Pages

KAPIPI TV

Monday, November 24, 2014

UHARAMIA ZIWA TANGANYIKA KIGOMA HAUKWEPEKI

Na Mageth Magosso,Kigoma

“MAPATO  ya halmashauri ya kigoma hutegemea shughuli za uvuvi na kila mwezi kupitia mwalo wa kibirizi ambayo  inakusanya kiasi cha shilingi milioni 12 ,uporaji wa zana za wavuvi ziwa Tanganyika limebaki kwa wahanga wenyewe,serikali haisikii ,kilio cha wavuvi kinaishia majini  thamani yetu ipo katika  kodi tu, alisema ” Mwenyekiti wa Wavuvi  mkoani kigoma Sendwe Ibrahim.

“kipindi cha miezi 11  zaidi ya injini 25 zimeporwa, shida  ipo katika uwajibikaji,kila tunapopata  tarifa ya tukio  kutoka kwa wavuvi ziwani tunafikisha kwa uongozi wa juu ,jiografia ya ukanda wa ziwa ni fursa kwa wahalifu” alisema  Ibrahim.

Hayo yalisemwa jana asubuhi mbele ya wananchi waliokwenda kulangua dagaa na samaki katika mwalo wa Kibirizi uliopo manispaa ya kigoma ujiji,aliwambia zao hilo lipo mashakani kutoa ajira kutokana na wimbi la uporwaji wa zana husika.

Katibu wa Umoja wa wavuvi kigoma (UWAKI)Mohamed Kasambwe alisema usiku wa saa 4.00 ,23,Novemba mwaka huu km 5 kutoka bandari ya kigoma mjini eneo la Nondwa kata ya kibirizi majambazi watatu wakiwa na silaha ya moto  aina ya SMG walipora injini 2 na 16,Novemba injini 9 ,mafuta ya petrol lita 3000 na mipira ya kunyonya mafuta.

Thamani ya injini moja ni sh.milioni 7,mpira wa kunyonya mafuta sh.100,000 na lita moja ya mafuta inauzwa  sh.2,500 hali inayochangia  kupanda kwa bei ya dagaa na samaki,ambapo boksi moja  la dagaa huuzwa sh.250,000 na samaki  sh.350,000.

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya kigoma Ramadhan Maneno akiri janga hilo katika ziwa tanganyika halina ujanja,kutokana na ukosefu wa mawasiliano ya simu za mkononi kwa ukanda wa ziwa hilo, wahalifu hujinufaisha na uporaji wa zana za wavuvi.

Pia wananchi huficha tarifa za raia wageni na likitokea tukio ovu ndio hutoa tarifa na kuwasihi watoe ushirikiano wa wazi  kwa vyombo vya dola na wasimwamini kila mtu wafichue wahamiaji wasio rasmi.

Mkuu wa idara ya uhamiaji kigoma Ebrosy Mwanguku alisema changamoto ya uharamia ziwani na utekaji mabasi ya abiria yatakoma kupitia mfumo mpya wa uandikishwaji wa wahamiaji wasio rasmi kupitia "Data system".

Lengo ni kubaini wanaoingia na kutoka ambapo wananchi wa vijiji vilivyopo mipakani  , watendaji na madiwani wahakikshe kila  raia mgeni andikishe tarifa zake eneo husika na muovu atabainika kupitia vifaa maalum.

Akithibitisha hilo Kamanda wa Polisi wa hapa Jafari Mohamed alisema wamemtuma Ofisa wa majini na anafuatilia ili kubaini tukio hilo.

No comments: