Na MagrethMagosso, Kigoma.
MKAZI mmoja amekufa papo hapo na mweingine kujeruhiwa mara
baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota maarufu kwa jina la Mchomoko lililokuwa likitokea Manyovu
kuelekea Mjini katika barabara ya Kigoma- Kasulu eneo la Sido lililopo Manispaa
ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.
Akitoa taarifa ya tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma
SACP Fredinandi Mtui alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu usiku
katika eneo Mlole - Sido ambapo gari
aina ya Toyota lenye namba za usajiri T616 DXR lililokuwa likiendesha na
Pitolus Silasi (33), lilisababisha ajali hiyo.
Kamanda alimtaja marehemu kuwa ni Pantoleo Philipo (30)
ambaye alikufa popa hapo haku abiria aliyekuwa amembeba katika pikipiki yake
akiwa amejeruhiwa vibaya maeneo ya kichwani na kuvunjika mkono na mguu.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari ambapo
mara baada ya ajali dereva wa gari alitokomea kusiko julikana na kwamba
jitihadi za kumsaka zilifanyika na kumkamata ambapo atafikishwa mahakamani mara
baada ya kukamilika kwa upelelezi.
Akithibitisha kupokea maiti na majeruhi katika Hospitali ya
rufaa Maweni mganga mfawidhi wa hospitali Fadhili Kibaya amesema majira ya
usiku alipokea mwili wa marehemu pamoja na majeruhi mmoja aliyetambuliwa kwa
jina la Michael Madyane ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa maweni kwa
matibabu.
Kibaya alisema hali ya majeruhi ni mbaya na kwamba anatakiwa
kufanyiwa upasuaji wa mifupa na hivyo kulazimika kumpatia rufaa katika hospitali
ya Bugando ambapo kuna madaktari bingwa
wa upasuaji huo.
Alisema licha ya hospitali hiyo kuwa ya rufaa lakini bado
inakabiliwa na changamoto ya madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali pamoja na
vifaa tiba ambapo jitihada za maksudi zinaendelea ili kukabiliana na changamoto
hiyo.
No comments:
Post a Comment