Na Mwajabu Kigaza, Kigoma.
WAVUVI katika ziwa Tanganyika mkoa wa Kigoma wametakiwa kuacha tabia ya kufanya uvuvi
haramu unaosababisha uharibifu wa mazalia ya samaki yaliyopo katika ziwa hilo
na kusababisha samaki kutoweka siku za badae.
Kauli hiyo imetolewa na katibu wa umoja wa Vijana UVCCM wilaya
Pantaleon Rumanyika wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji baraza kuu la umoja wa vijana wilaya
iliyofanywa katika vijiji mbalimbali vilivyopo mwambao wa ziwa Tanganyika Mkoa
wa Kigoma.
Alisema tabia ya uvuvi haramu kwa kutumia nyavu zisizo kubalika
kisheria zinaadhiri uharibifu wa mazingira katika ziwa hilo kwa kuuwa mazalia na
kusababisha siku za usoni kutoweka kwa samaki katika ziwa Tanganyika.
“Samaki hao wanapo vuliwa huwa wanaoza kwa muda mfupi kutokana na
nyavu zinazotumika kusababisha majeraha kwa samaki na hivyo wadudu kushambulia
na kuleta madhara kwa binadamu”alisema Rumanyika.
Rumanyika alisema lengo hasa la ziara hiyo katika vijiji vya
Kagongo, Mwamgongo, Kagunga, Mahembe pamoja Nyarubanda ni kuwaandaa vijana kuwa tayari kujiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura, kusoma vizuri rasimu ya katiba mpya pamoja na kuwahamasisha
kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali.
Akizungumzia hilo ofisa uvuvi
wilaya Josephat Gowele alisema tatizo la uvuvi haramu ni changamoto hasa ipo katika
maeneo ya Kaskazini ambapo chanzo kikubwa
cha uvuvi haramu ni wavuvi wanaotoka nchi jirani ya Burundi.
Amesema licha ya kuharibu mazalia ya samaki wakati wa uvuvi lakini
pia nyavu hizo huwa haziozi mara baada zinapotupwa ziwani na hivyo kusababisha
kila samaki anayepita karibu na nyavu hizo kunaswa.
Amesema uvuvi wa aina hiyo
unatoka nchi jirani ya Burundi wakishirikiana na wenyeji wa maeneo hayo hivyo
inakuwa vigumu kutokomeza uvuvi huo ambapo watu saba kutoka Burundi
walifikishwa mahakamani mara baada ya kufanya doria.
Gowele amesema ili kutokomeza tabia hiyo hakuna budi kufanya doria
za mara kwa mara, ulinzi shirikishi baina ya maafisa uvuvi na jamii ambapo
vikundi vya BMU vimeanzishwa katika
maeneo yote ya uvuvi lengo likiwa ni kulinda rasilimali zilizopo ziwani.
No comments:
Post a Comment