Na Magreth Magosso,Kigoma
WANANCHI wa kata ya Matendo iliyopo Halmashauri ya wilaya ya
Kigoma Mkoa wa Kigoma wameandamana
kutoka katika kata hiyo hadi zilizpo ofisi za shirika la umeme Tanesco Tawi la
kigoma iliyopo katika Manispaa ya kigoma Ujiji kwa madai ya
malipo ya fidia za kufyekewa
mazao katika mashamba yaliyopitishwa
nguzo za umeme vijijini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wahanga Kasim Mpozemenya na Samweli Madebo
walisema mwaka 2012 walifanyiwa
tathimini ya mashamba na mazao ambayo
yalifyekwa na kuahidiwa kulipwa baada ya
miezi sita ilihali hawajui kiasi cha malipo stahiki.
Kitendo cha kuzungushwa
stahiki za malipo kwa miaka mitatu imechangia wahanga wandamane katika ofisi za shirika hilo kwa lengo la
kutaka walipwe na wafanye mambo mengine
sanjari na kuhama maeneo hayo,ambapo kisheria hawana fursa ya kuendeleza kilimo
na makazi kwa ujumla.
Akithibitisha tukio hilo Katibu Tawala wa wilaya ya kigoma
Elisha Joshua alisema uwajibikaji na
utekelezaji kwa wakati ni chachu ya kuondoa
adha za jamii kufikia hatua ya
mandamano na mandamano ni sehemu ya kudai haki stahiki kwa uongozi husika.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya kigoma Hamisi
Betese alisema kamati ya ulinzi na
usalama wilaya imefanya mazungumzo na uongozi wa shirika
Taifa na leo(jana) saa.7 mchana wahanga wote waliopitiwa na mradi wa umeme
vijijini watalipwa.
Alisema halmashauri itaingiziwa kiasi cha fedha zaidi
ya milioni 89 katika akaunti husika katibu tawala atawajibika kujiridhisha na
mchakato wa fedha na idadi ya
walengwa ili kuondoa hujuma na
kutoaminiana baina ya wananchi na uongozi wa halmashauri na kuwashauri waende
majumbani kuendelea na ujenzi wa taifa.
No comments:
Post a Comment