BUSINDE KIGOMA |
Na Magreth Magosso,Kigoma
ZAIDI ya wanafunzi 400 wanaosoma shule ya msingi ya Businde iliyopo
manispaa ya kigoma ujiji Mkoa wa kigoma wamelazimika kutumia choo cha walimu
,baada ya choo cha wanafunzi kutitia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
huku uongozi wa shule wapiga
marukuku matumizi ya choo hicho.
Kufungwa kwa choo hicho imekuwa faraja kwa wanafunzi husika
kuepuka na madhara mbalimbali hasa ya kiafya,ambapo kutitia kwa matundu nane
imechangiwa na uchakavu wa choo hicho
kilichojengwa na ukoloni wa mjerumani tangu mwaka 1954.
Akifafanua hilo Diwani wa kata ya businde Mauridi Makala
alisema lengo la kuzuia matumizi ya choo hicho ni faida ya kuepusha maafa kwa
wanafunzi husika,ambapo kwa sasa wanatumia matundu mawili ambayo walimu
wanayatumia.
“mvua zinazoendelea kunyesha imechangia kubomoka kwa choo,kaya
mbili kubomoka na kaya tano kuezuliwa mabati sanjari na barabara ya businde
ujiji kukatika na kupelekea adha kwa wananchi husika” alisema Diwani huyo.
Akithibitisha hilo mtendaji wa kata husika Richard Mgae
alisema changamoto ya kutitia kwa choo ilifikishwa
kwa uongozi wa manispaa ya ujiji na wamedai kupitia bajeti ya fedha ya mwaka 2014/15/ watahakikisha wanalifanyia kazi.
Naye mratibu wa elimu kata ya businde Noel Joel alisema ni kweli
wamewaruhusu wananfunzi watumie choo cha walimu kwa muda hadi hapo adha hiyo
itakapofanyiwa kazi,kwa nia ya kuondokana na maafa yasiyo na lazima.
Baadhi
ya wanafunzi kwa nyakati tofauti Amina Rashid na Josefu emanuel
walisema walimu wamewaruhusu watumie choo chao,kwa kuwa choo cha
wanafunzi kimetitia ambapo ni hatari kwa matumizi kwa kuhofiwa
kutumbukia katika mashimo ya matundu hayo.
Mwandishi wetu alifika katika shule ya msingi ya businde na
kushuhudia bango lenye ujumbe wa kuwataka wananfunzi wasikitumie choo
hicho,sanjari na kumkuta mama mmoja Faida Luziga akiwa na watoto tisa, mmoja wa mwezi mmoja amejibanza kwenye
kibanda cha jiko baada ya nyumba kubomoka.
No comments:
Post a Comment