KIJIJI CHA SHELA, USINGE WILAYANI URAMBO MKOANI TABORA KIMECHOMWA MOTO NA ASKARI WA MALIASILI NA POLISI NA KUZIACHA FAMILIA KADHAA ZIKIWA HAZINA MAKAZI.
Mkazi wa Kitongoji cha Luganjo Mtoni katika Tarafa ya Usinge mkoani Tabora, Bahati Hussein (kulia), akiwa amekaa na familia yake nje ya mabaki ya nyumba yake, baada ya kuchomwa moto na askari wa wanyamapori na polisi agosti 15 mwaka huu kwa madai ya kujenga katika hifadhi. Nyumba 317 zilichomwa na watu 773 hawana mahali pa kuishi wanaishi vichakani.
WATOTO PORINI:-Watoto wakicheza vichakani katika eneo la wazi walipopewa hifadhi na serikali ya kijiji huku wakiwa hawajui hatima yao.
KILIO:-Mama Mlemavu Magreth Jonas akilia kwa uchungu wakati akihojiwa na waandishi wa habari waliofika kushuhudia adha iliyowakumba wananchi hawa.
MAISHA MAPYA:-Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Shela waliochomewa nyumba zao wakiwa wanalala nje porini pasipokujua hatima yao.
CHAKULA:-Mama akipikia nje baada ya nyumba yake kuchomwa moto huku watoto wake wakisubiri chakula kiive tayari kwa mlo wa mchana.
No comments:
Post a Comment