Pages

KAPIPI TV

Tuesday, August 5, 2014

MFUKO WA FURSA SAWA KWA WOTE(EOTF)WAKABIDHI MSAADA WA VITABU KWA TAASISI 48 ZA ELIMU NCHINI


pix 1 (6)Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote(EOTF), Emmanuel  Matee akielezea historia ya mfuko huo kwa wadau mbalimbali wa elimu katika hafla ya kupokea vitabu kwa ajili ya shule za Msingi, Sekondari na Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka Marekani leo jijini Dar es Salaam.
pix 2 (4)Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote(EOTF), Mama Anna Mkapa akitoa neno la shukrani kwa wahisani wakati wa hafla ya kukabidhi  vitabu kwa ajili ya kusaidia  shule 45 na vyuo 3 vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bibi.Paulina Mkonongo na katika ni mwakilishi wa Balozi wa Nigeria nchini Bibi. Abiola Delupe.
pix 3 (4)Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimkabidhi kitabu mwakilishi wa Shule ya Sekondari Overland, iliyopo Kisarawe ndg. Allison Sila  wakati wa hafla ya kukabidhi  vitabu kwa ajili ya kusaidia  shule 45 na Vyuo 3 vya Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani na kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria  leo jijini Dar es Salaam.
pix 4 (2)Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimkabidhi kitabu mwakilishi wa Shule ya Msingi Little Hood, Ignas Kamuntu wakati wa hafla ya kukabidhi  vitabu kwa ajili ya kusaidia  shule 45 na Vyuo 3 vya Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani na  kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria n  leo jijini Dar es Salaam.
pix 5 (2)Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimkabidhi kitabu mwakilishi kutoka Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka Bagamoyo, Bibi. Victoria Kessy wakati wa hafla ya kukabidhi  vitabu kwa ajili ya kusaidia  shule 45 na Vyuo 3vya Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani  na kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria  leo jijini Dar es Salaam.
pix 7Mwakilishi kutoka shule ya Sekondari Ujenzi iliyopo Mkuranga ndg. Karumuna Sigsmundi akitoa shukrani kwa Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa kwa niaba ya wawakilishi wa shule zote zilizo kabidhiwa Vitabu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani na kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria   leo jijini Dar es Salaam.
pix 8Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wahisani wa Elimu wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu kwa ajili ya  kusaidia  shule 45 na Vyuo 3 vya Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani na kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria leo jijini Dar es Salaam. Picha na MAELEZO

"WATENDAJI WA SERIKALI BADO WANAENDELEA KUKIUKA HAKI ZA BINADAM,WACHOMA NYUMBA NA VYAKULA VYA WANANCHI WANYONGE"-URAMBO

Baadhi ya masalia ya Majengo na chakula kilichoteketezwa na maafisa wa wakala wa huduma za Misitu katika msitu wa Mishepu North Ugalla uliopo wilayani Urambo mkoani Tabora wakati wakidai kutekeleza zoezi la kuwaondoa watu waliovamia eneo la hifadhi ya msitu huo kitendo ambacho kimetafsirika ni unyama wa hali ya juu.
Kitendo cha uchomaji wa chakula na majengo kimelaaniwa sana na kwamba ni kinyume na haki za binadamu,Afisa misitu wilaya ya Urambo Nicolas Masese adai kuwafanyia hivyo wananchi ni halali kwa mujibu wa sheria.


MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE AZINDUA MAKTABA YA KISASA SHULE YA SEKONDARI CHALINZE

1
2
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni kabla ya kuzindua rasmi maktaba ya shule hiyo, Katikati ni Emma Lyu kutoka taasisi ya Read International na kushoto ni Raquel Araya kutoka Taasisi ya Read International pia.
3
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akionyeshwa vitabu mbalimbali vilivyopo katika maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze na Najma Juma kutoka Chuo Kikuuu cha Dar es salaam UDSM ambaye anafanya kazi za kujitolea katika taasisi ya Read Internional.
4
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakiangalia kitabu wakati akikagua maktaba hiyo kulia kwake ni Najma Juma wa Read International.
6
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakiweka alama za kiganja chake kama kumbukumbu wakati alipozindua maktaba hiyo jana kwenye shule ya sekondari ya Chalinze.
7
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo wakati Mwenyekiti  wa bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni alipokuwa akisoma risala yake mbele ya mbunge huyo, kutoka kulia ni Raquel Araya kutoa taasisi ya Read International na mkuu wa  ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
8
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwetea akizungumza na wanafunzi wa sule ya sekondari ya Chalinze pamoja na walimu mara baada ya kuzindua maktaba katika shule hiyo jana kushoto ni Mbwana Madeni mwenyekiti wa bodi ya shule, na kutoka kulia ni Raquel Araya kutoka Read International na mkuu wa  ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
9
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwetea akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua maktaba hiyo kushoto ni mdau wa masuala ya habari Dk Fadhil Kabujanta wa Fadhaget Sanitarium Clinic ya Mbezi Africana jijini dar es salaam.
11
Meneja masoko wa  Simba Cement Yasin Hussein akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Maktaba ya shule hiyo iliyojengwa na Kampuni hiyo gharama yake ikiwa ni shilingi milioni 42 za kitanzania.

WAKULIMA MBEYA WANEEMEKA NA ELIMU YA UZALISHAJI WA MBOGA MBOGA KUTOKA TAHA


Mh. Dr. Christine Ishengoma Mkuu wa Mkoa wa Iringa akipokea taarifa kuhusu mfumo wa taarifa za masoko kutoka TAHA unavyofanya kazi zake kutoka kwa Cyrila Antony Afisa wa Masoko
Mkuu wa mkoa wa Iringa  Mh. Dr. Christine Ishengoma akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa kilimo wa TAHA Bw Ringo kuhusu uzalishaji wa zao la nyanya 
Elimu ikiendelea kutolewa
 Vitalu na green houses
 Aina Mbalimbali za matunda ambazo zimezalishwa na wakulima kutokana na elimu Bora waliyo ipata kutoka TAHA
 Mwananchi akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa TAHA
 Teknolojia ya umwagiliaji kwa mfumo wa kilimo cha matone ambao pia unaonesha utengenezaji bora wa matuta, nafasi na usafi
Hivi ni  Vitalu vya TAHA na Barton Tanzania
 Vitalu vya mboga na green house kama zinavyoonekana katika picha
 Watangazaji wa Radio Sweet FM ya Mbeya wakishangaa ubora wa karoti ambayo ni daraja la kwanza inapopelekwa sokoni
 Zao la chines
Zao la karoti lililopandwa kwenye vitalu vilivyopo ndani ya viwanja vya Nanenane Mbeya kwenye Banda la TAHA
 Mwananchi akifurahia maelezo kuhusu zao la karoti daraja la kwanza


Wakulima na wananchi mkoani Mbeya
wameendelea kuneemeka na elimu ya bure ya uzalishaji wa mazao ya mboga, viungo
na matunda inayotolewa na Asasi ya wakulima, wafanyabiashara na watoa huduma ya
mazao ya horticulture nchini Tanzania (TAHA).
 
Wakulima hao wameneemeka na elimu
hiyo inayotolewa na maafisa wa ufundi wa kilimo kutoka TAHA kwa ushirikiano na
wale wa Barton Tanzania ambao kwa pamoja wameweka kambi katika viwanja hivyo
ili kuhakikisha jamii ya wakulima wa mboga kutoka ukanda wa Nyanda za Juu
Kusini wanapata elimu ya msingi bora ya uzalishaji wa mboga wenye tija.
 
“Mpaka sasa tumetembelewa na
wananchi na wakulima wasiopungua 460 ambao wamefika katika banda letu hapa
Nanenane kwenye viwanja vya John Mwakangale wakitaka kujifunza mbinu na misingi
ya awali ya uzalishaji wa mazao ya horticulture, hiyo ni ishara njema kwani
inaonesha ni kiasi gani wananchi
wanatafuta mbinu fasaha inayoweza kuwakwamua kutoka katika uzalishaji wa
mboga wa kawaida mpaka uzalishaji wa tija unaozingatia viwango vya kitaifa na
kimataifa” Alisema Likati Thomas afisa Mawasiliano kutoka TAHA.
Akifafanua zaidi kuhusu elimu ya
kilimo cha uzalishaji wa mboga kwenye banda la TAHA afisa mawasiliano huyo
alisema kuwa wamepanda mazao tofauti katika ploti zilizopo kwenye eneo lao
ambapo wakulima na wananchi wanaopata fursa ya kutembelea eneo hilo ujifunza
teknolojia mbalimbali za uzalishaji kama vile uzalishaji unaozingatia Mbegu
bora zenye tija.
 
Teknolojia nyingine ni pamoja na
upandaji mazao unaozingatia nafasi kati ya miche na miche, umwagiliaji kwa njia
ya matone(drip irrigation) unaozingatia uhifadhi wa maji na mazingira pamoja na
ulimaji wa matuta yaliyoinuka ili kutoa nafasi kwa mizizi ya mimea kupenyeza
kwenye udongo ili kujitafutia lishe.
 
Mbali na elimu hiyo ya uzalishaji
wa mboga, wananchi wa Mbeya wanaotembelea banda hilo pia wanapata fursa ya
kujifunza elimulishe kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya lishe wa TAHA Bi.
Lawrencia …..ambaye amekuwa akiwafundisha wananchi juu ya umuhimu wa ulaji wa
mboga na faida zake kwa afya ya miili yetu.

MZEE YUSUPH AINGIA RASMI KWENYE FILAMU NA HII NDIO TRELA YA MUVI YAKE IITWAYO NITADUMU NAYE

Itaanza Kupatikana Kuanzia Jumatatu ya tarehe 11 August 2014 katika Maduka yote Tanzania. Usikose Nakala Yako.

MAHAKAMA YAFUTILIA MBALI KESI INAYOWAKABILI VIONGOZI WA MSIKITI MKUU WA IJUMAA GONGONI-TABORA

Baadhi ya waumini wa dini ya kiislam wakimpongeza aliyekuwa Sheikh wa mkoa wa Tabora Shaaban Salumu muda mfupi mara baada ya mahakama ya hakimu mkazi Tabora kufutilia mbali kesi iliyokuwa ikiwakabili Shaaban Salum na waumini wengine watano ambao walifunguliwa mashitaka ya kutaka kutishia kufanya fujo na kumuondoa eneo la kuongozea Ibada kaimu Sheikh wa mkoa wa Tabora Sheikh Ibrahim Mavumbi katika msikiti mkuu wa Ijumaa Gongoni,....Uamuzi huo wa mahakama umetokana na maombi upande wa Serikali kutaka ifutwe kutokana na kushindwa kuendelea na kesi hiyo ambayo kwa sehemu kubwa ilionesha kuwagawa waislam wa Tabora mjini.




Monday, August 4, 2014

STAR OILS KAMPUNI DADA YA MeTL GROUP YAPATA MKOPO WA BILIONI 100 KUTOKA NBC

DSC_0098
.MetTL yajipanga kupanua soko lake la mafuta Afrika Mashariki na Kusini

Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Mohammed Enterpries Tanzania Limited (MeTL GROUP) kupitia kampuni yake dada ya kuingiza, kuhifadhi na kusambaza mafuta nchini ya Star Oils Ltd. imepata mkopo wa bilioni 100 kutoka kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hafla ya utiliaji saini wa mkopo huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu na Mbunge wa Singida Mjini, Mhe, Mohammed Dewji (MO) amesema mkopo huo utafungua mianya zaidi kwa kampuni ya Star Oils kusambaza mafuta nje na ndani ya nchi.

Amesema kwamba baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya timu ya wataalamu kutoka MeTL makao makuu na maafisa wa NBC kutoka nchini na Afrika Kusini wamefikia makubaliano ya kupata mkopo huo mkubwa na wa aina yake katika sekta ya mafuta hapa Tanzania.
DSC_0141
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji (MO), akizungumza kwenye hafla hiyo ya utiliaji saini wa mkopo wa bilioni 100 za kitanzania.
Amesema kwamba kampuni ya Star Oils ina mipango ya kusambaza mafuta katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la Sahara ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kujipanua kibiashara ndani na nje ya Afrika.

“Mpango huu utaiwezesha Star Oils kupanua malengo yake katika soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na kukuza uzalishaji na usambazaji wake katika ngazi ya Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la sahara,” amesema MO.

MO aliongeza kuwa hatua ambayo kampuni hiyo imefikia ni kubwa kwa kuonyesha dhamira ya kuwekeza na kufanya biashara ya mafuta Afrika mashariki na kusini mwa jangwa la sahara.
“Mkopo huu utasaidia kampuni ya Star Oils kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mafuta ya kwenye soko la Afrika mashariki na kusini mwa Afrika,”
DSC_0068
Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter akizungumza na wageni waalikwa kwa kutaja shughuli mbalimbali na bidhaa huduma za benki hiyo.

“Sisi tuna mipango ya kuanza kusambaza mafuta na bidhaa za Petroli katika nchini za Kusini mwa Afrika kama sehemu ya jitihada za kampuni za kupanua biashara zake katika soko la Afrika,” amesema.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Star Oils Ltd, Nazir Haji amesema kwamba mkopo huo utachochea chachu ya uzalishaji, uhifadhi na usambazaji wa mafuta na kusukuma maendeleo ya sekta mafuta nchini.

Amesema kwamba kampuni ya Star Oils inajipanga kufanya biashara ya mafuta kuwa endelevu hapa nchini na Afrika mashariki ili uchumi wa nchi za Afrika mashariki ziweze kukua kwa kutegemea tija ya uzalishaji wa mafuta.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu amesema kuwa benki hiyo inahitimisha safari ya majadiliano na kampuni mama ya Star Oils, Mohammed Entrepries Tanzania Limited (MeTL GROUP) ya mkopo wa bilioni 100.

“Star Oils ni kampuni dada ya METL ni moja ya makampuni yanayokwenda kasi katika biashara ya ushindani katika Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la sahara na rekodi yao ya mauzo na biashara ni ya kuridhisha,” amesema.
DSC_0060
Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter akionyesha toleo la jarida la “THE AFRICA REPORT” lilioandika mafanikio ya kampuni ya MeTL GROUP zilizomvutia zaidi na kupelekea kuwa na imani na kampuni hiyo na kuamua kufanya biashara nao.

Aliongeza kwamba METL ni moja ya makampuni yalionyesha rekodi nzuri katika biashara ya viwanda, nguo, vinywaji, bima na mafuta na wanastahili kuwezesha kwa kupata mikopo mikubwa na ya muda mrefu kupitia taasisi za kifedha nchini na nje ya nchi,”

“Sisi kwenye benki ya NBC tunayofuraha kubwa kwa kupata nafasi ya kufanya biashara na moja ya makampuni yanayokuja kwa kasi katika bara la Afrika na vile vile NBC ni benki ambayo ipo tayari kusaidia wateja wake,” aliongeza

Bi. Melu alisisitiza kuwa baada ya NBC kuridhisha na shughuli za kibiashara na mzunguko wa fedha wa MeTL wameamua kutoa mkopo huo ili waweze kupanua biashara yao katika masoko ya kimataifa.

Star Oils kwa sasa inatekeleza awamu ya pili ya mradi mkubwa wa kuhifadhi mafuta ya Petroli na baadaye kujenga usambazaji wa mafuta nchi nzima kwa njia ya mlolongo wa vituo vya karibu 200 vya Petroli nchini.
DSC_0082
Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter akipeana mkono wa pongezi na Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe, Mohammed Dewji.

Uwezo wa jumla ya uhifadhi wa kituo hiki juu ya kukamilisha mradi itakuwa lita 68 milioni, kuundwa tu kwa ajili ya kuhifadhi ya Petroli, Gesi Mafuta na mafuta ya taa. Wingi wa bidhaa hizi kwa sasa ni kuuzwa kwa misingi ya jumla na mipango ya baadaye soko lao kupitia vituo vya METL Group vya rejareja vya petroli.

NBC imetiliana saini ya mkopo wa shilingi za kitanzania bilioni 100 na kampuni ya kusambaza mafuta ya jijini Dar es Salaam, Star Oils Ltd katika mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya mafuta nchini.
DSC_0051
Picha juu na chini ni Baadhi ya wafanyakazi wa makampuni ya MeTL GROUP na Benki ya NBC waliouhudhuria hafla hiyo ya utiliaji saini wa mkopo baina MeTL na NBC.
DSC_0081
DSC_0167
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu na Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 100 za kitanzania.
DSC_0169
Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL GROUP, Vipul Kakad (wa pili kulia walioketi) na Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter wakiweka saini zao kwenye mkataba huo.
DSC_0172
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu na Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji wakibadilishana hati za mkopo huo katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
DSC_0184

Picha ya pamoja baina ya MeTL GROUP na NBC baada ya utiliaji saini wa mkopo huo.
DSC_0180
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu, Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji, Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipuk Kakad na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni dada ya MeTL GROUP Star Oils Ltd, Nazir Haji kwenye picha ya pamoja.
DSC_0109
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni dada ya MeTL GROUP Star Oils Ltd, Nazir Haji akitoa shukrani zake kwa NBC.
DSC_0103
Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL GROUP, Vipul Kakad (katikati) na wasaidizi wa Mheshimiwa Mohammed Dewji kwenye hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
DSC_0036
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji akimwonyesha kitu kwenye simu yake ya kiganjani Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu wakati wa hafla hiyo.
DSC_0219
Wafanyakazi wa NBC na MeTL Group wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo.
DSC_0202
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe. Mohammed Dewji (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu (kulia), Mwanasheria Mkuu wa MeTL GROUP, Zakia Riyaz Ali (wa pili kulia), na Vikash KG wa Star Oils Ltd wakati wa hafla hiyo.
DSC_0253
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji akifurahi jambo na mmoja wa wafanyakazi wa NBC wakati wa hafla hiyo.
DSC_0258
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji akiteta na wafanyakazi wa NBC kwenye hafla hiyo.