Na Magreth Magosso,Kigoma
Halmashauri ya Wialaya ya Kigoma vijijini inatarajia kutumia zaidi ya milioni 47 kwa ajili ya motisha kwa Walimu
430 watakaokwenda kufundisha shule zilizopo mwambao wa ziwa Tanganyika na kaskazini kwa tija ya kuboresha viwango vya
ufaulu wa wanafunzi .
Hayo yalisemwa katika kikao
maalum cha wadau wa tasisi za mabenki na
mifuko ya hifadhi ya jamii lengo likiwa
ni kupata maoni ili kuhakikisha changamoto ya walimu kukataa kuishi vijijini ilipungua
na kuboresha ufaulu wa wanafunzi wa
shule za msingi na sekondari ambapo kwa miongo kadhaa imekuwa sintofahamu.
Akizungumzia hilo Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo Miriam Mmbaga alisema katika maeneo ya vijijini kunachangamoto
ya ukosefu wa walimu ambapo wilaya hiyo imepangiwa walimu 300 wa shule za
msingi na walimu 130 shule za Sekondari tatizo hilo litapungua kwa asilimia 50.
Mmbaga alisema kuwa maeneo ya
mwambao wa ziwa walimu 102 watapelekwa katika shule za msingi na walimu 37
sekondari nao watapelekwa huko ambapo waliobaki watapelekwa katika vijiji vya
wilaya hiyo na kueleza kuwa licha ya kupungua kwa changamoto hiyo lakini bado
kunatatizo la ukosefu wa walimu wa masomo ya mchepuo wa Sayansi.
“ Kwa ukanda wa ziwa motisha yao
itakuwa godoro ,taa za sola na redio ya kuchaji ,ukanda wa kaskazini watapewa
taa za solar na redio ili waweze kupata m,awasiliano na jamaa zao sanjari na nyumba bora ya makazi “ alisema Mbaga.
Aidha aliwataka wakuu wa idara
kuondoa urasimu katika maeneo yao ya kazi ili kuweka uwazi na uwajibikaji jambo
litakalowafanya walimu na watumishi waliopo katika maeneo ambayo mazingira ni
magumu waweze kuishi na kufanya kazi kama inavyotakiwa ikiwa ni pamoja na kuwanao
karibu na kuwazungukia mara kwa mara
kujua hali halisi ya maendeleo ya ufundishaji.
Kwa upende wa wadau walichangia kiasi cha
milioni 21 ambapo kila tasisi husika itatoa milioni tatu ili kufanikisha
motisha kwa walimu hao,wakati huohuo halmashauri itatoa milioni 25 ikiwemo usafiri,chakula
na malazi kwa siku tatu ikiwa ni sehemu ya kuwafariji na
kuzoea mazingira halisi ya mkoa huo.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kigalya Husein Kasala alisema changamoto
kubwa inayokabili wakazi wa vijijini ni uhaba wa walimu ukilinganisha na idadi
ya wanafunzi sambamba na ukosefu wa
nyumba bora za walimu hali inayochangia walimu wanaopangiwa kuishi huko
kukimbia.
Alisema ili kudhibiti hali hiyo wananchi wa kijiji chake wamejitolea
nyumba bora nne kwa ajili ya walimu watakaopangiwa kufundisha huko ,wakati vijiji vya Pamila ,Kalya na Kalema wameweka
utaratibu wa kuwachangia walimu mahitaji mbalimbali ikiwemo mchele,samaki,gunia
za mkaa na maharage ili wafundishe vyema.
Aidha tasisi zilizoshiriki
kuchangia ni pamoja na CRDB,NMB,Benki ya Posta,Exim Bank,LAPF,NSSF,PSPF,NHIF,na
kuahidi kukamilisha michango machi,25,2014,ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma
za jamii,huku wadau wakishauri walimu kuzingatia maadili na kuipenda kazi kwa kufuata
kanuni,sheria na taratibu zilizopo.
No comments:
Post a Comment