Wakili Harold Sungusia mkurugenzi wa sera na maboresho kituo cha Sheria na haki za binadam LHRC akitoa tamko kupitia vyombo vya habari kwa niaba ya mkurugenzi wa kituo hicho kuhusu kupinga hatua ya Serikali kuruhusu wawekezaji kuendesha shughuli ya uchimbaji madini ya Uranium ambayo yanatajwa kuwa na athari kubwa kwa maisha ya viumbe hai,uchimbaji huo unatarajiwa kufanyika katika wilaya za Manyoni na Bahi,maeneo ambayo tayari kwa sasa utafiti unafanywa na makampuni ya Uranex Tanzania na Mantrak.
Mfugaji wa ng'ombe katika kijiji cha Mitoo wilayani Manyoni akihojiwa na mkuu wa kitengo kinachoshughulikia wajibu wa mashirika na makampuni wa kituo cha sheria na haki za binadam LHRC Wakili Flaviana Charles wakati alipotembelea wilaya hiyo ambayo kwa sehemu kubwa utafiti na uchimbaji wa madini ya Uranium unafanyika.
Mfugaji akiwa na hofu juu ya maisha yake na mifugo baada ya eneo la malisho ya mifugo kuanza kufanyiwa utafiti wa uchimbaji madini ya Uranium eneo la kijiji cha Mitoo wilayani Manyoni mkoani Singida.

No comments:
Post a Comment