Laibu
Leonard Meneja Huduma wa kampuni ya simu ya TTCL akikabidhi vyakula
mbalimbali kwa Mary Haule Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ocean Road ya
jijini Dar es salaam ambavyo vimetolewa na kampuni hiyo kwa waginjwa wa
hospitali hiyo, kulia ni Devotha Kovaga Afisa habari wa hospitali ya
Ocean Road. Benjamin
Bizele mmoja wa maofisa kutoka kampuni ya simu ya TTCL akishusha
vyakula hivyo huku muugumzi mkuu wa hospitali hiyo Mary Haule
akivipokea. Muuguzi
Mkuu wa hospitali ya Ocean Road Mary Haule akitoa shukurani zake kwa
kampuni ya simu ya TTCL kwa msaada ilioutoa kwa wagonjwa wa hospitali
hiyo.
………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Dar
es Salaam. Wagonjwa wa saratani wa mikoani sasa watapata matibabu ya
ugonjwa huo kwa njia ya mtandao baada ya kampuni ya simu Tanzania (TTCL
kuzindua huduma ijulikanayo kwa jina la Afya Mtandao ambayo itamwezesha
mgonjwa kupata huduma akiwa katika moja ya hospitali ya rufaa.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi misaada ya vyakula kwa Taasisi ya Kansa ya Ocean
Road jana, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja cha TTCL, Laibu Leonard
alisema kuwa kupitia kwa Afya-Mtandao ambayo inatumia mkongo wa taifa
wa mawasiliano, madaktari wa Taasisi ya Ocean Road wataweza kuendesha
huduma mbalimbali za matibabu pamoja na upasuaji huku wakiwa katika
chumba maalum ambacho kitawawezesha kuona na kutoa mtazamo wa wa zoezi
la upasuaji linaloendelea mikoani.
Laibu
alisema kuwa hata huduma ya mionzi itafanyika kwa kushirikisha
madaktari bingwa waliounganishwa na huduma hiyo ambayo ni ya kisasa
zaidi. Alifafanua kuwa mbali ya mikoani, tiba hiyo inaweza kufanywa hata
kwa kushirikisha hospitali kubwa za nchi mbalimbali na hivyo kupunguza
gharama kubwa za matibabu.
“Hakuna
haja ya kwenda India, Uingereza, Ujerumani na nchi nyingine kwa ajili
ya upasuaji au huduma nyingine za tiba, unaweza kufanyiwa upasuaji
Bugando, madaktari wa Ocean Road, KCMC, Tumbi, Temeke, Mwanyamala na
nchi ya Tanzania wataona na kushiriki ipasavyo katika tiba hiyo, hii
inatokana na kuunganishwa kwa mtandao ambao utaonyesha picha za video,
za kawaida na huduma ya sauti,” alisema Leonard.
Alisema
kuwa lengo la TTCL ni kuunganisha hospitali zote za rufaa nchini
ifikapo mwezi Machi mwakani ili kuraisisha huduma hiyo. Kuhusiana na
msaada wa vyakula wenye thamani ya Sh Milioni 3, Leonard alisema kuwa
wameamua kutoa msaada huo ili kupunguza gharama za vyakula kwa wagonjwa
ambao wamelazwa katika taasisi hiyo.
No comments:
Post a Comment