Pages

KAPIPI TV

Saturday, September 27, 2014

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE KOROGWE KWA KISHINDO

Katibu  Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishona nguo kwenye kituo cha ushonaji cha Veronica Simba (kushoto) alipokagua kituo hicho enbeo la Mombo Sokoni, leo Septemba 27, 2014, akiwa katika ziara kukagua na kuhimiza utekeleza w ilani ya CCM, katika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Kulia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani.
  TUNASHONA HIVI: Katibu  Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimuelekeza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kushona nguo kwenye ofisi ya Veronica Simba (kushoto) iliyopo Mombo Sokoni.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakinunua matunda kwenye banda ya mfanyabiashara ya matunda hayo, mjini Mombo,  kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara, leo Septemba 26, 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (katikati) wakiwapungia mikono wananchi walipowasili kwenye uwanja wa mkutano mjini Mombo leo Septemba 26, 2014
 Diwani wa kata ya Mombo akishangiia baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kutamka wazi kuwa katika kuhakikisha wanapata halmashauri ya mji mdogo.
 
 Wananchi wakiwa wamekaa kwa shauku ya kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahan Kinana.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mombo ambapo aliwaambia wananchi hao wanachofanya wapinzani ni biashara, kwani kwao kuandamanisha watu ni mtaji mzuri wa kuwaingizia pesa kutoka nje.

 Umati wa watu ukimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Tanga Aisha Kigoda pamoja na Mjumbe wa NEC wilaya ya Korogwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Tanga Dk. Edmund Mdolwa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Mombo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mombo.
Wananchi wakifuatilia mkutano wa Kinana mjini Mbombo
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa kwenye kiti tayari kupokea zawadi kutoka kwa wamasai wanaoishi Mombo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi kutoka kwa wamasai wa Mombo.
 Katibu wa CCM, Abdulrahman akipeana mkono wa shukrani kwa kiongozi wa wamasai wa Mbombo Samng'o Maikaambaye [ia ni mwenyekiti wa Tawi la Chang'ombe ,Mombo.

WANAFUNZI WA KIKE WASHINDWA KUFANYA MTIHANI BAADA YA KUKUMBWA NA UGONJWA WA AJABU-KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

Wanafuzi 16 wa kike katika shule ya sekondari ya Mugombe  wilaya ya Kibondo Mkoani hapa,wameshindwa kufanya mtihani wa majaribio wa kidato cha Nne baada ya kupatwa na hali ya kuchanganyikiwa akili ghafla katika mazingira ya kutatanisha.

Wakizungumzia hilo kwa nyakati tofauti mbele ya waandishi wa habari shuleni hapo, Tilifania Jonathan na Suzana Charles walisema Septemba 23,2014  majira ya mchana baada ya kumaliza mtihani wa tano walihisi maumivu  makali ya kichwa pamoja na kukosa nguvu mwilini kwa ghafla na kujikuta wanaanza kukimbiakimbia hovyo.

Akielezea hilo Mkuu wa shule hiyo Tanu Selemani alikiri  kuwepo kwa tukio hilo  kwa wanafunzi wa kike tu,ambapo rasmi walianza wanafunzi wawili  mnamo  17,septemba mwaka huu na hali kuwa mbaya zaidi tarehe 26,septemba na kusabaisha baadhi yao  kurudishwa nyumbani kwao hatua iliyofanya pia  kukosa kufanya  baadhi ya mitihani.
 
“Tulidhani ni mzaha lakini muda ulivyozidi hali ilikuwa mbaya zaidi ,tuliwafunga kamba za  mikono na miguu ili kudhibiti kukimbia holela na wengine kumi hawajarudi shuleni hadi leo  wapo majumbani kwao na wazazi hawajarudisha mrejesho juu ya afya zao aah ni tukio la kwanza” alisema Seleman.
 
Hata hivyo   wanafunzi wapatao kumi  kati yao bado wapo majumbani na watano walifanyiwa maombi na mchungaji wa kanisa moja la kilokole la wilayani humo Mwamko Lutego ambapo alidai walikutwa na nguvu za pepo na kufanikiwa kuyafukuza kwa mujibu wa imani ya dini yao huku ikithibitika kuwa hali zao zimeanza kuimarika.

Diwani wa kata ya Kumsenga Simoni Kanguye ambaye alifuatana na  timu ya wauguzi na mganga wa wilaya  pamoja na mchungaji huyo  katika kufuatilia hali na kutathimini uhalisia wa chanzo cha maradhi hayo ya aina yake,alisema  hali hiyo imewashangaza sana kwakuwa baada ya kuwapima wanafunzi hao walikuwa hawana ugonjwa wa aina hiyo.

Aidha shule hiyo ni ya mchanganyiko pia ina mabweni ya wanafunzi wa jinsia zote,lakini adha hiyo huwakumba wanafunzi wa kike pekee.

Friday, September 26, 2014

KINANA ASHIRIKI KAZI ZA KIJAMII MJINI KOROGWE

12
Mifereji ya maji kwenye shamba la skimu ya Mahenge

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyeka majani kwenye eneo la soko la sabasaba mjini Korogwe.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kujenga zahanati Mahenge kwa Mndolwa.
Mbunge wa Korogwe mjini Bw. Yusuph Nassir akielezea mipango ya maendeleo ya jimbo lake wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya Mahenge Kwamndolwa .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa vyumba vya maabara vya shule ya sekondari ya Old Korogwe.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Korogwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi ambapo aliwaasa vijana kuwa makini na wanasiasa wanaotanguliza madaraka kuliko utu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa Korogwe walifurika kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi hao kuchagua viongozi bora kwenye chaguzi zote zijazo,kuhakikisha watoto wao wanaenda shule na wasirudishwe kwa sababu ya ada na mwisho aliwasisitiza wakazi wa Korogwe kujiunga na mifuko ya Afya ya jamii.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mheshimiwa Mrisho Gambo kusalimia wananchi wa Korogwe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Mazoezi.
 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mheshimiwa Mrisho Gambo akiwahutubia wakazi wa Korogwe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi ya Mazoezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Korogwe kwenye mkutano uliokuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa na shauku ya kuuliza maswali kuhusu maendeleo yao ya Korogwe.
(Picha na Adam Mzee)

MASHINDANO YA VIPAJI VYA WANAWAKE (WOMEN TALENT SYSTEM) YALIVYOFANA KATIKA HOTELI YA JB BELMONT SEPTEMBA 25-2014.

1[3]Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe, Fabiola Massula (kushoto) akizungumza wakati wa mashindano ya vipaji vya wanawake (WOMEN TALENT SYSTEM) ilifanyika Septemba 25,2014 katika Hotel ya JB BELMONT jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mshereheshaji wa shoo hiyo. Benki hiyo ni mmoja wa wadhamini wa shoo hiyo.2[1]Mkurugenzi wa Women Talent System, Angels Howell (katikati) akizungumza jambo kuhusiana shoo hiyo (kulia kwake), Meneja kutoka Mmi Tanzania, Paolo Frattari.3[1]Rais wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa  Martina Maurizio (kushoto), akipiga makofi kushiria kufulaishwa na jambo wakati wa mashindano ya vipaji vya wanawake (WOMEN TALENT SYSTEM) ilifanyika Septemba 25,2014 katika Hotel ya JB BELMONT jijini Dar es Salaam.4[1]Wageni waalikwa pamoja na wasanii wakifuatilia shoo hiyo.5[1]Wacheza shoo walioandaliwa kutoa burudani wakionesha uwezo wao.6[1]Rais wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa  Martina Maurizio akionesha uwezo wake wakuvunja vibao kwakutumia mkono.7[1]Profesa  Martina Maurizio akionesha uwezo kwa jiwe lilokuwa limewekwa kifuani kwake na kunjwa kwakutumia nyundo.8[1]Profesa  Martina Maurizio akionesha uwezo kwa jiwe lilokuwa limewekwa kifuani kwake na kunjwa kwakutumia nyundo.9[1]
10[1]Wacheza shoo walioandaliwa kutoa burudani wakionesha uwezo wao.

KAMPUNI YA PLATINUM YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA SHIMIWI.

SH1 Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Platinum Credit Ltd Bw. Elias Samwel akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo kwa baadhi ya Timu za Wizara na Taasisi za Serikali leoj jijini Dar es Salaam, vifaa hivyo vimetolewa ili kusaidia timu hizo zinazoshiriki mashindano ya SHIMIWI ambayo mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 27 Septemba hadi tarehe 11 Oktoba mkoani Morogoro.Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa SHIMIWI Moshi Makuka.SH2Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga akimtunuku cheti Mwakilishi wa Platinum Credit Ltd Bw. Ferdinand Kambanyumba ikiwa ni kutambua na kuthamini mchango wao katika kuendeleza michezo wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa Wizara watakaoshiriki mashindano ya SHIMIWI 2014
SH3a
SH3Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Concilia Niyibitanga akipokea kwa niaba ya Katibu Mkuu, msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya Platinum Credit Ltd Bw. Ferdinand Kambanyuma wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa baadhi ya timu za Wizara na Taasisi za Serikali zinazotarajia kushiriki mashindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 27 mwezi huu na kumalizika tarehe 11 Oktoba mkoani Morogoro.SH4Kaimu Katibu Mkuu wa SHIMIWI Bw. Moshi Makuka (kulia) akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Platinum Credit Ltd Bw. Elias Samwel wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa baadhi ya timu za Wizara na Taasisi za Serikali zinazotarajia kushiriki mashindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 27 mwezi huu na kumalizika tarehe 11 Oktoba mkoani Morogoro.SH5Mwenyekiti Timu ya Utumishi Bw. Lumuli Mtaki (kushoto) akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Platinum Credit Ltd Bw. Elias Samwel wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa baadhi ya timu za Wizara na Taasisi za Serikali zinazotarajia kushiriki mashindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 27 mwezi huu na kumalizika tarehe 11 Oktoba mkoani Morogoro.
Picha na Frank Shija, WHVUM

MKUTANO WA WANAHISA WA TBL WAFANA.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Cleopa Msuya akifafanua jambo, wakati akizungumza na wana hisa wa kampuni hiyo, wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka, uliofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Bw. Roberto Jarrin na Kampuni wa Kampuni hiyo, Bw. Huruma Ntahema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Cleopa Msuya akifafanua jambo, alipozungumza na wana hisa wa kampuni hiyo, wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka, uliofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Bw. Roberto Jarrin. (Na Mpigapicha Wetu)
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin (kulia), akitata jambo na Maofisa wa shirika hilo, Mkurugenzi wa Afrika Mashariki, Bw. Mario Van Gelden (kushoto) na Mkurugenzi wa Rasilimari watu, Bw. David Magese, wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wana hisa, uliofanyika Dar es Salaam
 Mkurugenzi akibadilishana mawazo na baadhi ya wanahisa wa TBL
Msuya akibadilishana mawazo na viongozi wa TBL WAKATI WA MKUTANO HUO
 Baadhi ya wanahisa wakiwa katika mkutano huo
 Mmoja wa wanahisa akiuliza swali katika mkutano huo
 Mwanahisa akiuliza swali katika kijiji hicho
 Meza kuu
 Wanahisa