Pages

KAPIPI TV

Friday, September 19, 2014

TANZANIA NA THAILAND WAKUBALIANA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA MADINI.

pix 1Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo (mwenye shati la batiki), akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito wa Thailand, walipotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya 54 ya Vito na Usonara ya Bangkok, yaliyofanyika Septemba 9 hadi 13 mwaka huu.
pix 2Makamu wa kwanza wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara wa Thailand, Bw. Sutipong Dumrongsakul, akimkabidhi zawadi maalumu Mkuu wa Ujumbe kutoka Tanzania ulioshiriki maonesho ya vito ya Bangkok, Archard Kalugendo, mara baada ya kikao kati ya Ujumbe huo na Viongozi wa Taasisi hiyo ya Wafanyabiashara wa Thailand.
pix 3Wateja mbalimbali wakihudumiwa katika Banda la Tanzania kwenye maonesho ya vito na usonara ya Bangkok yaliyofanyika hivi karibuni nchini Thailand.Baadhi ya Watanzania walioshiriki maonesho ya vito na usonara nchini Thailand, wakimsikiliza mmoja wa wateja aliyetembelea Banda la Tanzania.
pix 5Ujumbe wa Tanzania (Kulia) wakiwa katika kikao na Uongozi wa juu wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara wa Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa maonesho ya vito na usonara ya Bangkok.
pix 6Baadhi ya Watanzania walioshiriki maonesho ya vito na usonara ya Bangkok, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungwa rasmi kwa maonesho hayo.
pix 7Watanzania walioshiriki maonesho ya vito na usonara ya Bangkok walitumia fursa ya maonesho hayo kutangaza pia utamaduni na vivutio mbalimbali vya utalii vipatikanavyo nchini Tanzania. Pichani ni Eva Mowo (kushoto) Afisa kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Lightness Makundi, Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakiwa wamevalia mavazi ya kimasai.
pix 8Ujumbe wa Tanzania ulioshiriki katika maonesho ya vito na usonara ya Bangkok pia walitumia fursa ya maonesho hayo kutangaza maonesho ya vito ya Arusha yanayotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu jijiji Arusha. Pichani ni Eva Mowo, Afisa kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Lightness Makundi, Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa wamepozi katika bango lenye ujumbe wa kutangaza maonesho ya Arusha. Maafisa hao walivalia mavazi ya asili (vitenge) na mikufu yenye vito vya Tanzanite kutangaza utamaduni wa Kitanzania na madini hayo maarufu ya vito yapatikanayo Tanzania pekee.  
pix 9Makamu wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito – Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa Maonesho ya Vito ya Bangkok, Tony Brooke akizungumza na baadhi ya Watanzania walioshiriki katika Maonesho hayo nchini Thailand alipotembelea Banda la Tanzania. Sambamba naye (mwenye shati la kitenge) ni Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania katika maonesho hayo, Archard Kalugendo.
 
Tanzania, Thailand kushirikiana katika madini vito
 
Na Veronica Simba – Aliyekuwa Bangkok
Wafanyabiashara wa madini ya vito na usonara wa Thailand wameonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania katika sekta hiyo kwa lengo la kukuza uhusiano na kuzinufaisha pande zote mbili.
 
Hayo yalibainika hivi karibuni katika kikao kilichokutanisha Ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Maonesho ya Vito na Usonara yaliyofanyika Bangkok nchini Thailand na Uongozi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa madini hayo kutoka nchini humo.
 
Akiwasilisha  maoni na mapendekezo kutoka upande wa Tanzania katika kikao hicho, Kiongozi wa Ujumbe kutoka Tanzania, Archard Kalugendo ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), alisema Tanzania inapenda kushirikiana na Wa-Thailand katika sekta hiyo ili pamoja na mambo mengine kuiga na kujifunza kutoka kwao.
 
“Ninyi wenzetu mmeendelea sana katika sekta hii ya madini ya vito na usonara. Tunapenda kujifunza na kuiga kutoka kwenu ili nasi tufike hapo mlipofikia na hata zaidi ya hapo,” alisema Kalugendo.
 
Aliongeza kwamba, lengo la Serikali ya Tanzania ni kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha inawawezesha wananchi wake hususan wanaojishughulisha na biashara ya madini ya vito na usonara ili wanufaike ipasavyo kupitia kazi hiyo na pia kulinufaisha Taifa kwa ujumla kwa kukuza uchumi wa nchi.
 
Alisema, Serikali inayo nia na imejipanga kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara ya madini ya vito na usonara katika Bara la Afrika na kwamba inatumia njia mbalimbali kufanikisha hilo ikiwemo kuendelea kuboresha Maonesho ya Vito na Usonara ya Arusha (Arusha Gem Fair – AGF) yanayofanyika kila mwaka.
 
Kalugendo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha Wafanyabiashara wa Thailand katika Maonesho ya Vito ya Arusha yanayotarajiwa kufanyika mapema mwezi Novemba mwaka huu jijini Arusha.
“Tanzania inayo mazingira mazuri sana ya uwekezaji na ninawahakikishia kuwa ushiriki wenu katika maonesho hayo utakuwa wenye tija kwenu na kwetu pia,” alisema.
 
Aidha, Kalugendo alitoa maombi ya Tanzania kupatiwa nafasi kubwa zaidi katika Maonesho ya Vito na Usonara ya Thailand ili washiriki wengi zaidi wakiwemo wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hayo waweze kushiriki na kujipatia uzoefu utakaowasaidia kuboresha utendaji wao na hivyo kumudu ushindani katika soko na viwango vya kimataifa.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Maonesho ya Vito na Usonara ya Arusha, Peter Pereira alisisitiza umuhimu wa Thailand kushiriki katika maonesho ya Arusha na kuwahakikishia kuwa mazingira mazuri yameandaliwa kwa ushiriki wenye tija ikiwemo kuondoa gharama za kodi ya thamani katika bidhaa (VAT) kwa kipindi chote cha maonesho.
 
Akijibu hoja na mapendekezo kutoka upande wa Tanzania, Makamu wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito – Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa Maonesho ya Vito ya Bangkok, Tony Brooke alisema Thailand inapenda kushirikiana kwa ukaribu zaidi na Tanzania katika sekta hiyo.
 
Alisema Wafanyabiashara wa Thailand watashiriki katika maonesho ya vito ya Arusha na kuahidi kuboresha ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya vito ya Bangkok.
 
Brooke alitoa changamoto kwa Tanzania kujiandaa vema zaidi katika ushiriki wa maonesho kama hayo kwa kuhakikisha inapeleka madini na bidhaa kwa wingi kulingana na uhitaji wa wateja.
 
“Wateja wengi wanatembelea banda la Tanzania kuliko madini na bidhaa zilizopo. Ongezeni wingi wa bidhaa maana uhitaji ni mkubwa,” alisisitiza Brooke.
 
Alikubaliana na wazo la kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha madini ya vito na usonara katika bara la Afrika na kusisitiza kufanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma kwa hali juu ili kuhakikisha lengo hilo linatimia.
 
“Hatua mnayoona tumefikia katika sekta hii ya madini ya vito na usonara imekuja kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma, hivyo nanyi ili mfanikiwe mnapaswa kufanya hivyo,” alisema.
 
Nchi ya Thailand ina uzoefu wa miaka 40 katika biashara ya madini ya vito na usonara na imekuwa ikiandaa maonesho makubwa kila mwaka katika kipindi hicho chote ili kuuza bidhaa zitokanazo na madini ya vito na kujitangaza zaidi kimataifa.
 
Maonyesho ya Vito na Usonara ya Bangkok kwa mwaka huu yalifanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 na kushirikisha mataifa mbalimbali duniani.

MTOTO ALIYEZALIWA BILA SEHEMU YA KUTOLEA HAJA KUBWA AFANYIWA UPASUAJI

Na Allan Ntana, Sikonge

MTOTO Pili Ibrahimu (4) aliyezaliwa mwezi Februari 2010 katika zahanati ya Mole iliyoko katika kijiji cha Mole Kiloleli kata ya Mole wilayani Sikonge mkoani Tabora bila kuwa na sehemu ya kutolea haja kubwa amefanyiwa operesheni na madaktari bingwa katika hospitali ya Rufaa Bugando ili kumwezesha kuwa na kiungo hicho muhimu katika mwili wake.

Binti huyo alifanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo wiki mbili zilizopita baada ya wasamaria wema kujitokeza na kutoa michango ya fedha kiasi cha sh mil 2 ili kufanikisha safari ya kumpeleka hospitali ya Rufaa Bugando iliyoko jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu kama wazazi wake walivyokuwa wameshauriwa na wataalamu wa afya.

Mafanikio ya safari na matibabu ya mtoto Pili kwa kiasi kikubwa yalichangiwa na moyo wa huruma na jitihada za kipekee zilizofanywa na Meneja wa shirika la Care International wilayani Sikonge Waziri Rashid Njau kwa kushirikiana na Muuguzi wa zahanati ya kijiji hicho Bi.Deodata Raphael Lyimo aliyetoa taarifa za kuwepo kwa mtoto mwenye tatizo hilo.

Baada ya kupata taarifa za Pili, Njau alilazimika kusambaza taarifa za mtoto huyo katika mitandao mbalimbali ya kijamii ili kutafuta msaada toka kwa wasamaria wema jambo ambalo liligusa watu wengi sana ndani na nje ya mkoa wa Tabora na kuanza kutoa michango yao.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mtoto huyo kurejea kutoka Bugando alikofanyiwa upasuaji, ‘Njau akiwa amejawa na furaha’, alitoa shukrani zake za dhati kwa watu wote walioguswa na tatizo la mtoto huyo na kutoa msaada uliowezesha kupelekwa Bugado kwa ajili ya upasuaji zoezi lililofanyika kwa mafanikio makubwa.
 
Njau alibainisha kuwa Pili alikuwa anateseka sana kwa sababu haja kubwa ilikuwa inatokea sehemu ya haja ndogo na kupata maumivu makali sana kila wakati kwa kipindi chote hicho cha miaka minne jambo lililomfanya akimbiwe na watoto wenzake na kubaki mpweke.

Akizungumzia tatizo hilo mama mzazi wa Pili, Hamisa Masudi (35) alisema hali ya mwanae ilishamkatisha tamaa hasa ukizingatia kuwa anaishi maisha ya umaskini sana na hakuwa na uwezo wowote wa kumpeleka kwenye hospitali kubwa na mbaya zaidi mume wake alishamkimbia baada ya kuona amejifungua mtoto mwenye ulemavu.

Naye Deodata Raphael Lyimo muuguzi wa zahanati ya Mole alipongeza jitihada zilizofanywa na shirika la Care International kupitia mradi wake wa TABASAMU ambazo zimefanikisha matibabu ya mtoto huyo na sasa anaendelea vizuri huku akibainisha kuwa msaada zaidi bado unahitajika kwa vile mtoto huyo anatakiwa kupelekwa tena Bugando mwezi ujao kwa ajili ya uchunguzi wa maendeleo ya upasuaji uliofanyika.

Aidha alimshukuru Meneja wa Care International wilayani Sikonge kwa utayari wake na moyo wa kujali kwani baada ya kupewa taarifa za kuwepo kwa mtoto mwenye tatizo hilo kijijini hapo wakiwa katika ziara ya kukagua huduma za afya ya uzazi kwa wajawazito katika vituo vya afya na zahanati aliagiza mtoto huyo aletwe mara moja amwone.

NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AENDELEA NA ZIARA MKOANI PWANI

 
2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi mara baada ya kukagua jengo la wazazi katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe leo wakati alipofanya ziara katika jimbo hilo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mkoa wa Pwani akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo pamoja na kuimarisha uhai wa chama, Katibu Mkuu huyo katika ziara hiyo anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC, Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KISARAWE) 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Nape Nnauye kulia, na kada wa CCM Bw. Iddi Janguo mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la wazazi katika hospitali hiyo. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimjulia hali mama mmoja anayeuguliwa na mtoto wake ambaye jina lake halikupatikana mara moja aliyelazwa katika hospitali ya Kisarawe wodi ya watoto wakati alipotembelea wodi hiyo. 5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa moja ya majengo yanayokarabatiwa katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe. 6Moja ya majengo yanayojengwa katika hospitali hiyo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aki 8Jengo jipya linalojengwa katika kata ya Palaka9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa zahanati hiyo katika kijiji cha Palaka 11Katibu Mkuu wa CCM akishuhudia jinsi vijana wanavyofyatua matofali ya bei nafuu mradi ambao umebuniwa na Shirika la Numba kwa ajili ya kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana. 14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali ya ujenzi wa maabara ya sekondari ya Gongoni Kata ya Manerumango 15Wananchi wa kata ya Manerumango wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Nape Nnauye Katibu wa NEC, Siasa, Itikadi na Uenezi wakati wa mkutano wa hadhara katika kata ya Manerumango, Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao. 17 Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kisarawe Mzee Athman Janguo akisalimia wananchi huku Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Bi Joyce Masunga akiwa pembeni. 19Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Mwantumu Mahiza akizungumza na wana Kisarawe katika mkutano wa hadhara uliofanyika Manerumango leo 20 Nape Nnauye Katibu wa NEC, Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo. 21Umati uliohudhuria katika mkutano huo 22Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi na kuendesha mahakama ya wazi ya wananchi. 23Seleman Said Jafo mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza na wananchi wake katika kata ya 

25
Manerumango  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaliswa kwenye kigoda kama ishara ya upendo na kukubalika.26Wana CCM wakila kiapo mara baada ya kupokea kadi zao za uanachama wa CCM,

Wednesday, September 17, 2014

TFDA YAFUNGIA MACHINJIO YA MANISPAA KIGOMA



Na Magreth Magosso Kigoma


Mamlaka  ya  Chakula  Dawa na Vipodozi (TFDA ) imezifungia machinjio ya nyama zilizopo katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji mkoani hapa   kwa sababu ya kukithiri kwa uchafu sanjari na kukosa vigezo bora na taratibu za afya ili kuepusha  hatari  ya  kuenea kwa magonjwa ya mlipuko hasa ugonjwa wa Kimeta.


Akithibitisha hilo Mkuu wa idara mifugo na  uvuvi  Dr.John Shauri  alisema wamalaka ilifika hapo mwaka 2005 na iligundua madhaifu bora ya kuendelea kutoa huduma hiyo kwa jamii kutokana na machinjia yote yalikuwa chini ya kiwango cha sheria ya mwaka 2003.


“shida hazina vyoo,maji na shimo la kutupia mizoga ambapo kitaalamu ni kosa aha tumeboresha haraka machinjio ya kibirizi juzi kwa kuweka nyavu ili mbwa wasirukie nyama na kuhatarisha afya za walaji machinjio ya ujiji hatari ugonjwa wa kimeta hauepukiki sakafu mashimo maji yanatwama ,mizoga inatupwa hovyo  ” alibainisha Dkt.Shauri .


Msimamizi wa machinjio ya Kibirizi Lucas Bandiliki  alisema kuwa alikuja mtalaamu wa TFDA na kukagua eneo la machinjio na kutoa amri yafanyike marekebisho haraka kabla hazijachinjwa ng’ombe.


“nimeona nyavu leo asubuhi, mwenzangu alisema alikuwepo mganga wa manispaa  usiku wa kuamkia leo akiwa na mafundi  wakiweka nyavu ,ilikuwa usiku ,sisi tunafuata magizo kutoka kwa wakubwa” alisema Badilika.


Jamboleo likafanya mahojiano na mfanyabiashara wa kuuza na kusamabaza nyama  Laini Ramadhani  na Rama Yahaya  wakiri machinjio haina maji na hulazimika  kubeba nyama kichwani na kuziosha  mwalo wa Forodhani  na  kufungwa  kwa  Machinjio ya Ujiji  inawapa gharama kubwa katika utoaji wa huduma husika.



Kwa upande  wa Mwenyekiti  Nuru Sadiki na Diwani wa kata ya Kitongoni Kassim Zaid kwa nyakati tofauti walisema wanaunga mkono kufungwa kwa machinjio hiyo kutokana na kukosa sifa za usafi,kwa kuwa haina choo , maji hivyo inaweza kusababisha magonjwa kutoka kwenye  nyama .


 Walisema mapungufu yanachangiwa na hujuma na ushindani wa kisiasa hali inayochaochea  kudorora huduma za jamii kwa wakati,ambapo kikao cha DCC ,desemba,2008 ilipangiwa bajeti ya milioni 142 kwa ajili ya kuboresha  machinjio ya kisasa na bajeti ya mwaka 2013/14 ilitengwa milioni 140 halikutekelezwa na kushauri  wasimamie kuboresha  adha za jamii waache siasa kwenye tija.



Akijibia hilo   Meya wa Manispaa, Bakari Beji  alisema mapungufu  ni makubwa katika machinjio ya ujiji ikiwemo mashimo, kutokuwa na uzio na shimo la kuhifadhi damu  ilibidi  yafungiwe mpaka yatakapokarabatiwa.


Alisema kuwa mwaka jana walitenga shilling 1200,000/= ili kukalabati machinjio lakini pesa hazikupatikana na kwa mwaka huu walitenga shilingi 2500,000/= kwa lengo hilohilo lakini   pesa za miradi hazijafika na  zikifika zitatumika ipasavyo.


Aidha  Manispaa ina  maeneo ya  mawili ya Ujiji na  ya kibirizi ila iliyofungwa ni ile ya Ujiji kutokana na kuwa na mapungufu mengi ambayo yanahatarisha afya za walaji wa nyama hapa mkoani.

SAFARI YA KINANA KUTOKA NYAMISATI MPAKA MAFIA KWA BOTI YA KIZAMANI

16Ilikiwa ni safari ngumu lakini yenye mafunzo mengi nikiwa nimepanda kwenye boti ya Doria wakati wa msafara wa Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na msafara wake tukitokea Nyamisati kuelekea Mafia ambapo katibu Mkuu huyo yupo katika ziara ya kikazi ya mikoa ya Pwani, Tanga na Iringa akikagua miradi ya mendeleo inayotekelezwa na serikali kupitia ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Nilipangiwa kupanda boti hii ya mwendo kasi ili kupata taswira za msafara kwa ujumla na hizi ndiyo tawira zenyewe endelea kuperuzi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-PWANI) 5Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jamno pamoja na wabunge wa Mafia Abdulhimid Shah kulia na Abdull Marombwa wakati Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnnauye alipokuwa akiwaaga wananchi katika mji wa Nyamisati wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ukielekea Mafia wakati akiwa katikaziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo. 12Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnnauye akiwa pamoja na wananchi mara baada ya kupanda kwenye boti kuelekea kisiwani Mafia jana. 13Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na mbunge wa Mafia Mh. Abdulhimid Shah wakipungia mkono wananchi mara baada ya boti hiyo kuondoka katika pwani ya Nyamisati. 17Boti ikikata mawimbi baharini huku bendera za CCM zikipepea. 18Mawimbi makali kidogo lakini ndiyo mwendo wenyewe. 21Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wakiwa kwenye mtumbi kuelekea pwani ya Mafia baada ya kushuka kwenye boti wakati msafara ulipowasili kiwani humo jana. 24Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wakiwa kwenye mtumbi kuelekea pwani ya Mafia baada ya kushuka kwenye boti wakati msafara ulipowasili kiwani humo jana. Katikati anayepunga mkono ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe Mlao 26Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi pamoja na mbunge wa Mafia Mh. wakiwa Mafia Mh. Abdulhimid Shah kwenye pwani ya Mafia baada ya kushuka kwenye boti wakati msafara ulipowasili kisiwani humo jana. 27Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitoa burudani mara baada ya kwasili kisiwani Mafia jana. 28Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi katika uwanja wa stendi ya mabasi mjini mafia jana. 29Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stendi jana mjini Mafia. 30Mh. Abdulhimid Shah mbunge wa Mafia akiwahutubia wananchi wa jimbo lake. 31Naibu Waziri wa Nishati nishati na madini Mh. Charles Kitwanga akiwahutubia wananchi wa Mafia na kuwaelezea mipango ya serikali juu ya huduma ya umeme katika kisiwa hicho.

Monday, September 15, 2014

TASWIRA BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA CHADEMA 2014

MATOKEO YA UCHAGUZI 


MWENYEKITI 

Mh Freeman Mbowe amepata kura 789
Mh Gambaranyere Mwangateka amepata kura 20

MAKAMU BARA

Prof Abdallah Safari amepata kura 775
Hakuwa na Mpinzani

MAKAMU ZANZIBAR

Mh Said Issa Mohamed amepata kura 645
Mh Hamad  Yusuph amepata kura 163