Na Magreth Magosso,Kigoma
MBUNGE wa Jimbo la Muhambwe Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma,Felix Mkosamali amepandishwa
kizimbani ( leo) katika Mahakama ya wilaya ya kibondo kujibu tuhuma dhidi ya
kufanya vurugu katika kituo cha kuandikisha wapigakura .
Akisomewa jalada la kesi hiyo yenye namba 320/2014 mbele
ya hakimu wa wilaya Erick Maley mwendesha mashitaka wa mahakama ya wilaya ya
kibondo Peter Makala alisema mbunge huyo alidaiwa kufanya fujo katika
kituo cha uandikishaji wa kupiga kura kilichopo kitongoji cha Nduta kijiji cha
kumuhasha kata ya Murungu wilayani humo.
Alisema Novemba,24,saa 9 alasiri mbunge huyo alitinga
maeneo ya tukio na kudaiwa kumzuia karani aliyekuwa akiandikisha wananchi waliofika
hapo kwa kumnyang`anya vifaa husika kwa madai
waliofika kujiandikisha hapo ni wanachama wa chama tawala(CCM) huku
vyama vya upinzani vikiachwa solemba.
Kitendo cha kumuinua karani na kuchukua vitabu vyote na kuingia
katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kibondo Mboya Judesadius na kumtupia makablasha
husika,ikiwa ni sehemu ya kuonesha kutoridhishwa na utaratibu wa uandikishaji katika kituo hicho.
Hakimu wa wilaya ya Kibondo Erick Malay alipomuliza
mtuhumiwa juu ya shtaka lake ,mbunge huyo machachari awapo Bungeni alikana
shtaka husika na kesi imeahirishwa na itasomwa tena Desemba,29,mwaka huu.
Awali Kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Jafari Mohamed akiri
mbunge huyo alifanya fujo Novemba
,24,2014,saa 9,alasiri katika kitongoji cha nduta alikiuka sheria za malalamiko
na kufanya fujo kituoni hapo, ilihali akijua ni kosa kisheria ambapo kwa raia
yeyote bila kujali nyadhifa aliyonayo atachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu
wa katiba husika.
No comments:
Post a Comment