Pages

KAPIPI TV

Wednesday, August 24, 2011

LHRC - KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU

Wednesday, August 17, 201


"TUTAKWENDA MAHAKAMANI ENDAPO SERIKALI ITAENDELEA NA SUALA HILI"

Wakili Harold Sungusia mkurugenzi wa sera na maboresho kituo cha Sheria na haki za binadam LHRC akitoa tamko kupitia vyombo vya habari kwa niaba ya mkurugenzi wa kituo hicho kuhusu kupinga hatua ya Serikali kuruhusu wawekezaji kuendesha shughuli ya uchimbaji madini ya Uranium ambayo yanatajwa kuwa na athari kubwa kwa maisha ya viumbe hai,uchimbaji huo unatarajiwa kufanyika katika wilaya za Manyoni na Bahi,maeneo ambayo tayari kwa sasa utafiti unafanywa na makampuni ya Uranex Tanzania na Mantrak.

Mfugaji wa ng'ombe katika kijiji cha Mitoo wilayani Manyoni akihojiwa na mkuu wa kitengo kinachoshughulikia wajibu wa mashirika na makampuni wa kituo cha sheria na haki za binadam LHRC Wakili Flaviana Charles wakati alipotembelea wilaya hiyo ambayo kwa sehemu kubwa utafiti na uchimbaji wa madini ya Uranium unafanyika.

 Mfugaji akiwa na hofu juu  ya maisha yake na mifugo baada ya eneo la malisho ya mifugo kuanza kufanyiwa utafiti wa uchimbaji madini ya Uranium eneo la kijiji cha Mitoo wilayani Manyoni mkoani Singida.





Wednesday, August 10, 2011


MADINI YA URANIUM

Mjasiliamali akiandaa chumvi yake baada ya kumaliza shughuli ya kuchimba na kuipika eneo la Chinangali wilayani Manyoni,hata hivyo chumvi hiyo inachimbwa katika eneo linalodaiwa huenda likachukuliwa na mwekezaji kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya Uranium ambayo ni hatari kwa maisha ya viumbe hai.


Baadhi ya wanawake wakibeba mizigo ya kuni kwa ajili ya kupikia chumvi ambayo inatajwa kuwa ni biashara kuu  ya wakazi wa Chinangali wilayani manyoni.
  
Mwanasheria wakili Flaviana Charles  kutoka kituo cha sheria na haki za binadam LHRC akizungumza na mmoja wa wakazi wa Namtumbo kuhusu ushirikishwaji wa wananchi katika uchimbaji wa madini ya Uranium ambayo yanaendelea kufanyiwa utafiti na kuchimbwa katika mbuga ya hifadhi ya Selou wilayani Namtumbo.

No comments: