Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi
katika uwanja wa michezo wa Ilulu mjini Lindi wakati akihitimisha ziara
yake mkoani humo leo kabla ya kuendelea na ziara mkoani Mtwara kesho.
Kinana amesema viongozi wanatakiwa kuwa waadilifu na wanaojituma
kuwatumikia wananchi, akaongeza kwamba muda wa kulindana haupo tena na
kiongozi akiharibu awajibike mwenyewe kwa makosa yake na ni muhimu
kiongozi akiingia madarakani ajue na wakati wa kutoka. Wakati huohuo
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema katika sakata
la ESCROW kila mtu aliyehusika abebe msalaba wake.Nape alisema CCM
haijabadili msimamo wake ambapo alifafanua kama katika sakata la
Richmond Waziri Mkuu alijiuzulu , hivyo hata kwenye ESCROW
atakayebainika kuhusika naye achukuliwe hatua.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa akizungumza na
wananchi katika mkutano huo wa hadharawakati akimkaribisha Katibu mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akinukuu baadhi ya
vifungu vya katiba mpya inayopendekea wakati alipokuwa akifafanua mambo
mbalimbali kwa wananchi kuhusu katiba hiyo
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo katika mkutano huo wa hadhara.
Umati wa wananchi ukiwa katika mkutano huo
Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo ukisubiri kuanza kwa mkutano.
Baadhi ya vijana wa chuo cha VETA wakionyesha kadi zao za umoja wa Vijana wa CCM UVCCM katika mkutano huo.
Moja ya vikundi kikitumbuiza katika mkutano huo
wananchi wakifuatilia mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono
wananchi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ilulu mjini Lindi.
Nape Nnauye akiwasili katika mkutano huo.
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijumuika na wanachama wa CCM kutoka Tawi la Magogoni/Rahaleo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa mafundi bati
wakati walipokuwa wakipaua jengo la umoja wa vikundi vya akina mama
washonaji nguo..
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia nyavu za
kuvulia samaki wakati alipokitembelea mradi wa kuvua samaki huko Jamhuri
Machole.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa munyumba ya mwalimu shule ya msingi Nanyenje mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamba la mihogo la kikundi cha kuzalisha mbegu bora za muhogo.
Muhogo wenyewe ndiyo huu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba mtari wa kilimo cha umwagiliaji mbogamboga Mingoyo Mnazi Mmjoa.
No comments:
Post a Comment