Pages

KAPIPI TV

Saturday, August 2, 2014

MANISPAA YA KINONDONI YAFANYA MAKUBWA UTEKELEZAJI ILANI YA CCM JIMBO LA KAWE

*Yatekeleza agizo la Rais Kikwete
*Ni la jimbo kuwa na hospitali kubwa
 NA BASHIR NKOROMO
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeshuhudia makubwa yaliyofanywa na Manispaa ya wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya jimbo la Kawe.

Miongoni mwa miradi ambayo chama kililazimika kumpongeza Meya wa Manispaa hiyo ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, ni utekelezaji wa agizo la Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ya ujenzi wa Hospitali kubwa katika jimbo la Kawe yenye hadhi kama zilivyo za Mwananyamala,
Amana na Temeke.

Katika uteekelezaji agizo hilo la Rais Kikwete ambayo haikuwemo katika ilani, tayari Manispaa ya Kinondoni imeshaanza ujenzi wa hospitali hiyo katika eneo la Mabwepande, kwa jengo la kupokea wagonjwa (OPD), linalotarajiwa kukamilika mwaka huu, ambapo imeelezwa hadi mwishogharama yake itakuwa sh. milioni 288 ambazo kati yake sh. milioni Sh.153 zimeshalipwa kwa mkandarasi.

Wakiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 katika jimbo la Kawe, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni, waliokuwa kwenye ziara hiyo jana, walielezwa kwamba, baada ya kukamilika ujenzi wa jengo hilo la kupokea wagonjwa, utaanza ujenzi wa wodi ya kina mama.

"Ndugu wajumbe, wakati Rais Kikwete akiwa katika kampeni zake katika uchaguzi mkuu uliopita, aliagiza kwamba kila jimbo latika mkoa wa Dar es Salaam, lazima liwe na hospitali yenye hadhi kubwa. Sasa ukiangalia agizo hilo ni kama lilikuwa linatulenga sisi wa jimbo la Kawe, maana Jimbo la Kinondoni ipo ya Mwananyamala, Ilala ipo Amana na Temeke pia ipo, ndiyo sababu tumefanya kila jijitahada kuhakikisha sisi Manispaa tunajenga hospitali hii.", alisema Mwenda.

Wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya CCM, wakiendelea na ziara hiyo, pia walishuhudia mradi mkubwa wa ujenzi wa Shule ya sekondari unaoendelea katika eneo la Mikocheni, unaotekelezwa kwa gharama ya sh. bilioni 1.5 kwenye awamu ya kwanza.

Mwenda alisema, kukamilika kwa shule hiyo kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa adha ambayo imekuwa ikiwapata wananchi wa jimbo hilo kwa watoto wao kwenda maeneo ya mbali wanapojiunga na shule ya sekondari baada ya mitihani ya darasa la saba.

Alisema, ujenzi wa shule hiyo ambao sasa upo kwenye hatua ya orofa ya kwanza, unatarajiwa kukamilika mapema na marajio ni kuwezesha watoto watakaomaliza darasa la saba mwaka huu, kuanza kidato cha kwanza kwenye shule hiyo.

Wajumbe hao pia walitembelea mradi wa ujenzi wa soko la kisasa katika eneo la Bunju B, ambalo ujenzi wake unafanyika ili kuwahamishia wafanyabishara ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao pembezoni mwa barabara ya Bagamoyo katika eneo hilo la Bunju B na hivyo kuhatarisha maisha yao na pia kuharibu mandhari ya mji.

Ujenzi wa soko hilo umekamilika kwa asilimia 90, na taratibu za kuanza kuwahamishia hapo wafanyabiashara zinaendelea kufanywa na mamlaka zinazohusika.

Baadhi ya miradi mingine ambayo wajumbe hao waliikagua na kuonyesha kuwasisimua, ni ujenzi wa wodi na kina mama na nyumba ya mganga ambavyo vimekamilika, katika zahanati ya Ndumbwi
kwenye jimbo hilo la Kawe.

Pia alikagua na kuridhiwa na hatua iliyopigwa na Manispaa ya Kinondoni katika ujenzi wa barabara za Maandazi iliyopo Masasani, na barabara ya Jourunalism iliyopo eneo la Feza, Mikocheni.

HABARI KATIKA PICHA KUHUSU ZIARA HIYO
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wakiwa kwenye Jengo la mapokezi ya wagonjwa (OPD) ambalo linajengwa katika eneo la Mabwepande, likiwa ni sehemu ya Hospitali ya Jimbo la Kawe katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, walipotembelea kiradi mbalimbali ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2010-2015 katika jimbo la Kawe.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yussuf Mwenda, akizungumza na watumishi wa Manispaa hiyo yeye na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni walipofika kwenye mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Jimbo la Kawe unaofanyika Mambwepande, jana.
 Mwenda (wapili kushoto) akikagua ujenzi wa jengo la kupokea wagonjwa (OPD) la hospitali ya Jimbo la Kawe inayojengwa Mabwepande, Dar es Salaam.
 Mwenda akiingia ndani ya chumba cha mapokezi cha jengo hilo la mapokezi ya wagonjwa (OPD) wakati wa ziara hiyo.
 Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohammed Cholage akiwaonyesha wenzake eneo aliloona kuwa ni kama kasoro kwenye ujenzi wa jengo la kupokea wagonjwa (OPD) kwenye hospitali hiyo.
 Mwenda akifanya majumuisho na wajumbe baada ya kutembelea jengo la kupokea wagonjwa (OPD) kwenye Hospitali ya jimbo la Kawe inayojengwa mabwepande.


UJENZI WODI YA KINA MAMA NA NYUMBA YA MGANGA ZAHANATI YA NDUMBWI
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda akiongozwa jana na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ndumbwi, Sophia Kasubi, kuingia kwenye jengo la wodi ya Kina mama ambalo ujenzi wake umekamilika kwa ajili ya zahanati hiyo.
 Mwenda akisaini kitabu cha mapokezi kwenye jengo hilo wodi ya Kina mama kwenye zahanati ya Ndumbwi baada ya kuingia yeye na wageni wenzake
 Mwenda akiongozana na Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni Athumani Sheshe baada ya kukagua nyumba ya mganga kwenye zahanati ya Ndumbwi.
 Mwenda akiagana na watumishi wa zahanati ya Ndumbwi
 Baadhi ya watumishi katika zahanati ya Ndumbwi


UJENZI SHULE YA SEKONDARI KATIKA ENEO LA MIKOCHENI
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akiongoza msafara kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ambayo inajengwa na Manispaa hiyo katika eneo la Mikocheni.
 Mwenda akishiriki ujenzi wa shule hiyo ya sekondari kwa kuchanganya mchanga na saruji wakati wa ziara hiyo.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kinondoni Pili Chande akishiriki ujenzi Shule ya Sekondari inayojengwa Mikocheni, jana. Kushoto ni Mwenda akishuhudia na aliyesimama kulia ni Katibu wa Itikadi na uenezi Kata ya Kawe, Eddy Mlaponi
 Mwenda akizungumza na wajumbe kufanya majumuisho baada ya kukagua shule hiyo ya sekondari Mikocheni na kuridhika kwamba ni mradi mzuri unaopaswa kupigiwa mfano katika utekelezaji wa ilani ya CCM


UJENZI SOKO BUNJU 'B'
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akiongoza msafara kukagua ujenzi wa soko katika eneo la Bunju B jana.
 Mmoja wa wajumbe akilazimika kwenda kukagua hali ya choo kwa ajili ya soko hiyo ipoje kwa ajili ya matumizi ya binadamu?
UJENZI DARAJA MIKOCHENZI FEZA
 Wajumbe wakikagua daraja lililojengwa katika utekelezaji wa ilani ya CCM katika eneo la Mikochezi-FEZA.
Wajumbe wakiwa wameshuka kwenye basi kukagua ujenzi wa barabara ya Maandaazi eneo la Msasani ambayo pia imeboreshwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM. (Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog)

Friday, August 1, 2014

PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI – MBEYA

PG4A8000
uwekezaji  la Nyanda za Juu kusini  kwenye ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya August 1, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A8077
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro  (kushoto) na Mkuu wa WIlaya ya Wanging’ombe,, Esterina Kilasi  kutoka kwenye ukumbi  wa Mkapa jijini Mbeya  baada  ya kufungua Kongamano  la Uwekezaji la Kanda ya Nyanda za Juu Kusini August 1, 2014. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS KIKWETE AWASILI WASHINGTON KUHUDHURIA MKUTANO WA VIONGOZI WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AMERIKA NA AFRICA (US-AFRICA LEADERS SUMMIT)

dc1[1]
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles tayari kwa Mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Amerika na Africa (US-Africa Leaders summit) uliondaliwa na Rais Barak Obama unaoanza Agosti 4-hadi 6, 2014, ambao utatanguliwa na mikutano mingine ya maendeleo ya sekta mbalimbali na uwekezaji  (2-3 Agosti, 2014)  jijini Washington DC. PICHA NA IKULU dc3[1]
dc4[1]

RAIS WA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN AFUNGUA RASMI MAONESHO YA NANE NANE, 2014 KITAIFA, MKOANI LINDI

image_5
photo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein(kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi Mhe. Agnes Hokororo mapema leo Agosti 1, 2014 alipowasili Viwanja vya Gongo tayari kwa ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 21 ya Wakulima na Wafugaji yanayofanyika Mkoani Lindi Kitafa kwa mara ya kwanza tangu yaanzishwe hapa Nchini.
image
Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Kamani akitoa Salaam za Wizara katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein(Meza Kuu)katika ufunguzi wa Maonesho hayo ya Wakulima na Wafugaji ambayo yanafanyika Mkoani Lindi Kitaifa.
image_1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein(katika Jukwaa) akiwahutubia Wakulima, Wafugaji pamoja na Wananchi wa Mikoa ya Kusini yaani Lindi na Mtwara katika Ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Nane Nane Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Gongo, Mkoani Lindi leo Agosti 1, 2014.
image_2
Baadhi ya Washiriki mbalimbali wa Maonesho ya Nane Nane Kitaifa wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar, Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein(hayupo pichani). Waliovaa Tisheti za Bluu ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza toka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Kitengo cha Kilimo na Mifugo.
image_3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Ali Mohamed Shein akipata maelezo toka kwa Maafisa Wataalamu wa Benki Kuu ya Tanzania ya namna Wakulima wanavyoweza kupata dhamna ya Mikopo katika Mabenki mbalimbali hapa Nchini kwa Benki Kuu ya Tanzania alipotembelea Banda hilo leo Agosti 1, 2014 katika Sherehe za Maonesho ya Nane Nane Kitaifa yanayofanyika Mkoani Lindi kwa mara ya kwanza.
image_4
Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni wakicheza ngoma ya kijadi Maarufu sana Mkoani Lindi.

CHUO CHA CBE CHAZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 JIJINI DAR, WADAU MBALIMBALI WAPONGEZA UBORA WA ELIMU INAYOTOLEWA

Picha_na_1[1]
 Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) akikata utepe kuashiria uzindunzi wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Picha_na_2[1]
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiangalia moja ya picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho Januari, 1965. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel Mjema, Mh. Musa Zungu (Mb) jimbo la Ilala,Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda,Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Prof. Mathew Luhanga na Prof.Eliuta Mwageni Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.
Picha_na_3[1]
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (katikati). Nyuma ni bango lenye picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho mwaka 1965.
Picha_na_4[1]
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kwa niaba ya wanafunzi waliosoma katika chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam akizungumza na wadau na wanajumuiya wa Chuo hicho wakati wa  uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho jijini Dar es salaam. 
Picha_na_5[1]
 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema (kulia) akiwaongoza wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Picha_na_6[1]
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda (katikati) akizungumza akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Mathew Luhanga (kushoto).Wengine Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema.
Picha_na_7[1]
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam wakiendelea na shughuli mbalimbali chuoni hapo
Picha_na_8[1]
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema (kulia) akiwakaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Picha_na_9[1]
Wadau mbalimbali  na Wanajumuiya wa Chuo Cha Elimu ya Biashara wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Picha_na_10[1]
Kikundi cha ngoma kutoka Jeshi la Polisi kikiongozwa na Afande Juma Boha Mnyaa kikitoa burudani ya ngoma ya asili ya ya Kibati kutoka Kusini Pemba wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es salaam.

UKAWA WAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR


Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutoa Tamko kuhusu Wito wa Viongozi wa Dini wa kurudi Bungeni.kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema,Mh. Freeman Mbowe na wa pili kulia ni Mwenyeti wa NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia.Kulia ni Katibu Mkuu wa Chadema,Dkt. Wilbrod Slaa.
Viongozi wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakishikana mikono kuashiria umoja mara baada ya kuongea na wandishi wa habari kutoa Tamko la Ukawa kuhusu Wito wa Viongozi wa Dini wa kurudi Bungeni.kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi,Mosena Nyambabe,Mwenyekiti wa Chadema,Mh.Freeman Mbowe ,Mwenyekiti wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba,Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia na Katibu Mkuu wa Chadema,Dkt. Wilbrod Slaa wakiwa nje ya makao makuu ya cuf.

WANANCHI WAMEASWA KUTOLINDANA KWA VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI-KIGOMA

 
 
Na Magreth  Magosso, Kigoma
 
WITO umetolewa kwa viongozi wa serikali za Vijiji  mkoani hapa,waache hulka ya kulindana dhidi ya wahamiaji haramu ,hali inayochangia jamii kuishi kwa kulipizana visasi.
 
Akizungumzia hilo Kamamda wa Polisi wa hapa Frasser Kashai alibainisha kuwa,Julai ,27 ,2014 saa 12.30 jioni , Elias Balandes (36) ambaye ni muhamiaji haramu wa kijiji cha Nyamidaho wilaya ya kasulu amemua mgambo kwa kile kinachodaiwa kulipa kisasi.
 
“alimuua askari mgambo Shaban Mabad(34) kisa kulipiza kisasi kwa mgambo huyo,kwa sababu zinazodaiwa kuwa alimfikisha kwa mwenyekiti wa kijiji mhamiaji  huyo kutokana na kuishi hapo kinyume cha sheria,lakini aliachiwa katika mazingira tata ” alisema Kashai.
 
Aliongeza kwa kusema siku hiyo wakiwa wanakunywa pombe za kienyeji  kilabuni katika  kijiji hicho,ndipo yalitokea marumbano baina ya marehemu na Balandes akishirikiana na Faustine Phidel(55) walimshambulia  mlengwa kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali chini ya ziwa la kushoto na kiganjani.
 
Kashai alisema marehemu alijikongoja peke yake hadi hospitali ya wilaya hiyo ambapo siku ya tatu aliaga dunia,watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi kwa hatua zaidi.Wakati huohuo Mkurugenzi wa idara ya uhamiaji  Ebrosy Mwanguku alisema  changamoto ya uhamiaji haramu  kigoma ni kubwa ambapo baadhi ya  viongozi wa vijiji sio raia halali.
 
Mwanguku alibainisha kuwa,jamii  inalindana  yenyewe kwa yenyewe kutokana na mahusiano ya ukaribu wa kuoleana ,hali inayokwamisha operesheni ya uhamiaji haramu mkoani hapa na kusisitiza wananchi watajihukumu wenyewe kwa kuchezea amani iliyopo.
 
Akichangia hilo Katibu Taifa chama cha NRA Hamis Fadhili  akiri wananchi hutumia fursa za uchaguzi vibaya hasa kuwasimika viongozi  wahamiaji haramu kushika nyadhifa mbalimbali kama udiwani na watendaji wakuu wa vijiji,hali inayochangia kulindana baina ya wahamiaji  wanaoendelea kuja na viongozi husika.
 
Julai 12,mwaka huu  wahamiaji haramu 99 wakiwemo watoto  29 walio chini ya miaka 18 walikamatwa  katika operesheni ya  idara ya uhamiaji  mkoani hapa,ambapo wengi wao hutumiwa kama vibarua katika mashamba ya wananchi wa hapa.
 
Aidha changamoto hiyo inachangiwa na sheria dhaifu za idara hiyo,ambayo jamii huona ni nyepesi na hivyo wengi hushiriki kuwahifadhi na kushika nyadhifa za uwajibikaji katika serikali husika,ili hali idara inakabiliwa na watumishi wachache.

MARAIS WASTAAFU THABO MBEKI, FESTUS MOGAE NA BENJAMIN MKAPA WAKUTANA DAR ES SALAAM

1a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Festus Mogae wa Botswana wakiigia kwenye chumba cha Mkutano katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa Africa Readership Forum ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es salaam ambao ulikuwa unajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi za Afrika na kuangalia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za kushughulikia changamoto hizo.
2a
Rais mstaafu wa wa Afrika Kusin Thabo Mbeki akizungumza katika mkutano huo uliojumuisha viongozi mbalimbali wa afrika na taasisi mbalimbali kweye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
3a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini katikati ,Festus Mogae wa Botswana kushoo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa wakiwa wakiongoza mkutano huo.
4a
Baadhi ya viongozi kutoka taasisi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.
5a
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe katikati ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katik mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
6a
Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye kulia ni Mh. Balozi Ali Karume walikuwa ni miogoni wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo pia.