Baadhi ya waumini wa dini ya kiislam wakimpongeza aliyekuwa Sheikh wa mkoa wa Tabora Shaaban Salumu muda mfupi mara baada ya mahakama ya hakimu mkazi Tabora kufutilia mbali kesi iliyokuwa ikiwakabili Shaaban Salum na waumini wengine watano ambao walifunguliwa mashitaka ya kutaka kutishia kufanya fujo na kumuondoa eneo la kuongozea Ibada kaimu Sheikh wa mkoa wa Tabora Sheikh Ibrahim Mavumbi katika msikiti mkuu wa Ijumaa Gongoni,....Uamuzi huo wa mahakama umetokana na maombi upande wa Serikali kutaka ifutwe kutokana na kushindwa kuendelea na kesi hiyo ambayo kwa sehemu kubwa ilionesha kuwagawa waislam wa Tabora mjini. |
No comments:
Post a Comment