Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein(kulia) akisalimiana na
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi Mhe. Agnes Hokororo mapema leo
Agosti 1, 2014 alipowasili Viwanja vya Gongo tayari kwa ufunguzi rasmi
wa Maonesho ya 21 ya Wakulima na Wafugaji yanayofanyika Mkoani Lindi
Kitafa kwa mara ya kwanza tangu yaanzishwe hapa Nchini.
Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya
Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Kamani akitoa Salaam za Wizara katika Maonesho ya
Nane Nane Kitaifa kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar
Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein(Meza Kuu)katika ufunguzi wa Maonesho hayo
ya Wakulima na Wafugaji ambayo yanafanyika Mkoani Lindi Kitaifa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein(katika Jukwaa)
akiwahutubia Wakulima, Wafugaji pamoja na Wananchi wa Mikoa ya Kusini
yaani Lindi na Mtwara katika Ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Nane Nane
Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Gongo, Mkoani Lindi leo Agosti
1, 2014.
Baadhi ya Washiriki mbalimbali wa
Maonesho ya Nane Nane Kitaifa wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi Rais wa
Zanzibar, Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein(hayupo pichani). Waliovaa
Tisheti za Bluu ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza toka Makao
Makuu ya Jeshi la Magereza Kitengo cha Kilimo na Mifugo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Alhaj Ali Mohamed Shein akipata maelezo toka kwa
Maafisa Wataalamu wa Benki Kuu ya Tanzania ya namna Wakulima wanavyoweza
kupata dhamna ya Mikopo katika Mabenki mbalimbali hapa Nchini kwa Benki
Kuu ya Tanzania alipotembelea Banda hilo leo Agosti 1, 2014 katika
Sherehe za Maonesho ya Nane Nane Kitaifa yanayofanyika Mkoani Lindi kwa
mara ya kwanza.
Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni wakicheza ngoma ya kijadi Maarufu sana Mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment