MGOMO CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TABORA WAMALIZIKA.
''MKURUGENZI MKUU AUNDA TUME KUCHUNGUZA KAULI ZA WALIMU WA CHUO HICHO''
Wanachuo chuo cha Utumishi wa Umma wakati walipokuwa na mgomo wa kutoingia darasani kushinikisha Uongozi wa Chuo hicho kusikiliza madai yao.
Wanachuo Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora wakiendelea na masomo baada ya kumalizika kwa mgomo.
Bw.Saidi Nassor amelazimika kuunda tume hiyo kuchunguza baadhi ya kauli za viongozi ambazo alidai kuwa zimekuwa ni sehemu ya kuwachanganya wanachuo na kuona kana kwamba chuo hakina nia nzuri na wanachuo hao.
Akifafanua zaidi Bw.Nassor alisema chuo tangu kusajiliwa kwake na Nacte kwa ajili ya kuboresha mafunzo tayari kimelazimika kufuata taratibu za baraza hilo ikiwa ni pamoja na mfumo wa utoaji wa vyeti kwa kozi mbali na hasa za ngazi ya Diploma.
Aidha amesema kufuatia hali hiyo madai ya wanachuo yaliyokuwa yakidai kupatiwa cheti cha Diploma ya miaka miwili ni kinyume na utaratibu wa Nacte ambapo kwa utaratibu wa baraza hilo mwanachuo anayetaka kujiunga na chuo hicho akiwa na elimu ya kidato cha nne atasoma kozi ya utunzaji kumbukumbu na katibu muhtasi Diploma kwa muda wa miaka mitatu wakati wale wa elimu ya kidato cha sita watasoma kozi hizo kwa Diploma ya miaka miwili.
Hata hivyo amekiri kuwepo kwa madhaifu katika chuo hicho ambapo baadhi ya walimu wamejigeuza kuwa wasemaji wakuu hali iliyosababisha kuwayumbisha wanachuo waliokuwa wakihitaji ufafanuzi wa taratibu hizo na hivyo kujikuta wakianzisha mgomo wa kutoingia darasani.
''Hatuwezi kulivumilia hilo kwa hiyo ndio maana tumeunda tume huru na ikibainika kuhusika kwa mwalimu yeyote atalazimika atoe ufafanuzi kwa maandishi na kisha taratibu za kinidhamu katika utumishi zitafuata''alisema mkurugenzi huyo.
Aidha kwa mujibu wa mkurugenzi huyo amesema tume hiyo ya watu wanne kutoka nje ya chuo hicho imepewa muda wa siku saba kukamilisha uchunguzi na baada ya matokeo hatua za kinidhamu zitachukuliwa ili kuendelea kulinda heshima ya chuo hicho kilicho chini ya ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa Umma.
Katika hatua hiyohiyo wanachuo wameendelea na masomo na kushiriki shughuli za chuo kama kawaida.
''MKURUGENZI MKUU AUNDA TUME KUCHUNGUZA KAULI ZA WALIMU WA CHUO HICHO''
Wanachuo chuo cha Utumishi wa Umma wakati walipokuwa na mgomo wa kutoingia darasani kushinikisha Uongozi wa Chuo hicho kusikiliza madai yao.
Uongozi wa chuo cha utumishi wa umma.
Walimu Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora wakipata elimu zaidi kuhusu sheria mpya inayohusiana na vyuo nchini kusajiliwa NACTE.Wanachuo Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora wakiendelea na masomo baada ya kumalizika kwa mgomo.
Mkurugenzi mkuu Chuo
cha Utumishi wa
Umma nchini Bw.Said
Nassor ameunda tume
huru kuchunguza kauli
ya baadhi ya
walimu walizozitoa na kusababisha mgomo
kwa wanachuo
wakati wakidai kueleweshwa mabadiliko
ya mfumo juu ya utolewaji
wa kozi mbalimbali kwa
ngazi za diploma.
Bw.Saidi Nassor amelazimika kuunda tume hiyo kuchunguza baadhi ya kauli za viongozi ambazo alidai kuwa zimekuwa ni sehemu ya kuwachanganya wanachuo na kuona kana kwamba chuo hakina nia nzuri na wanachuo hao.
Akifafanua zaidi Bw.Nassor alisema chuo tangu kusajiliwa kwake na Nacte kwa ajili ya kuboresha mafunzo tayari kimelazimika kufuata taratibu za baraza hilo ikiwa ni pamoja na mfumo wa utoaji wa vyeti kwa kozi mbali na hasa za ngazi ya Diploma.
Aidha amesema kufuatia hali hiyo madai ya wanachuo yaliyokuwa yakidai kupatiwa cheti cha Diploma ya miaka miwili ni kinyume na utaratibu wa Nacte ambapo kwa utaratibu wa baraza hilo mwanachuo anayetaka kujiunga na chuo hicho akiwa na elimu ya kidato cha nne atasoma kozi ya utunzaji kumbukumbu na katibu muhtasi Diploma kwa muda wa miaka mitatu wakati wale wa elimu ya kidato cha sita watasoma kozi hizo kwa Diploma ya miaka miwili.
Hata hivyo amekiri kuwepo kwa madhaifu katika chuo hicho ambapo baadhi ya walimu wamejigeuza kuwa wasemaji wakuu hali iliyosababisha kuwayumbisha wanachuo waliokuwa wakihitaji ufafanuzi wa taratibu hizo na hivyo kujikuta wakianzisha mgomo wa kutoingia darasani.
''Hatuwezi kulivumilia hilo kwa hiyo ndio maana tumeunda tume huru na ikibainika kuhusika kwa mwalimu yeyote atalazimika atoe ufafanuzi kwa maandishi na kisha taratibu za kinidhamu katika utumishi zitafuata''alisema mkurugenzi huyo.
Aidha kwa mujibu wa mkurugenzi huyo amesema tume hiyo ya watu wanne kutoka nje ya chuo hicho imepewa muda wa siku saba kukamilisha uchunguzi na baada ya matokeo hatua za kinidhamu zitachukuliwa ili kuendelea kulinda heshima ya chuo hicho kilicho chini ya ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa Umma.
Katika hatua hiyohiyo wanachuo wameendelea na masomo na kushiriki shughuli za chuo kama kawaida.
No comments:
Post a Comment