Mamlaka ya Chakula
Dawa na Vipodozi (TFDA ) imezifungia machinjio ya nyama zilizopo katika Manispaa
ya Kigoma-Ujiji mkoani hapa kwa sababu ya kukithiri kwa uchafu sanjari na
kukosa vigezo bora na taratibu za afya ili kuepusha hatari ya
kuenea kwa magonjwa ya mlipuko hasa
ugonjwa wa Kimeta.
Akithibitisha hilo Mkuu wa idara mifugo na uvuvi Dr.John Shauri alisema wamalaka ilifika hapo mwaka 2005 na
iligundua madhaifu bora ya kuendelea kutoa huduma hiyo kwa jamii kutokana na
machinjia yote yalikuwa chini ya kiwango cha sheria ya mwaka 2003.
“shida hazina vyoo,maji na shimo la kutupia mizoga ambapo
kitaalamu ni kosa aha tumeboresha haraka machinjio ya kibirizi juzi kwa kuweka
nyavu ili mbwa wasirukie nyama na kuhatarisha afya za walaji machinjio ya ujiji
hatari ugonjwa wa kimeta hauepukiki sakafu mashimo maji yanatwama ,mizoga
inatupwa hovyo ” alibainisha Dkt.Shauri
.
Msimamizi wa machinjio ya Kibirizi Lucas Bandiliki alisema kuwa alikuja mtalaamu wa TFDA na
kukagua eneo la machinjio na kutoa amri yafanyike marekebisho haraka kabla
hazijachinjwa ng’ombe.
“nimeona nyavu leo asubuhi, mwenzangu alisema alikuwepo
mganga wa manispaa usiku wa kuamkia leo
akiwa na mafundi wakiweka nyavu ,ilikuwa
usiku ,sisi tunafuata magizo kutoka kwa wakubwa” alisema Badilika.
Jamboleo likafanya mahojiano na mfanyabiashara wa kuuza na kusamabaza
nyama Laini Ramadhani na Rama Yahaya wakiri machinjio haina maji na hulazimika kubeba nyama kichwani na kuziosha mwalo wa Forodhani na
kufungwa kwa Machinjio ya Ujiji inawapa gharama kubwa katika utoaji wa huduma
husika.
Kwa upande wa
Mwenyekiti Nuru Sadiki na Diwani wa kata
ya Kitongoni Kassim Zaid kwa nyakati tofauti walisema wanaunga mkono kufungwa
kwa machinjio hiyo kutokana na kukosa sifa za usafi,kwa kuwa haina choo , maji
hivyo inaweza kusababisha magonjwa kutoka kwenye nyama .
Walisema mapungufu yanachangiwa na hujuma na ushindani wa
kisiasa hali inayochaochea kudorora
huduma za jamii kwa wakati,ambapo kikao cha DCC ,desemba,2008 ilipangiwa bajeti
ya milioni 142 kwa ajili ya kuboresha machinjio ya kisasa na bajeti ya mwaka 2013/14
ilitengwa milioni 140 halikutekelezwa na kushauri wasimamie kuboresha adha za jamii waache siasa kwenye tija.
Akijibia hilo Meya
wa Manispaa, Bakari Beji alisema
mapungufu ni makubwa katika machinjio ya
ujiji ikiwemo mashimo, kutokuwa na uzio na shimo la kuhifadhi damu ilibidi
yafungiwe mpaka yatakapokarabatiwa.
Alisema kuwa mwaka jana walitenga shilling 1200,000/= ili
kukalabati machinjio lakini pesa hazikupatikana na kwa mwaka huu walitenga
shilingi 2500,000/= kwa lengo hilohilo lakini
pesa za miradi hazijafika na
zikifika zitatumika ipasavyo.
Aidha Manispaa ina maeneo ya mawili ya Ujiji na ya kibirizi ila iliyofungwa ni ile ya Ujiji
kutokana na kuwa na mapungufu mengi ambayo yanahatarisha afya za walaji wa
nyama hapa mkoani.
No comments:
Post a Comment