Pages

KAPIPI TV

Thursday, March 20, 2014

MAWESE KUPANDA BEI KIGOMA!!!

Na Magreth Magosso,Kigoma

Bidhaa ya Mafuta ya mawese Mkoa wa Kigoma itapanda bei,kutokana na Halmashauri ya wilaya hiyo, kukabidhiwa mradi wa  Kiwanda kidogo cha  kisasa cha uchakataji  wa mafuta hayo.

Pia kujengwa kwa kiwanda hicho ni shabaha ya  kupunguza changamoto ya uchakataji wa awali ambao ulikuwa ukitumia nguvu na muda mrefu katika uchakataji wake, sambamba na ubora usio na kiwango  cha kuteka soko la nje.

Akikabidhi mradi kwa Halmashauri,Meneja wa Mradi wa uhifadhi  Ziwa Tanganyika  Seleboni Mushi alisema bidhaa hiyo itazidishwa ubora na hivyo kuweka ushindani wa soko la nje na nchi za Bara la Asia,huku akitaka halmashauri hiyo watumie sheria,kanuni na taratibu  ili kiwanda hicho kiwe endelevu  leo na siku zijazo.

Kwa Upande wa wachakataji wa zao hilo Fatuma Hamis na Rajabu Hassan alisema kiwanda hicho ni tija kwao kutokana na ubora wa jengo na zana za kisasa ambapo itasaidia kuongeza ujazo wa lita pamoja na ufungaji wa kisasa hali itakayoongeza kipato kuanzia ngazi ya mkulima na mchuuzi wa mafuta hayo.

“hivi sasa bei ya soko la ndani tunauza dumu la lita 20 kwa sh.21,000 lakini kupitia hii itapanda zaidi ya hapa kutokana na ubora wake na kuongezeka kwa lita kutokana na kukamua makapi sahihi” alisema Hamisi

Naye Mgeni rasmi  Katibu tawala wa Mkoa Eng.John Ndunguru alisema ili kulinda mazingira maofisa kilimo wa wilaya hiyo watumie mabaki ya mawese kwenye mfumo wa mbolea ambayo italeta tija kwa wakulima wa kijiji hicho .

Mradi huo umefadhiliwa na GEF ,UNDP huku  kiasi cha milioni 247.55 kimegharimu ujenzi wa kiwanda hicho, wakilenga kupunguza changamoto ya uharibifu wa mazingira katika mfumo wa ucheketaji wa kienyeji ambao hauna tija kwa wakulima na wacheketaji wa mafuta hayo.

No comments: