Na Magreth Magosso, Kigoma
WITO
umetolewa kwa viongozi wa serikali za Vijiji
mkoani hapa,waache hulka ya kulindana dhidi ya wahamiaji haramu ,hali
inayochangia jamii kuishi kwa kulipizana visasi.
Akizungumzia
hilo Kamamda wa Polisi wa hapa Frasser Kashai alibainisha kuwa,Julai ,27 ,2014
saa 12.30 jioni , Elias Balandes (36) ambaye ni muhamiaji haramu wa kijiji cha
Nyamidaho wilaya ya kasulu amemua mgambo kwa kile kinachodaiwa kulipa kisasi.
“alimuua
askari mgambo Shaban Mabad(34) kisa kulipiza kisasi kwa mgambo huyo,kwa sababu zinazodaiwa kuwa alimfikisha kwa mwenyekiti wa kijiji mhamiaji huyo kutokana na kuishi hapo kinyume cha sheria,lakini
aliachiwa katika mazingira tata ” alisema Kashai.
Aliongeza
kwa kusema siku hiyo wakiwa wanakunywa pombe za kienyeji kilabuni katika kijiji hicho,ndipo yalitokea marumbano baina ya
marehemu na Balandes akishirikiana na Faustine Phidel(55) walimshambulia mlengwa kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali
chini ya ziwa la kushoto na kiganjani.
Kashai
alisema marehemu alijikongoja peke yake hadi hospitali ya wilaya hiyo ambapo siku
ya tatu aliaga dunia,watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi kwa hatua zaidi.Wakati
huohuo Mkurugenzi wa idara ya uhamiaji Ebrosy Mwanguku alisema changamoto ya uhamiaji haramu kigoma ni kubwa ambapo baadhi ya viongozi wa vijiji sio raia halali.
Mwanguku
alibainisha kuwa,jamii inalindana yenyewe kwa yenyewe kutokana na mahusiano ya
ukaribu wa kuoleana ,hali inayokwamisha operesheni ya uhamiaji haramu mkoani
hapa na kusisitiza wananchi watajihukumu wenyewe kwa kuchezea amani iliyopo.
Akichangia
hilo Katibu Taifa chama cha NRA Hamis Fadhili akiri wananchi hutumia fursa za uchaguzi vibaya
hasa kuwasimika viongozi wahamiaji haramu kushika nyadhifa mbalimbali kama udiwani na watendaji wakuu wa
vijiji,hali inayochangia kulindana baina ya wahamiaji wanaoendelea kuja na viongozi husika.
Julai
12,mwaka huu wahamiaji haramu 99
wakiwemo watoto 29 walio chini ya miaka
18 walikamatwa katika operesheni ya idara ya uhamiaji mkoani hapa,ambapo wengi wao hutumiwa kama
vibarua katika mashamba ya wananchi wa hapa.
Aidha changamoto
hiyo inachangiwa na sheria dhaifu za idara hiyo,ambayo jamii huona ni nyepesi
na hivyo wengi hushiriki kuwahifadhi na kushika nyadhifa za uwajibikaji katika
serikali husika,ili hali idara inakabiliwa na watumishi wachache.
No comments:
Post a Comment