MKAPA ATINGA IGUNGA AZINDUA KAMPENI ZA CCM, ROSTAM ASHANGAZA WALIOFIKIRIA HATOFIKA KWENYE KAMPENI.
*Rais mstaafu wa awamu ya tatu na mwenyekiti mstaafu wa CCM Benjamin William Mkapa akimnadi mgombea ubunge jimbo la Igunga kwa tiketi ya Chama hicho,wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
*Mbunge mstaafu wa jimbo la Igunga akimuombea kura mgombea ubunge wa jimbo
hilo Dr.Peter Kafumu Dallaly wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi mdogo wilayani Igunga.
Kundi la wachkeshaji maarufu nchini ZEKOMEDY nao hawakubaki nyuma katika kampeni hizo ambao walifanya ongezeko la idadi ya watu katika uzinduzi huo. |
KAMPENI IGUNGA ZAANZA KUCHUKUA KASI KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE.
JUMA KAPIPI
TABORA.
Rais mstaafu wa awamu ya tatu na mwenyekiti mstaafu wa Chama cha mapinduzi Benjamini Wiliam Mkapa amezindua kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga na huku akisema kuwa sera ya Chama hicho ya
kujitegemea ndio msingi pekee utakaosaidia kuleta maendeleo ya wananchi na Taifa
zima kwa ujumla.
Rais Mstaafu Benjamini Mkapa akihutubia
umati mkubwa wa wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo wa kampeni hapa wilayani Igunga ,akatumia fursa hiyo pia kuwataka wananchi kuwabeza wapinzani wanaodai kuwa serikali ya ccm hadi hivi sasa haijafanya lolote huku akianisha mafanikio kadhaa yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa sekta mbalimbali zikiwemo za elimu,afya na kilimo.
Amesema serikali ya CCM itaendelea kuwahakikishia huduma
bora wananchi wake ingawa kila jambo linafanyika kwa wakati kulingana na changamoto zinazozikabili sekta mbalimbali na hasa za kiuchumi.
Kwa upande mwngine akatumia fursa hiyo kuumbusha umma wa watanzania
kwa yale mafanikio yaliyopatikana tangu
wakati wa serikali ya awamu ya tatu huku akiyaainisha kuwa ni pamoja na ujenzi
wa Bunge la kisasa la jamhuri ya muungano wa Tanzania,ujenzi wa barabara kwa
kiwango cha lami hatua ambayo pia bado amedai kuwa inaendelezwa na serikali ya
awamu ya nne ambayo kwa sehemu kubwa
imeendelea kuboresha elimu kwa ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma.
Kwa upande wake mbunge mstaafu wa jimbo hilo Bw. Rostam Azizi ambaye ilivumishwa kuwa huenda asinge shiriki katika uzinduzi huo wa kampeni kutokana na hatua ya kujiuzuru kwake,jambo ambalo kwasasa lilikuwa ni kinyume na hivyo akapanda jukwaani kumpigia debe mgombea wa ubunge kupitia chama cha mapinduzi Dr.Peter Kafumu.
Hata hivyo kitendo cha Rostam kupanda jukwaani na kumnadi mgombea wa CCM kimeendelea kuzua minong'ono hapa wilayani Igunga kutokana na ukweli kwamba idadi kubwa ya watu walikuwa bado wanamhitajia kuwa awe mbunge wao na hata kufikia hatua kujiuzuru kwake
Aidha katika uzinduzi huo wa kuanza mbio za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga unaoshirikisha vyama vinane vya siasa,kwa upande wa ccm uzinduzi huo ambao umefanyika katika viwanja vya sokoine ulipambwa kwa ngoma mbalimbali ikiwemo bendi maarufu nchini ya T.O.T ,wasanii maarufu Vick kamata ,Dokii,Afsa kazinja na kundi la orijino komedi toka jijini Dar-es-salaam.
No comments:
Post a Comment