Na Kibada Kibada -Mwanza
MWALO.
Wafanyabiashara ya samaki na bidhaa nyingine
za maliasili katika soko la samaki la Mwalo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemeala
Jijini Mwanza wako hatarini kupatwa na Magonjwa ya mlipuko hasa wakati huku mvua
zinazoendelea kunyesha kutokana na changamoto ya uchafuzi wa mazingira uliopo
katika soko hilo.
Mbali ya uchafuzi huo pia zipo changamoto nyingine
za uhaba wa vitendea kazi na miundo
mbinu mibovu ya kutolea maji kwenye meza za kupokelea samaki pamoja na
mrundikano wa taka ngumu na taka nyepesi katika maeneo mbalimbali ya Soko
hilo la Mwalo wa Samaki.
Upungufu wa vitendea kazi kwa wafanyakazi wanashughulikia
usafi katika soko hilo hasa samaki ambapo wafanyakazi wanaparua samaki bila
kuwa kinga yeyote kwenye mikono yao na wala mabuti ya kuvaa wakati wakiwa
kazini hali inayowafanya wafanye kazi katika mazingira magumu.
Changamoto hizo zimebainika hivi karibuni
pale Madiwani wa Halmashauri ya Mpanda Mkoani Katavi walipofanya ziara
ya mafunzo katika Mwalo huo wa samaki kwa lengo la kujifunza namna ya uendeshaji
wa Mwalo.
Ziara hiyo iliwatembeza
maeneo mbalimbali ya soko na kupata ufafanuzi wa kina namna ya uendeshaji wa
Mwalo kutoka kwa Viongozi wa Soko hilo,Halmashauri na kutembezwa maeneo
mbalimbali hadi kufika katika
maeneo ya kupokelea na samaki na
kujionea jinsi hali ya usafi wa soko ulivyo ambapo walikutana na changamoto
hiyo ya uchafuzi wa mazingira kama uwepo
wa taka ngumu na nyepesi.
Soko hilo la Mwaloni hali ya usafi hairidhishi kutokana na kurudikana kwa taka ngumu, taka nyepesi na
miundo mbinu duni ya vitendea kazi kwa watenda kazi wanaoshughulika na shughuli
za kila siku katika soko hilo ambalo limesheheni kila aina ya bidhaa hasa mazao
ya majini kama samaki pamoja na mazao mengine ya kilimo kama matunda na
mbogamboga.
Akizungumza
na Madiwani waliotoka Halmashauri ya Mpanda kwenda kujifunza masuala ya mwalo
Jijini Mwanza Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Manispa ya Ilemela Fabiani Maha
ameleza kuwa ipo changamoto kubwa ya uzalishaji wa taka ngumu katika soko hilo
kama inavyoonekana ingawa
zinashughulikiwa kadiri inavyowezekana ingawa bado miundo mbinu bado ni
changamoto.
Mbali ya
changamoto ya miundo mbinu pia ameleza kuwa ameeleza kuwa soko linapokea na
kuuza biashara za maliasili,kilimo na kuchukua takwimu za uvuvi ,pia kutoa
vibali vya uvui na ubora wa mazao ya uvuvi na ushuru wake.
Awali Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhandisi Lukaza Justini alieleza kuwa ziwa ni uchumi na maisha na soko
hilo lilijengwa mwaka 2006 kwa gharama ya shilingi bilioni sita na shirika la
misaada la kijapani JAICA.
Mhandisi
Lukaza akaeleza kuwa soko linalohudumia wakazi wa Mwanza, Mikoa ya jirani na
wale wa ndani na nje ya nchi ambazo ni
Kenya, Uganda,Kongo DRC,Rwanda na Burundi pamoja na Sudani Kusini kwa sasa
dagaa wa mwanza na samaki wameonekana kupata soko katika nchi za Asia.
No comments:
Post a Comment