Na Magreth Magosso, Kigoma.
KAMATI
ya utekelezaji ya baraza kuu la umoja wa vijana UVCCM wilaya, mkoani Kigoma imefanya ziara katika vijiji
vya mwambao wa ziwa Tanganyika na kubaini changamoto mbalimbali zinazo wakabili
wananchi wa maeneo hayo.
Katibu wa vijana wilaya Pantaleon Rumanyika
akizungumza na wandishi wa habari mkoa wa Kigoma alisema baada ya ziara na kubaini changamoto kadhaa ikiwemo ya ukosefu
wa mganga pamoja na nesi katika zahanati ya Kijiji cha Kagunga.
Amesema zahanati hiyo ina mtumishi mmoja
ambaye analalamikiwa na wananchi kutokuwa na vigezo vya kitaalamu sanjari na
akinamama wajawazito kutokubali kujifungulia katika zahanati hiyo kwa kuhofia
aibu.
Rumanyika alisema mtumishi aliyepo ni
mwanaume na hivyo kuwa ngumu kwa akinamama wajawazito kufika katika zahanati
hiyo na kulazimika kwenda katika vituo vingine na wengina kujifungulia
majumbani.
Alisema sambamba na hilo wakazi hao waliiomba
serikali iweze kuwatatulia tatizo la ukosefu wa miundombinu ya barabara ya
Chankere, Mwamgongo hadi Kagunga ambayo imekuwa ni kero ya muda mrefu licha ya
diwani wa kata hiyo Kassimu Nyamkunga kupiga kelele ujenzi wa barabara hiyo
katita vijao vya baraza la madiwani.
Alisema kukamilika kwa barabara hiyo
itasaidia kuponguza ajali na vifo vinavyojitokeza kwa wasafiri pamoja na
akinamama wajawazito ambapo kwa usafiri wa boti hutumia masaa kumi na moja
kufika Kigoma mjini kufuata huduma ya kujifungua.
Rumanyika alisema lengo hasa la ziara hiyo
katika vijiji vya Kagongo, Mwamgongo, Kagunga, Mahembe pamoja Nyarubanda ni kuwaandaa vijana kuwa tayari kujiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura, kusoma vizuri rasimu ya katiba mpya pamoja na kuwahamasisha
kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali.
Mganga mkuu wa wilaya Dkt. Jems Jumanne alikiri
kuwepo kwa tatizo hilo na kueleza kuwa taratibu za kuagiza mtumishi katika
Zahanati zinaendelea na kwamba taratibu za kupata nesi kwa lengo la kuwahudumia wajawazito
zitafanyika.
Alisema tatizo kubwa ni upungufu wa watumishi
katika wilaya hiyo ambapo ina jumla ya watumishi 130 na hivyo kuwa na upungufu
wa watumishi 294 ambapo kila kijiji kina Zahanati katika wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment