Pages

KAPIPI TV

Tuesday, March 18, 2014

THRD YAKUTANA NA WABUNGE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA DODOMA

Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba pamoja na Sekretarieti ya Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu wakati wa mkutano wa utambuzi wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini THRD uliofanyika ukumbi wa Dodoma hotel.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu nchini Bw.Onesmo Olengulumwa akitoa ufafanuzi wa mtandao wa THRD na kuwataka wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba kuhakikisha wanaingiza kipengele cha kuwatambua watetezi wa haki za binadamu nchini katika rasimu ya Katiba mpya ambayo inaanza kujadiliwa hivi karibuni Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa Bunge Maalumu la Katiba Bw.James Mbatia akizungumza katika mkutano huo wa Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba na Sekretarieti ya Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu THRD.
Mbunge wa Bunge Maalumu la Katiba Bw. Tundu Lissu
Baadhi ya Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba wakisikiliza kwa makini kuhusu Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu namna unavyoweza kufanya kazi hapa nchini.
Mbunge wa Bunge Maalumu la Katiba Bi.Magdalena Sakaya ambaye kwa nafasi yake alipongeza kuwepo kwa mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu nchini
Mtandao wa Watetezi wa Binadamu Wakutana na Waandishi wa habari na Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba Dodoma.

Sekretariati ya THRDC Jumapili ya tarehe 16 Machi ilikutana na waandishi wa habari za Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodomakwa ajili ya semina ya uandishi wa habari za watetezi wa haki za binadamu na pia juu ya masuala kadhaa ambayo watetezi wanataka yawekwe katika katiba mpya.

Matukio yote mawili yaliyoandaliwa mjini Dodoma kati ya THRDC na waandishi na lile la wabunge na Mtandao, yote yaliratibiwa na Bw. Ali Uki ambaye ni mhadhiri wa sheria, mwandishi wa habari wa zamani.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Bw. Onesmo Olengurumwa alisema kwamba watetezi wa haki za binadamu wana haki ya kutambuliwa kikatiba na kulindwa. Alisema kuna umuhimu wa wanahabari kutoa taarifa nyingi za watetezi kwa umma. 

Mgeni Rasmi Bi Samia Suluhu, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba

Aliishukuru sekretariati ya THRDC kwa mualiko huo na kusema kwamba kutambuliwa kwa watetezi wa haki za binadamu kutaisaidia serikali katika utendaji wake. Na pia akaongeza kwamba majadiliano ni njia yenye nguvu kuliko silaha yoyote.

Aliongeza kwamba watetezi wa haki za binadamu wanatambuliwa kimataifa kupitia Azimio la Umoja wa Mataifa lwa Mwaka 1998 juu ya Watetezi wa Haki za Binadamu. Na akasema kutambuliwa kwao kutaongeza ufanisi katika utawala bora kwa kushirikiana na taasisi nyingine kama vile mahakama na kwa kuheshimu mikataba mingine ya kimataifa.

Mkutano wa Mchana na Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.

Hotuba ya Mratibu Bw. Onesmo Olengurumwa

Alisema kwamba watetezi wa haki za binadamu wanakutana na changamoto nyingi katika shughuli zao. Pia akaongeza kwamba watetezi huongozwa na miito kwa kazi hiyo na wala siyo kwa vigezo vya vyeti vya kitaaluma. Aliongeza kwamba mkutano huo ulilenga kuwafahamisha wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba juu ya shughuli za watetezi na namna ya kuyaingiza masuala yao katika katiba mpya.

Mhe. Tundu Lissu mtetezi, mwanasheria na mjumbe wa Bunge la Katiba

Aliwashukuru watetezi kwa kuandaa semina hii lakini akasema waongeze jitiahada zaidi katika mashirika yao ya haki za biandamu na hata kurekebisha lugha inayotumika katika katiba yenyewe.

Bw. James Mbatia Mbunge, Bunge Maalumu la Katiba

Alikosoa kwa kiwango kikubwa uendeshaji wa haki za baindamu nchini Tanznaia na kuadai kwamba hata sasa hali hiyo ya ukiukwaju wa hakai za biandamu inajonyesha hata katika Bunge Maalumu la Katiba lenyewe kwa viongozi kukiuka kanuni zilizotungwa na wabunge wa Baunge hilo.

Mhe. Samia Suluhu-Makamu Mwenyekiti Bunge Maalumu la Katiba

Alisema katika kipindi hiki tayari Taifa la Tanzania limepiga hatua kubwa ya haki za baindamu ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya mwaka 1992.

Alisema kuwapo kwa mashirika ya watetezi kama vile HakiElimu, Sikika, HakiArdhi n.k. ni kiashiria tosha kwa kwamba taifa hili linaziheshimu na kuzitambua  haki za binadamu. Alisisitiza kwamba katiba mpya iwe yenye kuleta baraka kwa sababu imeundwa katika kipindi cha amani.

Prof Ibrahim Lipumba mjumbe Bunge Maalumu la Katiba

 Wakati akifunga mkutano huo alisema kwamba masuala ya haki za binadamu yasiishie mijini bali yaende hadi vijijini ambako kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Alishauri kwamba makundi yanayotetea haki za binadamu yawe na umoja madhubuti kwa sababu Jeshi la Polisi limekuwa likiwabambikizia kesi wapinzani na watu wengine (wakiwamo watetezi) ambao kwa kulia au matendo yao huwaudhi watawala.

No comments: