Na Magreth Magosso, Kigoma.
ZAIDI ya wakazi 200 wanaoishi katika kata ya Buhanda mtaa wa Mgeo Manispaa ya Kigoma
Ujiji mkoani hapo, wamekosa malipo ya fedha zao kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) ilihali wanavocha ya kupata fedha hizo na kudai viongozi husika wanahusika na uchakachuaji wa stahiki za malipo yao .
Lengo
la serikali ni kuzinusuru kaya zilizogubikwa na hali duni ya
kipato,lakini uchakachuaji wa majina kwenye zoezi la utojai wa fedha
umekuwa na utata kwa walengwa hasa wazee.
Hayo yalisema mkoani humo na wakazi zaidi ya 200 , walisema kitendo cha kuondolewa kwa
baadhi ya majina ambayo yalipitishwa awali kwa kufuata vigezo vilivyotolewa
imewatia mashaka na kudai ni dhuluma inayofanywa na viongozi husika.
Kassim
Kagoma (73), Mwajuma Juma (62) na
Mariamu Bakari (75) wote wakazi wa kata ya Buhanda na wahanga wa tukio
hilo kwa nyakati tofauti walisema majina yao yamekatwa katika mchakato
wa ulipaji wa fedha za mpango wa TASAF ambapo awali majina hayo
yalikuwemo
katika orodha ya wanaolipwa.
“Hatuelewi
sababu ya sisi wazee kukatwa majina ,tupo 50 ajabu vijana wamelipwa wengi wao wana miaka 19 tu,wakiwa ni vijana wana uwezo
wa kumudu maisha ya kila siku, wamedai fedha zilizobaki zitarudishwa benki” walisema wakazi hao.
Serikali
ina nia ya kuwakomboa raia wake lakini shida ipo kwa viongozi husika
,ambao si waminifu na hawana imani ya walengwa ili waondokane na adha
zinazowakabili ,ambapo hutumia nafasi hiyo kujinufaisha wenyewe.
Aidha mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa mpango wa kulipa fedha katika kaya maskini Azizi Rusiga alisema jumla ya kaya zilizopo kwenye orodha ya malipo ni takribani kaya 533 kati ya hizo kaya 288 ndio zimelipwa na kaya 244 hazijalipwa fedha hizo.
Mchakato wa ulipaji ulianza rasmi Novemba 20 mwaka huu ambapo zaidi
ya sh. milioni 13.9 kilitengwa kwa ajili ya kulipa kaya 533 na v
kiasi kiongozi walilipa sh.milioni 7.6 na zaidi ya milioni 6.4 zikiwa zimebaki na kudaiwa zitarudishwa benki.
Alisema
aligundua uongozi wa TASAF ulitumia orodha mpya ambayo
hatukushirikishwa kama ile orodha ya awali haijakidhi kigezo,mbaya zaidi
uongozi wa kata hawajui ilihali walengwa wana vocha za kupewa sh.17
kila baada ya miezi miwili na walipoomba orodha mpya walinyimwa.
Mratibu
wa TASAF mkoa wa Kigoma Staphod Lilakoma alipohojiwa shutuma hizo alisema malipo
yaliyolipwa yamelenga kuanzia mwezi Septemba hadi Octoba na majina
yanayotumika kulipa ni majina yaliyofanyiwa marekebisho kwa mara ya pili katika
kipindi cha Novemba hadi Desemba ambayo yalikuwa hayana mashaka.
Alisema
chanzo cha kukatwa majina ni kutokana na udanganyifu uliotokea awali
na kwamba majina yaliyoorodheshwa awali yalikuwa na mashaka baada ya kugundua
kuwepo kwa kaya ndani ya kaya na lengo la mpango ni kusaidia kaya moja .
No comments:
Post a Comment