Pages

KAPIPI TV

Wednesday, August 26, 2015

JESHI LA POLISI TABORA LAOMBA WATUMISHI WA MUNGU WASAIDIE KUKOMESHA VITENDO VYA MAUAJI YA RAIA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Hamisi Seleman
Na Allan Ntana, Tabora



JESHI la Polisi mkoani Tabora limetoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wachungaji, mapadre, mashekhe, viongozi wa serikali za mitaa, vitongoji na wengineo kusaidia kuelimisha jamii umuhimu wa kudumisha amani katika maeneo yao ili kutokomeza vitendo vya mauaji ya raia.


 Rai hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoani hapa ACP Hamis Selemani alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mauaji ya watu 17 yaliyotokea hivi karibuni katika maeneo mbalimbali mkoani humo.


Alisema vitendo vya mauaji vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku katika maeneo tofauti tofauti chanzo kikubwa kikiwa ni imani za kishirikina, wivu wa kimapenzi, tamaa ya mali na uhasama baina ya familia na familia.


Alieleza kuwa katika kipindi cha siku 15 tu kuanzia tarehe 10 hadi 24 Agosti mwaka huu wananchi wapatao 17 wameuawa kwa kukatwa katwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao matukio ambayo ni ya kusikitisha na yanahatarisha amani ya wananchi kwa kiasi kikubwa.


‘Naomba watumishi wa Mungu wa dini na madhehebu mbalimbali watusaidie kueneza neno la Mungu kwa waumini wao ili wawe na hofu itakayosaidia kukomesha vitendo hivyo vya mauaji ya raia wasio na hatia, naomba sana tushirikiane kurejesha amani katika jamii’, aliasa.


Aidha aliwataka viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo watendaji wa vijiji na kata kusaidia kuelimisha jamii ili kukomesha vitendo hivyo vya kujichukulia sheria mkononi kwani vinachochea uvunjifu wa amani kwa wanajamii.


‘Watu hawana huruma kabisa, hata imani kwa Mungu hawana, wamekuwa kama wanyama, naomba sana ndugu zangu watumishi wa Mungu tushirikiane kuielimisha jamii ili waachane na chuki zisizokuwa na maana, tunataka kukomesha mauaji ya aina zote’, aliongeza.


Aidha Kamanda Selemeni alizitaka taasisi zote za kifedha zilizopo hapa nchini kuhamasisha jamii umuhimu wa kutunza fedha zao benki kwa usalama zaidi kuliko hali ilivyo sasa ambapo wananchi wengi hususani wale wa vijjini wamekuwa na tabia ya kutunza fedha zao majumbani hali inayochochea vitendo vya wizi.


Akizungumzia mauaji yaliyotokea mwishobi mwa wiki Kamanda alisema, mnamo tarehe 23 Agosti mwaka huu katika kitongoji cha Mtakuja kijiji cha Mwanzugi kata ya Nsenda tarafa P wilayani Urambo aliuawa Kashindye Majebele (45) msukuma kwa kukatwa shingo na kisu chenye ncha kali kwa imani za kishirikina.


Katika mauaji hayo msako wa jeshi la polisi ulifanikiwa kumtia nguvuni Hamis Lwangamko (55) msukuma ambaye ni mkulima wa Kamgembya na yupo mahabusu.


Aidha wauaji hao pia inadaiwa waliwaua kwa kuwachoma moto Shija Madobo (80) mkazi wa kijiji cha Kamgembya tarafa ya Urambo wilayani Urambo ambaye ni mume wa Kashinje Majebele, Charles Shija (30) msukuma mkazi wa kijiji cha Msumbiji na Hamis Kingamkono (55) mnyamwezi mkazi wa Kamgembya.


Alitaja watuhumiwa wengine waliokamatwa kwa mahojiano zaidi na jeshi hilo kwa kujichukulia sheria mkononi na kuwaua wenzao kuwa ni  William Seni (68) msukuma mkazi wa kijiji cha Azimio, Paul Maduka (38) msukuma mkazi wa kijiji cha Mtakuja na Zungu Ng’wandu (65) msukuma mkazi wa kijiji cha Kasisi.

HUKUMU YA MMLIKI WA ST. MATHEW YAAHIRISHWA HADI ALHAMISI

court_gavel
Na Mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Mwanzo Kizuiani Mbagala Jijini Dar es Salaam, imeshindwa kutoa hukumu kwenye kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na mkazi wa Singida, Magreth Mwangu dhidi ya Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mathew na St. Marks,Thadei Mtembei.
Katika madai yake ya Msingi, Mwangu anaomba mahakama imuamuru mdaiwa kutoa Sh. Milioni 800 na makazi ya kukaa mdai na watoto wake.
Hakimu wa mahakama hiyo Rajab Tamaambele akiahirisha alisema kwamba mzee mmoja wa mahakama amefiwa.
Mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu hiyo alhamisi ya tarehe 27/10/2015.
Katika kesi hiyo Miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani hapo ni pamoja na Mwangu ambaye alidai kuwa alianza kuishi na Mutembei mwaka 1995 Kongowe Mbagala ambapo mwaka 1998 alikwenda kwa wazazi wa Mwangu kijiji cha Kwaye Iguguno Singida ambapo alitoa mahali na walifunga ndoa ya kimila.
Alisema mtoto wa kwanza alizaliwa mwaka 1998, huku mtoto wa pili akizaliwa mwaka 2000 na mtoto wa tatu 2003
Katika ushahidi wao, watoto wa Mwangu ambao wanasoma katika shule za St Mary’s International na Hijra Seminari ya Dodoma, wamedai kuwa wanasumbuliwa ada na kwamba wanahitaji malezi yote kutoka kwa baba yao.
Watoto hao waliiambia mahakama kuwa, mara ya mwisho kumuona baba yao ni mwaka 2011.
Mtoto wa kwanza wa Mwangu alidai kuwa mwaka 2012 walifika katika Hoteli ya baba yao ya Sleep inn ndipo aliwafukuza na kuwaambia kuwa hawezi kuwalipia ada na badala yake aliwapa S.h 40,000 kila mmoja, fedha ambazo aliziacha mezani.
Pia walidai kuwa Mtembei aliwatolea maneno ya kashfa kwamba hata mama yao aende wapi, anao uwezo na kwamba anajeshi ambalo popote linafika.
Wakati wa ushahidi wake Mutembei alisema alifahamiana na Mwangu wakati akiwa na mfanya usafi katika duka lake la dawa.
Alisema hakuwahi kumuoa mama huyo wala kuishi naye licha ya kuzaa naye watoto watatu.

KIPINDI CHA JUKWAA LANGU. JUMATATU AGOSTI 24, 2015

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Hii ni sehemu ya kwanza ya kipindi kilichosikika Agosti 24, 2015

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Agosti 24, 2015

MFUKO WA LAPF WATOA SHILINGI MILIONI TATU, KUSAIDIA WIKI YA NENDA KWA USALAMA.

 Meneja Masoko wa Mfuko wa  LAPF Kanda ya Mashariki, Yessaya Mwakifulefule (wa pili kulia)  akimkabidhi Katibu wa kamati ya Usalama barabarani kanda maalum,ACP Peter Sima (kushoto), hundi ya thamani ya million tatu  walizotoa kwa ajili yakusaidia vifaa kwa ajili ya wiki ya nenda kwa usalama wanaishuhudia ni mwenyekiti wa kamati hiyo Elifadhili Mgonja (wapili kushoto) na Ofisa Masoko wa Mfuko huo, Rehema  Mkamba.
 Katibu wa Kamati ya Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP),  Peter Sima, akizungumza katika mkutano huo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
Meneja Masoko wa Mfuko wa  LAPF Kanda ya Mashariki, Yessaya Mwakifulefule, akizungumza wakati wa kutoa mchango huo. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

WAZIRI WA FEDHA, SAADA MKUYA SALUM AZINDUA BODI MPYA YA PPF NA MAFAO MAPYA YA MFUKO HUO

 Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya PPF na Mafao Mapya ya Mfuko huo Dar es Salaam jana.
 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum, (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni moja, mwanachama wa mfuko huo, Sara Haule kama malipo ya fao la uzazi katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo sanjari  na uzinduzi wa fao  la uzazi.
 Waziri Fedha, Saada Mkuya akipeana mkono wa pongezi Mwanachama wa mfuko huo , Caroline Kiswaga, baada ya kumkabidhi sh. milioni moja ikiwa ni malipo ya fao la uzazi.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Khijjah (kushoto), akimkabidhi kadi ya kujiunga na huduma mpya za mfuko huo, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, wakati wa  hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini wa mfuko huo Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
 Wajumbe wa Bodi ya PPF ndani ya uzinduzi.
Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, akishangilia katika uzinduzi huo wakati Waziri Saada Mkuya alipokuwa akiwapongeza Mfuko huo kupata tuzo ya hesabu bora.
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Khijjah, akitoa hutuba yake katika uzinduzi huo.
Meneja Kiongozi Mratibu wa PPF, Mbaruku Magawa, akielezea kuhusu fao la uzazi.
 Waziri Saada Mkuya (katikati), na viongozi wengine wakipiga makofi wakati wa uzinduzi huo.
 Uzinduzi ukiendelea.
 Waziri Saada Mkuya Salum, Mwenyekiti wa Bodi ya PPF, Ramadhan Kijjah, na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya PPF.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya PPF na wakina mama waliopata malipo ya fao la uzazi.

Na Dotto Mwaibale

BODI ya Uhasibu NBAA imeipatia tuzo ya hesabu bora Mfuko wa Pensheni wa PPF yenye thamani ya zaidi ya sh.trilioni 2 kutokana kuwa na hesabu bora kati ya taasisi 40 za Serikali na Mashirika ya Umma.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini wa mfuko huo  na Mafao mapya ya mfuko wa Pensheni wa PPF Dar es Salaam jana.

"Nemefurahishwa kwa tuzo hiyo mliyopata hii inaonesha kiashiria cha utendaji uliojaa uadilifu jambo ambalo bila shaka linatoa faraja kubwa kwa wanachama na kuwapa uhakika wa kupata pensheni zao wakati utakapowadia" alisema Salum.

Salum alisema hatua hiyo ya mafanikio ya mfuko huo imethibitisha kuwa taasisi za umma zinaweza kufanya kazi kiasi cha kuwa mfano wa kuigwa kinyume cha dhana potofu iliyopo katika jamii kuwa Serikalini na katika mashirika na taasisi za umma kumejaa ubabaishaji.

Alisema tija na tuzo za kimataifa ilizopata mfuko huo sio tu vinafaida kwa mfuko na wanachama bali pia kwa uchumi wa nchi ya Tanzania na na ni fahari kwa nchi katika medani ya kimataifa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa mfukio huo, Ramadhan Khijjah alisema thamani ya mfuko huo imeongezeka kwa zaidi ya sh.trilioni moja ndani ya miaka mitatu kutoka sh. bilioni 859.5 mwezi Septemba 2011 hadi kufikia sh.trilioni 2.1 mwezi Juni mwaka huu.

Alisema mfuko huo umeweza kupata mapato yatokanayo na uwekezaji ya jumla ya sh. bilioni 318 mwaka 2013 na sh. 496.5 bilioni mwaka 2014/ 2015 ambapo ni sawa na asilimia 22 na 26.

Alisema hali hiyo imejidhihirisha kuwa mfuko umefanya uwekezaji wenye tija kwa kuzingatia kuwa mfumuko wa bei katika kipindi hicho ulikuwa na wastani wa asilimia 7.9 na 5.7.

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAZINDUA KAMPENI YA 'CHAGUA TIGO PESA, INALIPA

 Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi katika uzinduzi wa kampeni ya ya Chagua Tigo Pesa, Inalipa. Kulia ni Meneja  Bidhaa wa Tigo, William Mpinga.
 Meneja  Bidhaa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya simu ya mkononi ya tigo Tanzania imezindua Kampeni iitwayo"chagua tigo pesa,inalipa"ikiwa na lengo na la kuongeza upatikanaji wa fedha kwa njia ya simu ya mkononi kwa wateja.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Ruan Swanepoel alisema huduma hiyo ikiwa na muonekano mpya na sura kwa wateja wake wanaotumia huduma ya tigo pesa Tanzania nzima.

Alisema kuwa kwasasa mtandao wa tigo umeenea kwa wingi hapa nchini na unatumiwa na asilimia 90 ya wananchi wote wanaomiliki simu za mkononi.

Alisema kuwa mtandao wa tigo unakikisha inatoa huduma stahiki kwa wateja wakena kuhakikisha huduma ya tigo pesa inazidi kuwa na huduma pendwa kwa sababuinapatikana kirahisi na makini.

Alisema kuwa huduma hii inalipa kwa wateja wake na kukopa fedha hasa kwa wale wenye kipato kidogo na wasio na huduma za kibenki.

Alifafanua kuwa wateja wa tigo pesa watanufaika na kampeni hii kwa kuypata vifurushi vya bure kila wannunuapo bidhaa na kulipia kwa tigo pesa kutoka kwa wauzaji waliosajiliwa.

Pia aliongeza na kusema kuwa wateja watapata riba kila baada ya miezi mitatu kulingana na kiasi cha fedha ya kifurushi ambacho mteja atamnunulia mtu mwingine kwa tigo pesa.

MISATAN TO HOLD RTIWORKSHOP FOR SELECTED BLOGGERS AND EDITORS



MISATAN to sharpen Bloggers & Editors’ skills on RTI, Election Reporting
By Gasirigwa GS

The Media Institute of Southern Africa (MISA) Tanzania Chapter in association with the Centre for ICT Policy promotion in Africa (CIPESA) will tomorrow train a selected number of bloggers and editors on Right to Information with special focus on this year’s general election.

Editors and bloggers will be taught on the safest ways to access information and report responsibly during campaigns and the entire election period. Attention will be directed to the Cyber crime and the Statistics Acts which are already in effect and have dire consequences on media practice.

Participants will also be introduced to ‘The Broadcasting Services (Content) (The Political Party Elections Broadcasts) Code 2015’ which was gazetted on June 26, 2015. Bloggers, SMS pollsters, and broadcasters in general will seriously be affected by this Code. The Code was developed by the Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA).

About 20 selected Dar es Salaam-based editors and bloggers have confirmed to take part in this one-day workshop, scheduled for tomorrow Thursday the 27th of August at Kebbys Hotel in Dar es Salaam.

Similar training was held two weeks ago in Mwanza and drew participants from Geita, Mara and Mwanza itself. The Mwanza training specifically targeted journalists who basically cover rural areas.


MISATAN and CIPESA believe that the media needs to responsibly serve the public in a way that will provoke positive engagement and subsequent improvement in the political administration of the country.

Monday, August 24, 2015

HUKUMU YA KESI YA TALAKA NA MGAWANYO WA MALI YA MWENYE SHULE ZA ST MATHEW KESHO

court_gavel
Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya Mwanzo Kizuiani Mbagala Jijini Dar es Salaam, kesho, Oktoba 25 inatarajia kutoa hukumu kwenye kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na mkazi wa Singida, Magreth Mwangu dhidi ya Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mathew na St. Marks,Thadei Mtembei.

Katika madai yake ya Msingi, Mwangu anaomba mahakama imuamuru mdaiwa kutoa Sh. Milioni 800 na makazi ya kukaa mdai na watoto wake.
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Rajab Tamaambele.
Miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani hapo ni pamoja na Mwangu ambaye alidai kuwa alianza kuishi na Mutembei mwaka 1995 Kongowe Mbagala ambapo mwaka 1998 alikwenda kwa wazazi wa Mwangu kijiji cha Kwaye Iguguno Singida ambapo alitoa mahali na walifunga ndoa ya kimila.
Alisema mtoto wa kwanza alizaliwa mwaka 1998, huku mtoto wa pili akizaliwa mwaka 2000 na mtoto wa tatu 2003
Katika ushahidi wao, watoto wa Mwangu ambao wanasoma katika shule za St Mary’s International na Hijra Seminari ya Dodoma, wamedai kuwa wanasumbuliwa ada na kwamba wanahitaji malezi yote kutoka kwa baba yao.
Watoto hao waliiambia mahakama kuwa, mara ya mwisho kumuona baba yao ni mwaka 2011.
Mtoto wa kwanza wa Mwangu alidai kuwa mwaka 2012 walifika katika Hoteli ya baba yao ya Sleep inn ndipo aliwafukuza na kuwaambia kuwa hawezi kuwalipia ada na badala yake aliwapa Sh 40,000 kila mmoja, fedha ambazo aliziacha mezani.
Pia walidai kuwa Mtembei aliwatolea maneno ya kashfa kwamba hata mama yao aende wapi, anao uwezo na kwamba anajeshi ambalo popote linafika.
Wakati wa ushahidi wake Mutembei alisema alifahamiana na Mwangu wakati akiwa na mfanya usafi katika duka lake la dawa.
Alisema hakuwahi kumuoa mama huyo wala kuishi naye licha ya kuzaa naye watoto watatu.

"BAADHI YA WATANZANIA WASIKITISHWA NA KAULI YA MKAPA KWENYE UFUNGUZI WA KAMPENI YA CCM"

Kufuatia kauli ya Rais Mstaafu wa  Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania awamu ya tatu aliyoitoa katika ufunguzi wa kampeni ya Urais kama inavyoonesha na kusikika katika video hii viwanja vya Jangwani jijini Dar-es-Salaam hapo jana,baadhi ya watanzania katika maeneo mbalimbali ya nchi wameipokea kauli hiyo kwa hisia tofauti na kudai kuwa si ya kuridhisha kwakuwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki shughuli za kisiasa na kuelezea hisia zake katika kufikia lengo la kuleta ukombozi wa namna mbalimbali ikiwemo wa kiuchumi, kisiasa na kijamii  ilimradi asivunje sheria.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ambayo ilikuwa baadhi ya wananchi walikuwa wakijaribu kupashana habari mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo la Uzinduzi wa kampeni ya CCM  ambalo lilikuwa likirushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni nchini Tanzania,Wananchi walionesha kupingana na kauli za kiongozi huyo mkubwa aliyewahi kuwa Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania na kusema kuwa ni vema hata angeishia kubeza kauli zinazotolewa na viongozi wa vyama vya Upinzani lakini si kuwaita WAPUMBAVU NA MALOFA kwakuwa tamko hilo Watanzania wamelitafsiri kuwa ni tusi ambalo limeweza kuwakera sana hasa nyakati hizi za kuelekea Uchaguzi mkuu.

Hata hivyo wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania na wanaofuatilia kwa karibu zaidi mienendo ya wananchi wanavyoichukulia siasa kwa sasa,wamesema kauli ya kiongozi huyo huenda ikaleta madhara makubwa kisiasa kwa namna ambavyo imepokelewa na Watanzania ambao wamekuwa na mwamko  mkubwa juu ya kufuatilia masuala ya kisiasa na kuvutiwa zaidi na kuhitaji mabadiliko nchini Tanzania.  

 

UN KUBORESHA VYOO VYA SHULE 10 KILIMANJARO

IMG_4176
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu mara baada ya kuwasili katika shule ya msingi Kiboriloni kwa ajili ya kushiriki zoezi la kuweka msingi kwenye ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo. Kulia kwake ni Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu, Moshi
MASHIRIKA ya Umoja wa Mataifa nchini, yatasaidia kuboresha vyoo katika shule 10 zilizopo katika manispaa ya Moshi na wilaya ya Moshi vijijini.
Hayo yalisemwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye hafla ya kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi wa matundu 18 ya choo katika shule ya msingi Kiboriloni.
Alisema pamoja na mashirika hayo kusaidia uboreshaji huo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, amewataka watoto kukumbuka kutunza mazingira na miili yao kama sehemu ya mazingira hayo.
Aidha aliwataka wanafunzi kuhakikisha kwamba wanajenga mshikamano mkubwa na wenye upendo kila kundi likithamini kundi jingine kwa ajili ya ustawi wa taifa .
Alisema wasichana kwa wavulana kuheshimiana kwani katika hilo wataweza kutengeneza taifa linaloheshimiana na hivyo kulinda msingi wa maisha wa amani unaowezesha maendeleo na ustawi wa jamii.
Aliwataka wanafunzi hao kushikilia ndoto zao na kusaidia kutambua kwamba wanahitajika kutunza mazingira na kujali afya zao.
IMG_4174
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem aliyeambatana na Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu wa shule ya msingi Kiboriloni.
Akimkaribisha Mratibu huyo kuzungumza na wanafunzi mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Kiboriloni Salehe Msuya alisema kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1946 eneo la Msaranga na kuitwa kwa jina hilo na baadae kuhamishiwa Kiboriloni ambako kulikuwa na makazi ya Mangi mwaka 1955 inakabiliwa na ukosefu wa matundu 18 ya choo, maktaba na bwalo la chakula.
Alisema ingawa shule ilianzishwa ikiwa na wanafunzi 12 ilipohamishiwa Kiboriloni 1955 na kupewa jina hilo mwaka 1990, sasa ina wanafunzi 613 kuanzia darasa la awali hadi la 7 na kukabiliwa na changamoto za matundu.
Shule hiyo inahitaji kuwa na matundu 32 lakini yaliyopo sasa ni 14.
Mwalimu huyo aliishukuru UN kwa kuwasaidia kutengeneza matundu yaliyobaki na kuwaomba pia kusaidia kuboresha mazingira ya kusomea katika kuwa na maktaba na bwalo la kulia chakula.
Kwa sasa shule hiyo inatoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wake na hawana mahali pa kulia.
Pamoja na taaluma kuzidi kuimarika shuleni hapo, shule haina maktaba.
IMG_4181
Maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwasili kwenye eneo la tukio ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_4625
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kuweka msingi wa ujenzi wa vyoo 18 ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira bora ya kusomea sambamba na maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_4602
Sehemu ya wanafunzi wa shule msingi Kiboriloni wakifurahi habari za kujengewa vyoo.
IMG_4159
Wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni wakinawa mikono yao kwa sababu mara baada ya kutoka msalani kama walivyokutwa na camera ya modewjiblog
IMG_4569
Baadhi ya vyumba vya vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni.
IMG_4184
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) akiwapungia wanafunzi wa shule msingi Kiboriloni (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili shuleni hapo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_4192
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akiweka maji wakati wa maandalizi ya kutengeneza zege kwa ajili ya kuweka msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakisubiri kuchanganya zege.
IMG_4198
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) wakianza matayarisho ya kuchanganya zege huku Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Martha Ofunguo akimwaga maji kwenye mchangayiko huo.
IMG_4207
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakiendelea na zoezi la kuchanganya zege.
IMG_4210
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakishiriki zoezi la kubeba maji na kokoto kwa ajili ya kuchanganya zege la msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni.
IMG_4215
IMG_4217
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akishuhudia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati akimwaga zege waliloandaa kwenye ujenzi wa msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni.
IMG_4225
Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Titus Osundina (kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakishiriki zoezi la kumwaga zege katika msingi huo.
IMG_4252
Hapa ni kazi tu.....; Ni maneno ya Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu wakati akishiriki zoezi la kuchanganya zege katika shule msingi Kiboriloni. Kwa matukio zaidi Bofya hapa

BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI MAREKANI MHE, WILSON MASILINGI AWASILI WASHINGTON DC

    Balozi mpya atakayeiwakilisha Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi akiwa amefuatana  na Mkewe  Marystella Masilingi pamoja na mwanae Nelson Masilingi wawasili kituoni kwake Washington DC, awali ya hapo Mhe Wilson Masilingi alikua Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi.
Mhe Wilson Masilingi mara baada ya kutua Washington DC akisalimiana na atakayekua dereva wake Virgilio Paz maarufu kama Bong.
Safari ya Mheshimiwa Balozi pamoja na mama ikianza kuelekea Hotelini kwake ambapo atapumzika kwa muda kabla ya kuingia nyumbani kwake Bethesda ,Maryland.
Mhe Wilson Masilingi mara baada ya kufika Hotelini kwake akisaidiwa mlango na Afisa wa Ubalozi Swahiba Habib Mndeme.
Mhe Balozi Wilson Masilingi akisalimiana na baadhi ya Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliofika kumlaki pichani ni mmoja wa Maafisa Andrew Mugendi Zoka.
Mama Marystella Masilingi naye hakua nyuma kusalimiana na baadhi ya Wafanyakazi na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania.
Mhe Wilson Masilingi akiwa na bashasha tele kuona kwa jinsi gani Tanzania House walivyo na upendo na kuonyesha ushirikiano wao wa dhati kwenye tukio hilo muhimu.
Mhe Wilson Masilingi alifuatana na Mtoto wake Nelson Masilingi.
Maafisa wa Ubalozi Swahiba Mndeme pamoja na Alfred Swere wakiteta jambo kidogo.
Mhe Balozi Wilson Masilingi pamoja na Familia yake kwenye picha  ya pamoja na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta.
Mhe Wilson Masilingi alipata fursa kidogo kutembelea mitaa ya jijini akiwa ameongozana na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta

Baadhi ya Wafanyakazi na Maafisa wa Tanzania House wakiwa Hotelini alipofikia Mhe Wilson Masilingi.

   PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI KWA PICHA ZAIDI UNGANA NASI PUNDE.