.MetTL yajipanga kupanua soko lake la mafuta Afrika Mashariki na Kusini
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI
ya Mohammed Enterpries Tanzania Limited (MeTL GROUP) kupitia kampuni
yake dada ya kuingiza, kuhifadhi na kusambaza mafuta nchini ya Star Oils
Ltd. imepata mkopo wa bilioni 100 kutoka kwa Benki ya Taifa ya Biashara
(NBC).
Akizungumza
na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hafla ya utiliaji saini wa
mkopo huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu na
Mbunge wa Singida Mjini, Mhe, Mohammed Dewji (MO) amesema mkopo huo
utafungua mianya zaidi kwa kampuni ya Star Oils kusambaza mafuta nje na
ndani ya nchi.
Amesema
kwamba baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya timu ya wataalamu
kutoka MeTL makao makuu na maafisa wa NBC kutoka nchini na Afrika Kusini
wamefikia makubaliano ya kupata mkopo huo mkubwa na wa aina yake katika
sekta ya mafuta hapa Tanzania.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji (MO), akizungumza
kwenye hafla hiyo ya utiliaji saini wa mkopo wa bilioni 100 za
kitanzania.
Amesema
kwamba kampuni ya Star Oils ina mipango ya kusambaza mafuta katika nchi
za Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la Sahara ikiwa ni sehemu ya
mikakati yake ya kujipanua kibiashara ndani na nje ya Afrika.
“Mpango
huu utaiwezesha Star Oils kupanua malengo yake katika soko la kimataifa
ikiwa ni pamoja na kukuza uzalishaji na usambazaji wake katika ngazi ya
Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la sahara,” amesema MO.
MO
aliongeza kuwa hatua ambayo kampuni hiyo imefikia ni kubwa kwa kuonyesha
dhamira ya kuwekeza na kufanya biashara ya mafuta Afrika mashariki na
kusini mwa jangwa la sahara.
“Mkopo
huu utasaidia kampuni ya Star Oils kuongeza uzalishaji na usambazaji wa
mafuta ya kwenye soko la Afrika mashariki na kusini mwa Afrika,”
Mkuu
wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC,
Andre Potgieter akizungumza na wageni waalikwa kwa kutaja shughuli
mbalimbali na bidhaa huduma za benki hiyo.
“Sisi
tuna mipango ya kuanza kusambaza mafuta na bidhaa za Petroli katika
nchini za Kusini mwa Afrika kama sehemu ya jitihada za kampuni za
kupanua biashara zake katika soko la Afrika,” amesema.
Kwa
upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Star Oils Ltd, Nazir Haji amesema
kwamba mkopo huo utachochea chachu ya uzalishaji, uhifadhi na usambazaji
wa mafuta na kusukuma maendeleo ya sekta mafuta nchini.
Amesema
kwamba kampuni ya Star Oils inajipanga kufanya biashara ya mafuta kuwa
endelevu hapa nchini na Afrika mashariki ili uchumi wa nchi za Afrika
mashariki ziweze kukua kwa kutegemea tija ya uzalishaji wa mafuta.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu amesema kuwa
benki hiyo inahitimisha safari ya majadiliano na kampuni mama ya Star
Oils, Mohammed Entrepries Tanzania Limited (MeTL GROUP) ya mkopo wa
bilioni 100.
“Star
Oils ni kampuni dada ya METL ni moja ya makampuni yanayokwenda kasi
katika biashara ya ushindani katika Afrika Mashariki na Kusini mwa
jangwa la sahara na rekodi yao ya mauzo na biashara ni ya kuridhisha,”
amesema.
Mkuu
wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC,
Andre Potgieter akionyesha toleo la jarida la “THE AFRICA REPORT”
lilioandika mafanikio ya kampuni ya MeTL GROUP zilizomvutia zaidi na
kupelekea kuwa na imani na kampuni hiyo na kuamua kufanya biashara nao.
Aliongeza
kwamba METL ni moja ya makampuni yalionyesha rekodi nzuri katika
biashara ya viwanda, nguo, vinywaji, bima na mafuta na wanastahili
kuwezesha kwa kupata mikopo mikubwa na ya muda mrefu kupitia taasisi za
kifedha nchini na nje ya nchi,”
“Sisi
kwenye benki ya NBC tunayofuraha kubwa kwa kupata nafasi ya kufanya
biashara na moja ya makampuni yanayokuja kwa kasi katika bara la Afrika
na vile vile NBC ni benki ambayo ipo tayari kusaidia wateja wake,”
aliongeza
Bi.
Melu alisisitiza kuwa baada ya NBC kuridhisha na shughuli za kibiashara
na mzunguko wa fedha wa MeTL wameamua kutoa mkopo huo ili waweze kupanua
biashara yao katika masoko ya kimataifa.
Star
Oils kwa sasa inatekeleza awamu ya pili ya mradi mkubwa wa kuhifadhi
mafuta ya Petroli na baadaye kujenga usambazaji wa mafuta nchi nzima kwa
njia ya mlolongo wa vituo vya karibu 200 vya Petroli nchini.
Mkuu
wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC,
Andre Potgieter akipeana mkono wa pongezi na Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL
GROUP, Mhe, Mohammed Dewji.
Uwezo
wa jumla ya uhifadhi wa kituo hiki juu ya kukamilisha mradi itakuwa
lita 68 milioni, kuundwa tu kwa ajili ya kuhifadhi ya Petroli, Gesi
Mafuta na mafuta ya taa. Wingi wa bidhaa hizi kwa sasa ni kuuzwa kwa
misingi ya jumla na mipango ya baadaye soko lao kupitia vituo vya METL
Group vya rejareja vya petroli.
NBC
imetiliana saini ya mkopo wa shilingi za kitanzania bilioni 100 na
kampuni ya kusambaza mafuta ya jijini Dar es Salaam, Star Oils Ltd
katika mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya mafuta nchini.
Picha
juu na chini ni Baadhi ya wafanyakazi wa makampuni ya MeTL GROUP na
Benki ya NBC waliouhudhuria hafla hiyo ya utiliaji saini wa mkopo baina
MeTL na NBC.
Mkurugenzi
Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu na Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP,
Mhe Mohammed Dewji wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 100 za
kitanzania.
Makamu
wa Rais wa Makampuni ya MeTL GROUP, Vipul Kakad (wa pili kulia
walioketi) na Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na
Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter wakiweka saini zao kwenye mkataba huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu na Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP,
Mhe Mohammed Dewji wakibadilishana hati za mkopo huo katika hafla
iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja baina ya MeTL GROUP na NBC baada ya utiliaji saini wa mkopo huo.
Kutoka
kushoto ni Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na
Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi.
Mizinga Melu, Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji,
Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipuk Kakad na Afisa Mtendaji Mkuu wa
kampuni dada ya MeTL GROUP Star Oils Ltd, Nazir Haji kwenye picha ya
pamoja.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni dada ya MeTL GROUP Star Oils Ltd, Nazir Haji akitoa shukrani zake kwa NBC.
Makamu
wa Rais wa Makampuni ya MeTL GROUP, Vipul Kakad (katikati) na wasaidizi
wa Mheshimiwa Mohammed Dewji kwenye hafla hiyo iliyofanyika mwishoni
mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji akimwonyesha kitu
kwenye simu yake ya kiganjani Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga
Melu wakati wa hafla hiyo.
Wafanyakazi wa NBC na MeTL Group wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe. Mohammed Dewji (wa pili kushoto),
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu (kulia), Mwanasheria Mkuu
wa MeTL GROUP, Zakia Riyaz Ali (wa pili kulia), na Vikash KG wa Star
Oils Ltd wakati wa hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji akifurahi jambo na mmoja wa wafanyakazi wa NBC wakati wa hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji akiteta na wafanyakazi wa NBC kwenye hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment