Kiwanja kipya cha maraha Uefa Goo Night Club kiko tayari kuzinduliwa leo katika mkesha wa sikukuu ya Krismas jijini Dar es salaam Kiwanja hiki ni cha Kisasa sana kama utakavyoona taswira zake zikionyesha maeneo mbalimbali ndani ya klabu hiyo ambayo iko maeneo ya Ukonga Mombasa Barabara ya kuelekea Moshi Baa Karibu na njia panda ya Mahita mita 200 kutoka barabara kuu iendayo Pugu, siku ya katika siku ya mkesha wa Krismas burudani kibao zimeandaliwa na kiwanja hicho kikamilika kila kitu ili kuwapa burudani wateja wake ikiwa ni pamoja na Ligi mbalimbali za ulaya, muziki wa kisasa kama vile Bongofleva, Zuku, Bolingo na miziki mingine mingi ambapo pia vyakula mbalimbali vitapatikana. Hii ndiyo mandari yake kwa ndani Injinia wa sauti akiweka sawa mambo yake Kaunta ikiwa imesheheni vinywaji mbalimbali tayari kwa kutoa huduma kwa wateja, Kaunta ya chini nayo ikiwa imesheheni vinywaji.
Wednesday, December 24, 2014
ALEX MSAMA AMWAGA ZAWADI ZA KRISMAS KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Bi. Honorata wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Honorata kilichopo Temeke jijini Dar es salaam leo wakati alipokabidhi msaada wa vyakula kwa vituo mbalimbali vya jijini Dar es salaam ikiwa ni zawadi yake ya sikukuu ya Krismas kwa vituo hivyo, Bw. Alex Msama amesema pia katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika kesho wakati wa sikukuu ya Krismas mkoani Mbeya, kiasi cha fedha zitakazopatikana zitakwenda kulipia ada za watoto yatima katika vituo mbalimbali vitakavyofikiwa na msaada huo, Ameongeza kwamba msaada huo wa vyakula una thamani ya shilingi milioni Nne na Nusu.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Bi. Halima Mpeta wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Bw. Rashid Mpinda katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre cha Kinondoni. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akigwa vyakula mbalimbali baada ya kukabidhi kwa vituo vya kulelea watoto yatima jijini Dar es salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo kwa wanahabari mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa vituo vya kulelea watoto yatima jijini Dar es salaam.
UNIC YAELIMISHA SIKU YA CHOO KWA VIJANA WALIO NJE YA SHULE
Siku ya choo duniani ambayo huadhimishwa tarehe 19 Novemba. UNIC waliadhimisha siku hii kwa kuwakutanisha vijana walioko nje ya shule tarehe 23 Desemba 2014 kwa lengo la kuwaelimisha na kuwahamasisha utumiaji wa vyoo ili na wao waweze kuelimisha jamii zinazowazunguka juu ya umuhimu wa kuwa na vyoo.
Tukio hili liliwakutanisha vijana toka vikundi 5: Azimio Youth Group, Makangarawe Youth Development Fund, Mashine Ya Maji Youth Development Centre,Temneke Youth Development Foundation na Tanzania Youth Development Society. Yafuatayo ni baadhi ya matukio katika picha.
Vijana wakiwa katika makundi kujadili na kuweka mikakati watakavyosaidia jamii kuhusu utumiaji wa vyoo na usafi wa mazingira.
Afisa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma-Ledama akitoa mada kuhusu siku ya Choo duniani pamoja na umuhimu wa utumiaji vyoo, na kampeni maalumu ya uhamasishaji wa kuwa na vyoo.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za Vijana Temeke (Temeke Youth Development Network -TEYODEN), Ismail Mnikite akitambulisha vijana waliohudhuria kutoka makundi mbalimbali.
Baada ya majadiliano, vijana wakiwasilisha maazimio na mikakati waliyoyakusudia kufanya ndani ya vikundi vyao katika jamii zinazowaunguka.
CHANGAMOTO YA UCHAFUZI WA MAZINGIRA-MWANZA
Na Kibada Kibada -Mwanza
MWALO.
Wafanyabiashara ya samaki na bidhaa nyingine
za maliasili katika soko la samaki la Mwalo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemeala
Jijini Mwanza wako hatarini kupatwa na Magonjwa ya mlipuko hasa wakati huku mvua
zinazoendelea kunyesha kutokana na changamoto ya uchafuzi wa mazingira uliopo
katika soko hilo.
Mbali ya uchafuzi huo pia zipo changamoto nyingine
za uhaba wa vitendea kazi na miundo
mbinu mibovu ya kutolea maji kwenye meza za kupokelea samaki pamoja na
mrundikano wa taka ngumu na taka nyepesi katika maeneo mbalimbali ya Soko
hilo la Mwalo wa Samaki.
Upungufu wa vitendea kazi kwa wafanyakazi wanashughulikia
usafi katika soko hilo hasa samaki ambapo wafanyakazi wanaparua samaki bila
kuwa kinga yeyote kwenye mikono yao na wala mabuti ya kuvaa wakati wakiwa
kazini hali inayowafanya wafanye kazi katika mazingira magumu.
Changamoto hizo zimebainika hivi karibuni
pale Madiwani wa Halmashauri ya Mpanda Mkoani Katavi walipofanya ziara
ya mafunzo katika Mwalo huo wa samaki kwa lengo la kujifunza namna ya uendeshaji
wa Mwalo.
Ziara hiyo iliwatembeza
maeneo mbalimbali ya soko na kupata ufafanuzi wa kina namna ya uendeshaji wa
Mwalo kutoka kwa Viongozi wa Soko hilo,Halmashauri na kutembezwa maeneo
mbalimbali hadi kufika katika
maeneo ya kupokelea na samaki na
kujionea jinsi hali ya usafi wa soko ulivyo ambapo walikutana na changamoto
hiyo ya uchafuzi wa mazingira kama uwepo
wa taka ngumu na nyepesi.
Soko hilo la Mwaloni hali ya usafi hairidhishi kutokana na kurudikana kwa taka ngumu, taka nyepesi na
miundo mbinu duni ya vitendea kazi kwa watenda kazi wanaoshughulika na shughuli
za kila siku katika soko hilo ambalo limesheheni kila aina ya bidhaa hasa mazao
ya majini kama samaki pamoja na mazao mengine ya kilimo kama matunda na
mbogamboga.
Akizungumza
na Madiwani waliotoka Halmashauri ya Mpanda kwenda kujifunza masuala ya mwalo
Jijini Mwanza Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Manispa ya Ilemela Fabiani Maha
ameleza kuwa ipo changamoto kubwa ya uzalishaji wa taka ngumu katika soko hilo
kama inavyoonekana ingawa
zinashughulikiwa kadiri inavyowezekana ingawa bado miundo mbinu bado ni
changamoto.
Mbali ya
changamoto ya miundo mbinu pia ameleza kuwa ameeleza kuwa soko linapokea na
kuuza biashara za maliasili,kilimo na kuchukua takwimu za uvuvi ,pia kutoa
vibali vya uvui na ubora wa mazao ya uvuvi na ushuru wake.
Awali Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhandisi Lukaza Justini alieleza kuwa ziwa ni uchumi na maisha na soko
hilo lilijengwa mwaka 2006 kwa gharama ya shilingi bilioni sita na shirika la
misaada la kijapani JAICA.
Mhandisi
Lukaza akaeleza kuwa soko linalohudumia wakazi wa Mwanza, Mikoa ya jirani na
wale wa ndani na nje ya nchi ambazo ni
Kenya, Uganda,Kongo DRC,Rwanda na Burundi pamoja na Sudani Kusini kwa sasa
dagaa wa mwanza na samaki wameonekana kupata soko katika nchi za Asia.
SKYLIGHT BAND YATOA RATIBA YAKE YA WIKI TUKIANZA NA MKESHA WA X-MASS USIKU WA LEO NDANI YA ESCAPE ONE
24.12.14 Mkesha wa XMASS tutakua ESCAPE1, show itaanzaa saa mbili usiku, kiingilio buku 7000/= tu: tukutane ESCAPE1 tuikaribishe XMASS
Vile vile tunapenda kutoa taarifa na kuwaomba radhi wadau wetu kutokana na safari yetu ya kanda ya ziwa XMASS hii, show zetu za ijumaa tarehe 26.12.14 thai village na jumapili 28.12.14 ESCAPE1 hazitofanyika.
Ila tukutane tena kwenye mkesha wa mwaka mpya 31.12.14 ndani ya ESCAPE1. .. Burudika na bendi yako katika msimu huu wa siku kuu...Skylight Band...just follow the light ♫
OLOLOSOKWAN WAJIWEKA TAYARI KUTIMIZA NDOTO YA KIJIJI CHA DIJITALI
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliposimama kwenye Kijiji cha Ngeresero kwa ajili ya kuwaungisha wanawake wa kimasai wanaofanya biashara ya kuuza bidhaa mbalimbali za shanga kwa watalii wanaosimama kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kupata mahitaji mbalimbali, wakati akielekea kijiji cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika lake la UNESCO.
Na Mwandishi wetu, Arusha
NDOTO ya kuwa na kijiji cha dijitali nchini Tanzania itaanza kutimia Januari mwakani wakati vifaa vinavyotakiwa kukamilisha mradi huo vitakapowasili kutoka kampuni ya Samsung Electronics.
Kwa mujibu wa watekelezaji wa mradi huo mkubwa unaotarajiwa kutumia dola za Marekani milioni 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) vifaa hivyo vinatarajiwa kuingia Bandari ya Dar es Salaam Januari tano mwakani.
Mkataba wa kuanzishwa kwa kijiji cha dijitali eneo la Ololosokwan tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro ulitiwa saini kati ya Unesco na Samsung electronics Novemba 6 mwaka huu.
Akizungumza na halmashauri ya kijiji cha Ololosokwan , Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues amewataka wanakijiji kujiandaa kwa mabadiliko makubwa ya kijiji chao kinapoingia katika dunia ya dijitali.
Alisema mambo ambayo wanastahili kuyaweka sawa ili kufanikisha ndoto zao kuhakikisha eneo ambalo mitambo na miundombinu ya mradi ipo ni lazima lisajiliwe kisheria ili kusiwepo na tatizo katika siku za usoni.
Aidha kutokana na ukubwa wa mashine zinazohusika, hasa makontena ni vyema wanakijiji wakaangalia maeneo korofi katika barabara za kuelekea huko na kuzirekebisha, ili magari hayo makubwa yenye vifaa yapite kwa usalama.
Alisema mradi huo wa miaka mitatu unatarajia kuwawezesha wananchi wa eneo hilo kuwa na ujasirimali, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika mawasiliano na utafutaji wa masoko, elimu na afya.
Kwa mujibu wa Bi. Rodrigues kijiji hicho pia kitakuwa na shule iliyoungwa na mtandao wa kompyuta duniani (intaneti), kliniki ya kisasa, tiba kwa kutumia teknolojia ya kompyuta na jenereta kubwa linalotumia nishati ya jua.
Bw. Abdulaziz Ali wa kitengo cha Transportation and Logistic kutoka UNESCO akitafsiri bei za bidhaa hizo za kimasai kwa wakimama hao wanaofanya biashara za urembo wa shanga kwa watalii na wazawa wanaopita katika kituo kijiji hicho ambapo wengine wao husimama kupata huduma ya chakula na vinywaji.
Aidha kuwapo na mtandao wa kompyuta kutawezesha UNESCO kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuanzisha mtaala utakaowawezesha vijana wa kimasai ambao ni wafugaji kupata elimu wanayoihitaji.
Mwakilishi huyo wa UNESCO amesema kwamba amefurahishwa na namna watu walivyoitikia mradi huo ambao umelenga kubadili maisha ya wafugaji hao kwa kuwawezesha pia kuitumia vilivyo sekta ya utalii.
“Kupitia mradi huu wananchi wanaweza kujifunza kusoma, kupata maarifa na katika harakati hizo kujua lugha ya kiingereza ili kuwasaidia kuwa na mawasiliano na watalii na watu wengine”, alisema Rodrigues.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwasili kwenye kata ya Ololosokwan kijiji cha Ololosokwan na kupokelewa na diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ndoinyo.
Alisema ni nia ya Unesco kuhakikisha kwamba inasaidia kufuta ujinga miongoni mwa wafugaji hao bila kuathiri utamaduni wao wanapoingia katika maisha ya kisasa.
Kijiji cha digitali cha Ololosokwan kitakuwa cha nne barani Afrika na yapo makubaliano ya msingi kwamba kijiji kingine kitajengwa Zanzibar mwakani.
Diwani wa kata ya Ololosokwan, Bw. Yannick Ndoinyo akiongozana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefika kijijini hapo kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNESCO pamoja na kukagua eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kijiji cha digitali cha Samsung.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisalimiana na baadhi ya kinamama wa mradi wa utalii unaofadhiliwa na shirika la UNESCO kata ya Ololosokwan kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza na wakina mama wa kimasai waliojumuika na waume zao mara baada ya kuwasili kijijini hapo ambapo aliwaasa kushiriki elimu ya afya ya uzazi wa mpango ili waweze kuzaa watoto wachache watakaoweza kuwahudumia na aliwaahidi kuwaanzisha program ya kusoma na kuandika kwa ajili ya kuboresha mawasiliano yao na watalii wanaotembelea kijiji chao na kununua biashara zao.
Pichani juu na chini ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwaonyesha jambo wakina mama wa kimasai jinsi gani teknolojia inayvowaleta watu kwa ukaribu zaidi kupitia "Tablet" ambapo katika kijiji hicho cha digitali cha Samsung wakazi wa eneo hilo watakua wakipewa mafunzo kutumia kifaa hicho cha "Tablet".
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua jambo nje ya maktaba inayofadhiliwa na UNESCO na kuwanufaisha wanafunzi wa shule ya sekondari Ololosokwani na vijana wa kata hiyo kupanua uelewa zaidi kwa kusoma vitabu mbalimbali wakati akikagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika lake. Kushoto ni Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ndoinyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa juu wa halmashauri ya kijiji wakati wa ziara yake kijijini hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na uongozi wa halmashauri ya kijiji cha Ololosokwan mara baada ya mazungumzo.
Bi. Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Ololosokwan kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na wakina mama wa kimasai wa kata ya Ololosokwan kijiji cha Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha mara baada ya kikao na halmashauri ya kijiji hicho.
Bi. Zulmira Rodrigues akiagana na baadhi ya wakinamama wa kimasai mara baada ya kikao cha halmashauri ya kijiji hicho.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) akifafanua jambo wakati wa kukagua eneo ambalo mitambo na miundombinu ya mradi itawekwa kwenye sehemu iliyotengwa na halmashauri ya kijiji kwa ajili ya kijiji cha dijitali cha Samsung. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya RAMAT, Pokare Koitumet, Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ndoinyo pamoja na Chifu wa kijiji cha Ololosokwan kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha.
Muonekano wa eneo hilo huku Bi. Zulmira Rodrigues akiendelea kulikagua.
Tuesday, December 23, 2014
TTCL YAANZISHA HUDUMA YA AFYA MTANDAO,YATOA MSAADA WA VYAKULA KWA TAASISI YA KANSA YA OCEAN ROAD
Laibu
Leonard Meneja Huduma wa kampuni ya simu ya TTCL akikabidhi vyakula
mbalimbali kwa Mary Haule Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ocean Road ya
jijini Dar es salaam ambavyo vimetolewa na kampuni hiyo kwa waginjwa wa
hospitali hiyo, kulia ni Devotha Kovaga Afisa habari wa hospitali ya
Ocean Road. Benjamin
Bizele mmoja wa maofisa kutoka kampuni ya simu ya TTCL akishusha
vyakula hivyo huku muugumzi mkuu wa hospitali hiyo Mary Haule
akivipokea. Muuguzi
Mkuu wa hospitali ya Ocean Road Mary Haule akitoa shukurani zake kwa
kampuni ya simu ya TTCL kwa msaada ilioutoa kwa wagonjwa wa hospitali
hiyo.
………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Dar
es Salaam. Wagonjwa wa saratani wa mikoani sasa watapata matibabu ya
ugonjwa huo kwa njia ya mtandao baada ya kampuni ya simu Tanzania (TTCL
kuzindua huduma ijulikanayo kwa jina la Afya Mtandao ambayo itamwezesha
mgonjwa kupata huduma akiwa katika moja ya hospitali ya rufaa.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi misaada ya vyakula kwa Taasisi ya Kansa ya Ocean
Road jana, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja cha TTCL, Laibu Leonard
alisema kuwa kupitia kwa Afya-Mtandao ambayo inatumia mkongo wa taifa
wa mawasiliano, madaktari wa Taasisi ya Ocean Road wataweza kuendesha
huduma mbalimbali za matibabu pamoja na upasuaji huku wakiwa katika
chumba maalum ambacho kitawawezesha kuona na kutoa mtazamo wa wa zoezi
la upasuaji linaloendelea mikoani.
Laibu
alisema kuwa hata huduma ya mionzi itafanyika kwa kushirikisha
madaktari bingwa waliounganishwa na huduma hiyo ambayo ni ya kisasa
zaidi. Alifafanua kuwa mbali ya mikoani, tiba hiyo inaweza kufanywa hata
kwa kushirikisha hospitali kubwa za nchi mbalimbali na hivyo kupunguza
gharama kubwa za matibabu.
“Hakuna
haja ya kwenda India, Uingereza, Ujerumani na nchi nyingine kwa ajili
ya upasuaji au huduma nyingine za tiba, unaweza kufanyiwa upasuaji
Bugando, madaktari wa Ocean Road, KCMC, Tumbi, Temeke, Mwanyamala na
nchi ya Tanzania wataona na kushiriki ipasavyo katika tiba hiyo, hii
inatokana na kuunganishwa kwa mtandao ambao utaonyesha picha za video,
za kawaida na huduma ya sauti,” alisema Leonard.
Alisema
kuwa lengo la TTCL ni kuunganisha hospitali zote za rufaa nchini
ifikapo mwezi Machi mwakani ili kuraisisha huduma hiyo. Kuhusiana na
msaada wa vyakula wenye thamani ya Sh Milioni 3, Leonard alisema kuwa
wameamua kutoa msaada huo ili kupunguza gharama za vyakula kwa wagonjwa
ambao wamelazwa katika taasisi hiyo.
WANACHAMA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA WILAYANI URAMBO WAFURAHIA HUDUMA BORA ZA MATIBABU
BENKI YA POSTA YAENDESHA SEMINA KWA WAJASILIAMALI MKOANI MBEYA
BENKI ya Posta Tanzania (TPB) Tawi
la Mbeya, imetoa semina kwa Wajasiriamali wa mkoa ikiwa na lengo la
kuwaongezea ujuzi kwenye biashara zao. Semina hiyo ya siku moja
imefanyika kwenye ukumbi wa Mtenda Sunset mjini Mbeya na kufunguliwa na
Mkuu wa Wilaya, Profesa Norman Sigallah.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa
semina hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
Posta, Sabasaba Moshingi, Mkuu wa Wilaya alitoa wito kwa wajisiriamali
kutoogopa kukopa kwenye mabenki ili kukuza mitaji yao na hatimae
biashara zao.
Prof. Sigallah alitoa changamoto
kwa wajasiriamali kuhakikisha biashara zao zinaubora unaotakiwa ili
kuweza kujenga imani na ushindani kwenye soko. Mkuu huyo wa Wilaya
alitoa changamoto kwa benki ya Posta kuweka dawati maalum la wataalam
watakaotoa ushauri kwa wajasiriamali pindi wanapokuja kuomba mikopo.
Aliwashauri wajasiriamali kujiepusha na makundi yenye muelekeo wa kuleta
vurugu na kuvunja amani, kwani ili kukua biashara yoyote inahitaji
amani na utulivi.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi, akijibu maswali mbalimbali
yaliyoulizwa na wajasiriamali hao zaidi ya 150 waliohudhuria semina
hiyo, alisema benki yake itaendelea kuboresha huduma zake hasa upande wa
mikopo, na pia kuangalia suala la riba zinazotozwa kwa aina tofauti ya
biashara.
“Benki yangu itaendelea kuangalia
ni namna gani tunaweza kuweka wataalam watakaotoa ushauri mzuri kwa
wajasiriamali ili kupunguza mlolongo mrefu wa nenda rudi kwa mkopaji.
Hii ni katika jitihada za kuhakikisha kuwa mkopaji anapata mkopo kwa
wakati ili kuwahi fursa iliyojitokeza,”.
Akiongea kwa niaba ya
wajasiriamali hao, Bi. Joyce Mkongo, aliishukuru sana benki ya Posta kwa
kutoa mafunzo hayo kwao,ambayo yamewafungua macho na kuwaondolewa woga
wa kutumia huduma za kibenki. Alisema wajasiriamali wengi wanasita
kuchukua mikopo kwa hofu kuwa mali zao zitataifishwa pindi
watakaposhindwa kulipa mkopo.