Pages

KAPIPI TV

Friday, November 28, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE NEWALA

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Neawala Mh George Mkuchika mara baada ya kuwasili mjini Newala akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Mtwara ziara yenye lengo la kukagua na kuhimiza Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wananchi, Katibu Mkuu Kinana emeembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa miondombinu ya maji , Zahanati Ofisi za Chama cha Mapinduzi na kuzungumza na wananchi katika mikutano mbalimbali, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE -NEWALA-MTWARA) 2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana viongozi wa kiwanda cha kubangua korosho mjini Newala kulia Niry Patel Mratibu wa Usafirishaji na katikati ni Ednyadayu Meneja wa ufundi. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubangua korosho na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
10
Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiendelea na kazi ya kubangua korosho
6
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mhandisi wa Maji Newala Bw. Nsajigwa Said wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Malatu mjini Neawala.
7
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa maji katika kata ya Malatu kushoto ni mkuu wa mkoa wa Mtwara B. Halima Dendegu.
8
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusuka nondo katika ujenzi wa tanki la maji la kijiji cha Kilidu kwa pamoja na wafanyakazi wa katika mradi huo wa tatu kutoka kulia aliyesimama ni Mbunge wa jimbo la Neawala Mh. George Mkuchika.
9
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Dr Yudas Ndugile Mganga mkuu wa wilaya ya Newala wakati alipokagua jengo jipya la Kituo cha Afya Mkwedu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa wilaya ya Newala BwMarx Simon Kamaoni na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendegu.
11
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishuhudia aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Newala Chadema Bw. Adam Nangwanda Sijaona akivua shati la CHADEMA na kuvaa la CCM mara baada ya kuondoka katika chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama mjini Newala.
12
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitupa shati hilo
13
Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Newala Chadema Bw. Adam Nangwanda akiwa amekabidhi kadi yake na ya mke wake kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kujiunga na CCM mjini Newala kulia ni Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
14
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama mjini Newala
15
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakisisitiza jambo katika mkutano huo.
16
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakikabidhi pikipiki kwa vijana ambazo zimekopeshwa kwao ili kujikomboa kiuchumi.
17
Umati wa watu wakisikiliza mkutano huo.

MWILI WA MPENDWA WETU SEBASTIAN MGIMBA WAPUMZISHWA KWA AMANI KATIKA MAKABURI YA KINONDONI

 Ndugu wa Marehemu Sebastian Mgimba Philipo Mgimba (katikati) akiwa amebeba msalaba huku pembeni ndugu mwingine akiwa pamoja na picha ya marehemu wakati wa misa fupi ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
Dada wa Marehemu Sebastian Mgimba, Mariam akiwa na ndugu zake wakati wa sala ya mazishi iliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni
 Rafiki wa Marehemu akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba mara baada ya sala fupi ya mazishi kufanyika
 Baba Mzazi wa Marehemu Sebastian Mgimba, Mzee Mgimba pamoja na Mama wakiwa na shada la maua tayari kwa kuweka juu ya kaburi la Mtoto wao Marehemu Sebastian Mgimba
 Ndugu wa Marehemu Sebastian Mgimba wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba
 Dada wa Marehemu Sebastian Mgimba, Bi Mariam Lukaza akiwa na mumewe Johnson Lukaza wakijiandaa kuweka shada la Maua juu ya Kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba katika mazishi yaliyofanyika  katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.
Mama Leoncia Lukaza akijiandaa kuweka Shada la Maua kwa niaba ya familia ya Lukaza katika kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba kwenye mazishi ya marehemu Sebastiani Mgimba yaliyofanyika  katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
Umati wa Watu waliojitokeza kwaajili ya Kumpumzisha Ndugu yetu Sebastian Mgimba katika makaburi ya Kinondoni.Picha na Josephat Lukaza - http://www.josephatlukaza.com
Marehemu Sebastian Mgimba alifariki dunia tarehe 20 Nov 2014 nchini Malaysia, Marehemu ameacha Mke na mtoto mmoja. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amin

Wednesday, November 26, 2014

"TANESCO TUNATAKA FIDIA ZETU" WANANCHI KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

WANANCHI wa kata ya Matendo iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Kigoma Mkoa wa Kigoma  wameandamana kutoka katika kata hiyo hadi zilizpo ofisi za shirika la umeme Tanesco Tawi la kigoma iliyopo katika Manispaa ya kigoma Ujiji kwa  madai ya  malipo ya fidia  za  kufyekewa  mazao katika mashamba  yaliyopitishwa  nguzo za umeme  vijijini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wahanga  Kasim Mpozemenya na Samweli Madebo walisema  mwaka 2012 walifanyiwa tathimini ya mashamba na mazao  ambayo yalifyekwa  na kuahidiwa kulipwa baada ya miezi sita ilihali hawajui kiasi cha malipo stahiki.
Kitendo cha kuzungushwa  stahiki za malipo kwa miaka mitatu  imechangia wahanga wandamane  katika ofisi za shirika hilo kwa lengo la kutaka  walipwe na wafanye mambo mengine sanjari na kuhama maeneo hayo,ambapo kisheria hawana fursa ya kuendeleza kilimo na makazi kwa ujumla.

Akithibitisha tukio hilo Katibu Tawala wa wilaya ya kigoma Elisha Joshua alisema uwajibikaji  na utekelezaji kwa wakati ni chachu ya kuondoa  adha za  jamii kufikia hatua ya mandamano na mandamano ni sehemu ya kudai haki stahiki kwa uongozi husika.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya kigoma Hamisi Betese alisema kamati ya ulinzi  na usalama  wilaya  imefanya mazungumzo na uongozi wa shirika Taifa na  leo(jana) saa.7 mchana  wahanga wote waliopitiwa na mradi wa umeme vijijini watalipwa.

Alisema halmashauri itaingiziwa kiasi cha  fedha  zaidi ya milioni  89 katika akaunti husika  katibu tawala atawajibika kujiridhisha na mchakato wa fedha  na idadi ya walengwa   ili kuondoa hujuma na kutoaminiana baina ya wananchi na uongozi wa halmashauri na kuwashauri waende majumbani kuendelea na ujenzi wa taifa.

Jitihada za kumpata meneja wa shirika hilo hazikuzaa matunda.

SERIKALI INAVYOENDELEA KUBORESHA MIUNDO MBINU TABORA MJINI

Baadhi ya miundo mbinu ambayo inaendelea kuboreshwa  na Serikali Tabora mjini hili ni eneo la Kata ya Malolo

POLISI TABORA WAKAMATA SMG,JAMBAZI LAWATOROKA SIKONGE

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akiwaonesha waandishi wa habari silaha zilizokamatwa katika operesheni maalumu ambapo SMG moja ilikamatwa huku jambazi aliokuwa ameihifadhi silaha hiyo kwenye begi akiwatoroka baada ya Polisi kumhisi kuwa amebeba kitu kisicho cha kawaida huko eneo la Mission wilayani  Sikonge.

KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI NANYUMBU

2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiponda mawe wakati aliposhiriki katika ujenzi wa Bwawa la maji linalojengwa katika kijiji cha Sengenya Mangaka wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara akiwa katika ziara yake ya kikazi akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali pamoja na wananchi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi CCM, Katika ziara hiyo leo Kinana amefanya kazi mbalimbali pamoja na kufanya mikutano kadhaa akiwa ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NANYUMBU-MTWARA) 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na mafundi kupanga mawe katika ukingo wa bwawa hilo linalojengwa katika kijiji cha Sengenya Mangaka wilayani Nanyumbu. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo wakati alipokuwa akikagua kituo cha afya cha Mangaka wilayani Nanyumbu ambapo ameelezwa kwamba kituo hicho kimeomba kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya ambapo kimekidhi vigezo vyote lakini wamesubiri kwa miaka mitatu bila mafanikio. 5Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo akizungumza na waandishi wa habari adha wanayoipata wagonjwa kutokana na kutopandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya pamoja na kukidhi vigezo vyote vya kuwa hospitali ya wilaya. 6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo katika chumba cha upasuaji kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo.7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo mara baada ya kutembelea kituo hicho katikati ni Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo S. Kiswaga. 8Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi, Mh. Festus Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakipita kwenye daraja la Umoja 10Ni Daraja lenye urefu wa zaidi ya mita 700. 11Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani, Mh. Festus Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakipita kwenye daraja la Umoja 12Mkurugenzi wa mtandao huu wa Fullshangwe akivinjari katika daraja hilo. 13Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata picha ya kumbukumbu na wanahabari walioko katika msafara wake. 14 15Shehena ya mbao ziliokamatwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita zikiwa zimehifadhiwa katika ofisi za Mamlaka ya mapato TRA Mtambaswala katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji. 16Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari kuelezea uzembe na ukiritimba wa baadhi ya watumishi wa serikali kutokana na suala hilo kuchukua muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi. 17Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nanyumbu 18Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nanyumbu
9
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi , Mh. Festus Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakipita kwenye daraja la Umoja.19
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo
20
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nanyumbu.

UPDATES YA MSIBA WA NDG SEBASTINA MGIMBA

 Ndugu pamoja na jamaa wa marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki dunia nchini Malaysia wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam eneo la Mizigo ukitokea nchini Malaysia.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki nchini Malaysia likiingizwa katika gari maalumu la kubebea jeneza katika uwanja wa Ndege wa Dar Es Salaam katika eneo la kutolea na kusafirishia mizigo mara baada ya mwili huo kuwasilini Nchini Leo ukitokea Nchini Malaysia.
Mchungaji akiendelea na ibada fupi iliyofanyika katika eneo la Kutolea mizigo katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam mara baada ya Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba kuwasili nchini leo.Picha zote na Josephat Lukaza - Wa http://www.josephatlukaza.com

Msiba wa Marehemu Sebastian Mgimba upo Sinza Kumekucha ambapo baada ya mwili kupokelewa leo uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam umepelekwa Kwake Sinza na Hatimaye Kesho Kutakuwa na Misa ya kumuombea marehemu na hatimaye Mwili wa Marehemu kupumzishwa Katika Nyumba yake ya Milele Katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam. 

Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amina
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe

Tuesday, November 25, 2014

MKOSAMALI APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUFANYA VURUGU KITUO CHA KUANDIKISHA WAPIGA KURA-KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

MBUNGE wa Jimbo la Muhambwe Wilaya ya Kibondo  Mkoa wa Kigoma,Felix Mkosamali amepandishwa kizimbani ( leo) katika Mahakama ya wilaya ya kibondo kujibu tuhuma dhidi ya kufanya vurugu katika kituo cha kuandikisha wapigakura .

Akisomewa jalada la kesi hiyo yenye namba 320/2014   mbele ya hakimu wa wilaya Erick Maley  mwendesha mashitaka wa mahakama ya wilaya ya kibondo Peter Makala alisema mbunge huyo alidaiwa kufanya fujo   katika kituo cha uandikishaji wa kupiga kura kilichopo kitongoji cha Nduta kijiji cha kumuhasha  kata ya Murungu  wilayani humo.

Alisema  Novemba,24,saa 9 alasiri mbunge huyo alitinga maeneo ya tukio na kudaiwa kumzuia karani  aliyekuwa akiandikisha wananchi waliofika hapo kwa kumnyang`anya vifaa husika kwa madai  waliofika kujiandikisha hapo ni wanachama wa chama tawala(CCM) huku vyama vya upinzani vikiachwa solemba.

Kitendo cha kumuinua karani na kuchukua  vitabu vyote na kuingia katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kibondo  Mboya Judesadius na kumtupia makablasha husika,ikiwa ni sehemu ya kuonesha kutoridhishwa na utaratibu wa uandikishaji  katika kituo hicho.

Hakimu wa wilaya ya Kibondo Erick Malay alipomuliza mtuhumiwa juu ya shtaka lake ,mbunge huyo machachari awapo Bungeni alikana shtaka husika na kesi imeahirishwa na itasomwa tena Desemba,29,mwaka huu.

Awali Kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Jafari Mohamed akiri mbunge huyo alifanya fujo  Novemba ,24,2014,saa 9,alasiri katika kitongoji cha nduta alikiuka sheria za malalamiko na kufanya fujo kituoni hapo, ilihali akijua ni kosa kisheria ambapo kwa raia yeyote bila kujali nyadhifa aliyonayo atachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa katiba husika.

SUZUKI ESCUDO INAUZWA BEI NZURI...IPO KWENYE HALI NZURI KABISA

Upande wa Kushoto unavyoonekana
Upande wa Kulia Unavyoonekana
TAARIFA KUHUSU GARI HII NI..........
REGISTRATION NUMBER: T 746 AAT
MAKE: SUZUKI
MODEL: ESCUDO
MODEL NUMBER: TDIIW
BODY TYPE: STATION WAGON
COLOR: BLUE METALLIC


Year Of Manufacture:1995
ENGINE CAPACITY: 1998 cc
FUEL USED: PETROL
HALAFU NI 4WD 

TRANSIMISSION: AUTOMATIC.

GARI HII IPO KWENYE HALI NZURI KABISA
BEI NI MIL 6.5 Tsh.
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA NAMBA HII 0712 390 200

TANGAZO LA MSIBA KUTOKA FAMILIA YA NDG SEBASTIAN MGIMBA WA DAR ES SALAAM

Marehemu Mathew Sebastian Mgimba Enzi za Uhai Wake.
2Timotheo 4:7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza Imani nimeilinda

Familia ya Ndugu Sebastian Mgimba inasikitika kutangaza kifo cha Mpendwa wao Mathew Sebastian Mgimba kilichotokea Nchini Malaysia tarehe 20/11/2014.

Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili leo tarehe 25/11/2014 na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwao Sinza Kumekucha.
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi - Amina

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI BUSINDE WATUMIA CHOO KIMOJA NA WALIMU WAO -KIGOMA

BUSINDE KIGOMA
Na Magreth Magosso,Kigoma

ZAIDI ya wanafunzi 400 wanaosoma shule ya msingi ya Businde iliyopo manispaa ya kigoma ujiji Mkoa wa kigoma wamelazimika kutumia choo cha walimu ,baada ya choo cha wanafunzi kutitia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha huku  uongozi wa shule wapiga marukuku  matumizi ya choo hicho.

Kufungwa kwa choo hicho imekuwa faraja kwa wanafunzi husika kuepuka na madhara mbalimbali hasa ya kiafya,ambapo kutitia kwa matundu nane imechangiwa na  uchakavu wa choo hicho kilichojengwa na ukoloni wa mjerumani tangu mwaka 1954.
 
Akifafanua hilo Diwani wa kata ya businde Mauridi Makala alisema lengo la kuzuia matumizi ya choo hicho ni faida ya kuepusha maafa kwa wanafunzi husika,ambapo kwa sasa wanatumia matundu mawili ambayo walimu wanayatumia.

“mvua zinazoendelea kunyesha imechangia kubomoka kwa choo,kaya mbili kubomoka na kaya tano kuezuliwa mabati sanjari na barabara ya businde ujiji kukatika na kupelekea adha kwa wananchi husika” alisema Diwani huyo.

Akithibitisha hilo mtendaji wa kata husika Richard Mgae alisema changamoto  ya kutitia kwa choo ilifikishwa kwa uongozi wa manispaa ya ujiji na wamedai kupitia bajeti ya  fedha ya mwaka  2014/15/ watahakikisha wanalifanyia kazi.

Naye mratibu wa elimu kata ya businde Noel  Joel alisema ni kweli wamewaruhusu wananfunzi watumie choo cha walimu kwa muda hadi hapo adha hiyo itakapofanyiwa kazi,kwa nia ya kuondokana na maafa yasiyo na lazima.

Baadhi ya wanafunzi kwa nyakati tofauti Amina Rashid na Josefu emanuel walisema walimu wamewaruhusu watumie choo chao,kwa kuwa choo cha wanafunzi kimetitia ambapo ni hatari kwa matumizi kwa kuhofiwa kutumbukia katika mashimo ya matundu hayo.

Mwandishi wetu alifika katika shule ya msingi ya businde na kushuhudia bango lenye ujumbe wa kuwataka wananfunzi wasikitumie choo hicho,sanjari na kumkuta mama mmoja Faida Luziga akiwa na watoto  tisa, mmoja wa mwezi mmoja amejibanza kwenye kibanda cha jiko baada ya nyumba kubomoka.

Monday, November 24, 2014

DAKTA SHEIN AKIWA KATIKA MKUTANO WA CCM MFENESINI

IMG_2308 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia) Mwenyekiti wa Wilaya ya Mfenesini Kichama Mjumbe Msuri wakiwa katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha  Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi Kichama nje ya Mji wa Unguja katika mkutano maalum wa kuimarisha Chama kwa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani,{Picha na Ikulu.]IMG_2372
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani  katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha  Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi Kichama akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Wilaya ya Mfenesini, {Picha na Ikulu.]