WATEMBELEA SHULE ZA MSINGI
MRADI WA VIJIJI VYA MILENIA MBOLA
Wafanyakazi wa Mradi wa Vijiji vya Milenia Mbola na wafadhili wa TABLE FOR TWO wakiwa nje ya ofisi ya MVP.
TABLE FOR TWO watembelea baadhi ya wakulima wa kijiji cha Inonelwa kuangalia mafanikio katika sekta ya kilimo.Wanafunzi Shule ya Msingi Ilolangulu wakinawa mikono na kuosha vyombo kwa ajili ya kuchukua chakula cha mchana kinachotolewa shuleni hapo.
TABLE FOR TWO.Alex Talpaert akisaidia zoezi la ugawaji chakula cha mchana shule ya msingi Ilolangulu wakati walipotembelea shule zilizopo eneo la mradi wa vijiji vya Milenia Mbola.
TABLE FOR TWO.Tomoko Kobayashi akipata chakula cha mchana na wanafunzi wa Shule ya Ilolangulu.
TABLE FOR TWO.Aya Miyaguchi akipata ugali maharage na mmoja wa wanafunzi wa darasa la pili.
Wananchi wakipata huduma ya maji safi katika moja ya visima vilivyochimbwa na mradi wa vijiji vya Milenia Mbola katika kijiji cha Inonelwa.
TABLE FOR TWO
KUTEMBELEA MRADI WA
MILENIA MBOLA.
TABORA.
Baadhi ya wafadhili
wa Shirika la kimataifa
la Table For
Two linalojumuisha wadau
kutoka nchi za
Japan,Marekani na China
wametembelea mradi wa
vijiji vya Millenia
Mbola kuangalia maendeleo
ya mpango wa
chakula kwa shule
za msingi zipatazo
kumi na saba
zilizopo eneo la
mradi huo.
Wakiwa katika ziara
ya siku mbili
wafadhili hao ambao
lengo lao kubwa
lilikuwa ni kuangalia
mpango huo wa chakula kwa
shule za msingi,
katika hatua za
awali walitembelea Shule
za msingi za Ilolangulu,Madaha na
Mbola zilizopo eneo
la mradi wa
vijiji vya Milenia.
Katika Shule ya
msingi Ilolangulu wafadhili
hao ambao watatu
wanatokea nchini Japan,mmoja
Marekani na mwingine
nchini China walifika
katika shule hiyo
majira ya saa
sita hadi saa
saba mchana muda
ambao wanafunzi walikuwa
wakiandaliwa kupata chakula
cha mchana na
hivyo kupata fursa
ya kushudia zoezi
la zima la
chakula cha mchana
kwa wanafunzi hao.
Akizungumza na kutolea
ufafanuzi kwa wafadhili
hao,mwalimu mkuu wa
shule ya Ilolangulu
Bi.Hawa Mwamba alisema
kwa kiasi kikubwa
mpango huo wa
chakula shuleni umesaidia
kwa kiasi kikubwa
na hasa kuongeza
mahudhurio kwa wanafunzi
kutoka aslimia 45
hadi asilimia 97.
Aliongeza kwa kusema
kuwa hatua hiyo
pia imesaidia usikivu
kwa wanafunzi wawapo
darasani na hata
kufikia pia matokeo
mazuri kwa ufaulu
kwa wanafunzi wa
darasa la saba
ikilinganishwa na hali
halisi kabla ya
kuanzishwa kwa mpango
huo wa chakula
shuleni.
Mwalimu Hawa aliwaeleza
wafadhili hao kuwa
mpango huo ni
wazo lililotolewa na
Mradi wa vijiji
vya Milenia Mbola
katika kufikia Malengo
manane ya Milenia
na hivyo Mradi
umekuwa ukichangia na
huku wazazi pia
wakitakiwa kuchangia mpango
huo wa lishe
kwa wanafunzi.
Hata hivyo wafadhili
hao wakiongozwa na
Bi.Tomoko Kobayashi kutoka
nchini Japani,walionesha kuridhishwa
kwao na utaratibu
wa mpango huo
ingawa umekuwa ukikabiliwa
na changamoto ya
upungufu wa vyombo
vya kupikia,mishahara kwa
ajili ya wapishi
na sehemu maalumu
ya kulishia chakula
hicho kwa wanafunzi.
Kwa upande wake
mratibu wa mradi
wa vijiji vya
Milenia Mbola Dr.Gerson
Nyadzi alisema mpango
huo wa chakula
shuleni ni moja kati
ya hatua za kuboresha
elimu katika
kutekeleza malengo manane
ya millenia kwa
kushirikisha wakazi wakiwemo
wazazi wa wanafunzi kuchangia
gunia moja la
mahindi unapofika msimu
wa mavuno kwa
kila mwaka.
Aidha Dr.Nyadzi akifafanua
zaidi aliwaeleza wafadhili
hao kuwa mradi
mbali na masuala
ya elimu pia
mafanikio makubwa yamejidhihirisha kwenye
sekta za kilimo,afya
na maji.
Kwa upande wa sekta
ya afya aliweka
bayana kuwa kiwango
cha magojwa ya
Malaria kwa wakazi
wa vijiji vya
millennia Mbola kimepungua
kwa kiasi kikubwa
hali aliyodai kuwa
imetokana na ugawaji
wa vyandarua vyenye
dawa sambamba na
elimu juu ya
matumizi ya vyandarua
hivyo.
Dr.Nyadzi pia alisema
vifo vya kinamama
wajawazito na watoto
chini ya umri
wa miaka mitano
vimepungua kutokana na
elimu ya kuwahimiza
kuhudhuria katika zahanati
zilizojengwa na mradi huo na
pengine wajawazito kujifungulia
hospitalini huku mradi
ukiwa umeweka gari
kwa ajili ya
wagonjwa wanaohitajika kupelekwa
hospitali ya mkoa
wa Tabora.
Aidha kwa upande
wa kilimo Dr.Nyadzi
alizungumzia mafanikio yaliyopatikana ni
pamoja na wakulima
kuongeza mavuno kutoka
wastani wa gunia
tano za mahindi
kwa hekari moja
ya shamba hadi
kufikia mavuno ya magunia
35 kwa hekari
moja hali iliyotokana
na kuwapatia pembejeo
na elimu ya
kilimo cha kisasa
na chenye kuleta
tija kwa mkulima.
Kuhusu suala la
maji Dr.Nyadzi alisema
mpango wa Mradi
ni kuchimba visima
na kuwasogezea karibu
wananchi huduma hiyo
ya maji jambo
ambalo limekwisha fanyika
karibu maeneo yote
ya vijiji vipatavyo
17 vinavyofadhiliwa na
mradi huo.
No comments:
Post a Comment