Pages

KAPIPI TV

Monday, August 24, 2015

"BAADHI YA WATANZANIA WASIKITISHWA NA KAULI YA MKAPA KWENYE UFUNGUZI WA KAMPENI YA CCM"

Kufuatia kauli ya Rais Mstaafu wa  Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania awamu ya tatu aliyoitoa katika ufunguzi wa kampeni ya Urais kama inavyoonesha na kusikika katika video hii viwanja vya Jangwani jijini Dar-es-Salaam hapo jana,baadhi ya watanzania katika maeneo mbalimbali ya nchi wameipokea kauli hiyo kwa hisia tofauti na kudai kuwa si ya kuridhisha kwakuwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki shughuli za kisiasa na kuelezea hisia zake katika kufikia lengo la kuleta ukombozi wa namna mbalimbali ikiwemo wa kiuchumi, kisiasa na kijamii  ilimradi asivunje sheria.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ambayo ilikuwa baadhi ya wananchi walikuwa wakijaribu kupashana habari mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo la Uzinduzi wa kampeni ya CCM  ambalo lilikuwa likirushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni nchini Tanzania,Wananchi walionesha kupingana na kauli za kiongozi huyo mkubwa aliyewahi kuwa Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania na kusema kuwa ni vema hata angeishia kubeza kauli zinazotolewa na viongozi wa vyama vya Upinzani lakini si kuwaita WAPUMBAVU NA MALOFA kwakuwa tamko hilo Watanzania wamelitafsiri kuwa ni tusi ambalo limeweza kuwakera sana hasa nyakati hizi za kuelekea Uchaguzi mkuu.

Hata hivyo wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania na wanaofuatilia kwa karibu zaidi mienendo ya wananchi wanavyoichukulia siasa kwa sasa,wamesema kauli ya kiongozi huyo huenda ikaleta madhara makubwa kisiasa kwa namna ambavyo imepokelewa na Watanzania ambao wamekuwa na mwamko  mkubwa juu ya kufuatilia masuala ya kisiasa na kuvutiwa zaidi na kuhitaji mabadiliko nchini Tanzania.  

 

No comments: