Pages

KAPIPI TV

Wednesday, August 26, 2015

HUKUMU YA MMLIKI WA ST. MATHEW YAAHIRISHWA HADI ALHAMISI

court_gavel
Na Mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Mwanzo Kizuiani Mbagala Jijini Dar es Salaam, imeshindwa kutoa hukumu kwenye kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na mkazi wa Singida, Magreth Mwangu dhidi ya Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mathew na St. Marks,Thadei Mtembei.
Katika madai yake ya Msingi, Mwangu anaomba mahakama imuamuru mdaiwa kutoa Sh. Milioni 800 na makazi ya kukaa mdai na watoto wake.
Hakimu wa mahakama hiyo Rajab Tamaambele akiahirisha alisema kwamba mzee mmoja wa mahakama amefiwa.
Mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu hiyo alhamisi ya tarehe 27/10/2015.
Katika kesi hiyo Miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani hapo ni pamoja na Mwangu ambaye alidai kuwa alianza kuishi na Mutembei mwaka 1995 Kongowe Mbagala ambapo mwaka 1998 alikwenda kwa wazazi wa Mwangu kijiji cha Kwaye Iguguno Singida ambapo alitoa mahali na walifunga ndoa ya kimila.
Alisema mtoto wa kwanza alizaliwa mwaka 1998, huku mtoto wa pili akizaliwa mwaka 2000 na mtoto wa tatu 2003
Katika ushahidi wao, watoto wa Mwangu ambao wanasoma katika shule za St Mary’s International na Hijra Seminari ya Dodoma, wamedai kuwa wanasumbuliwa ada na kwamba wanahitaji malezi yote kutoka kwa baba yao.
Watoto hao waliiambia mahakama kuwa, mara ya mwisho kumuona baba yao ni mwaka 2011.
Mtoto wa kwanza wa Mwangu alidai kuwa mwaka 2012 walifika katika Hoteli ya baba yao ya Sleep inn ndipo aliwafukuza na kuwaambia kuwa hawezi kuwalipia ada na badala yake aliwapa S.h 40,000 kila mmoja, fedha ambazo aliziacha mezani.
Pia walidai kuwa Mtembei aliwatolea maneno ya kashfa kwamba hata mama yao aende wapi, anao uwezo na kwamba anajeshi ambalo popote linafika.
Wakati wa ushahidi wake Mutembei alisema alifahamiana na Mwangu wakati akiwa na mfanya usafi katika duka lake la dawa.
Alisema hakuwahi kumuoa mama huyo wala kuishi naye licha ya kuzaa naye watoto watatu.

No comments: