha yake ya siku ya kuzaliwa na watoto wa kituo cha TZ 820 FPTC NG'AMBO STUDENT CENTER - Kilichopo Tabora.
Mrembo huyo akiongea na watoto
Miss Pauline (Mshindi namba 3 wa chuo cha Utumishi wa Umma-Tabora) akiongea na watoto.
Sarah akikata keki na watoto.
Baadhi ya vitu alivyowaandalia watoto hao na kuvikabidhi kwenye shirika hilo.
Suleiman H. Halletu (Mkurugenzi wa kituo) akishukuru baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Mrembo Sarah kwa ajili ya watoto.
Team nzima iliyomsindikiza mrembo katika hafla hiyo fupi. Kutoka kulia ni Marry, Richard, Miss Zennah (Miss Singida 2012/13), Miss Pauline, Miss Sarah (MissTabora2012), Miss Lilian (Mshindi No2 TPSC 2013), na Annah Henry (Afisa Ugani)
Sarah Paul, mshindi wa shindano la urembo la Redds Miss Tabora 2012, ambaye pia mwaka jana alishiriki katika shindano hilo hadi kufikia fainali za Miss Tanzania.
****
Leo katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa amefanikiwa kuwatembelea watoto wanakusanywa na kanisa la FPCT NG'AMBO wanaopewa msaada na Shirika la Compassion International Tanzania na kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Watoto hawa wanakusanywa kwa lengo la kuwatoa na kuwakomboa umaskini wa kiuchumi, kijamii, kimwili na kiroho na kuwawezesha waje wawe watu wazima wanaojua wajibu wao na kujitegemea.
Pia huwalipia ada, huwauguza na kuwapeleka hosipitali wanapoumwa, huwafundisha ujasiriamali n.k Aliyasema Suleiman H. Halletu mkurugenzi wa kituo kinachoitwa TZ 820 FPCT NG'AMBO STUDENT CENTER na kuongeza kuwa wana watoto 254 katika kituo chao.
ACCESS BENKI YAINGIA KWA KISHINDO TABORA,HOFU YATANDA KWA MABENKI MENGINE!
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Abubakar Mwassa wakati wa ufunguzi wa tawi la benki ya Access mjini Tabora ambalo tayari limeanza kutoa huduma kwa wakazi wa Tabora hasa utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu.
Na Mwandishi wetu, Tabora
WAKAZI wa manispaa ya Tabora na halmashauri zake
zote wameanza kunufaika na huduma za benki ya ACCESS yenye makao yake makuu
jijini Dar es salaam baada ya kuzinduliwa kwa tawi la benki hiyo mkoani humo.
Sherehe za uzinduzi wa tawi hilo jipya zilifanyika
juzi mbele ya ofisi za benki hiyo zilizoko katika jengo la NSSF mjini Tabora
ambapo ziliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwassa aliyeambatana na Mkuu
wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti ya
mkoa.
Akizungumza katika sherehe hiyo, Mwakilishi wa Mkurugenzi
wa benki hiyo kutoka makao makuu jijini Dar es salaam Emanuel Evans alisema
wameanzisha tawi hilo kwa lengo la kuwainua wananchi kiuchumi hususani wakulima
na wajasiriamali wadogowadogo.
Alisema benki hiyo imeanza kutoa huduma zake mkoani
Tabora tangu tarehe 15 Januari mwaka huu na tangu mda huo mpaka sasa wameweza
kutoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 950 kwa wananchi zaidi
ya 400 na wateja wapya zaidi ya 1,800 wamefungua akaunti.
Alisema kitendo cha wananchi kujitokeza kwa idadi
kubwa namna hiyo katika kipindi kifupi cha miezi miwili tu tangu kuanza kwa
huduma za benki hiyo ni jambo la kujivunia sana na benki imeahidi kuendelea
kuwasaidia ili kutimiza ndoto zao kiuchumi.
‘Kuanzishwa kwa tawi la benki hii hapa Tabora ni
habari njema kwa wakazi wote wa mkoa huu na mikoa ya jirani, tunaomba wananchi
wote mjitokeze kwa wingi kufungua akaunti na kujipatia mikopo pasipo usumbufu
wowote, kufungua akaunti ni sh 1000 tu’, alisema.
Katika taarifa yake mwakilishi huyo alisema Access
ni benki iliyodhamiria kuwasaidia Watanzania wenye kipato cha chini na cha kati
na pia imelenga kuwa kimbilio la wananchi wote hapa nchini kwa kuwapatia huduma
bora za kibenki zitakazowainua kimaisha.
Aliongeza kuwa Access Bank Tanzania (ABT) ni benki
ya kibiashara inayokua kwa haraka sana, ilianzishwa mwaka 2007 hapa Tanzania
ikilenga kuwasadia wakulima na wajasiriamali wadogo na wakati ambapo mpaka sasa
ina jumla ya matawi 10 katika mikoa mbalimbali na imeweza kutoa mikopo kwa
zaidi ya wateja 85,000 yenye thamani ya zaidi ya sh bil.325.
Afisa huyo alimwambia Mkuu wa mkoa kuwa ABT
imejiwekea utaratibu uliotofauti na taasisi nyingine hapa nchini ambapo huajiri
vijana wanaomaliza vyuo na kuwapa mafunzo bila kujali uzoefu wao wa kazi lengo
likiwa kuwajengea mshikamano, weredi na utamaduni wa benki.
Mpaka sasa ABT imeajiri wafanyakazi wapatao 600
tangu kuanzishwa kwake hapa nchini wakiwemo wafanyakazi zaidi ya 50 wa tawi la Tabora
jambo linaloifanya benki hiyo kuwa moja kati ya benki zilizoajiri wafanyakazi
wengi zaidi hapa nchini.
Akizungumzia huduma mbalimbali zinazotolewa na benki
hiyo, Evans alisema ABT inatoa mikopo ya kuanzia sh.100,000 hadi sh.900,000
kulingana na uwezo wa mwombaji, mikopo ambayo hutolewa kwa masharti nafuu sana.
Huduma nyingine ni akaunti ya akiba, akaunti ya
hundi, akaunti ya mda maalumu, akaunti ya malengo maalumu, akaunti ya
wanafunzi, akaunti ya wafanyakazi, huduma za utumaji na uhamishaji fedha ndani
na nje ya nchi kwa kutumia M-PESA, WESTERN UNION, TISS na SWIFT.