MAMLAKA ya mapato Tawi la kigoma (TRA) imetumia zaidi
ya sh. Milioni 1.6 kwa kutoa msaada kwa mahitaji ya
wajawazito katika vituo vya afya vlivyopo Mkoani ya kigoma ili kuhamasisha
jamii juu ya ulipaji kodi.
Mamlaka hiyo imetembelea vituo vya afya vya Kikunku iliyopo
manispaa ya Kigoma Ujiji pamoja na Kituo Cha kulea watoto (vichanga ) yatima ambacho kinapatikana Halmshauri ya Wilya ya
Kigoma vijijini kata ya manyovu ikiwa ni moja kati ya makundi yenye uhitaji
zaidi kwaajili ya ukuaji wao.
Misaada iliyotolewa ni pamoja na maziwa,sabuni ,sukari na mafuta ya kupaka kwa
watoto huku wodi ya wajawazito wakinufaika na neti, sabuni na gloves ili
kuwawezesha akina mama hawa kujifungua katika mazingira mazuri.
Akitoa misaada hiyo,
kaimu meneja wa TRA Patrice Mushi alisema hakujua kama kituo hicho kina
mahitaji makubwa zinzoendana na changamoto
za kulea watoto hao na kuhakikisha
mahitaji yao yote ya muhimu yanapatikana.
“ ofisa ustawi wilaya
ya kigoma alinishauri nilete msaada ,nahisi nilicholeta hakitakidhi
hitaji,watoto wana umri wa mika 0-1 wanahitaji madawa na uangalizi mzuri ,motisha
kwa walezi na hawa wenye mambukizi ya
virusi vya ukimwi na huyu ana maji kichwani
“
Akipokea msaada Mlezi wa kituo cha Matiazo Mary Leonard
alisema changamoto iliyopo ni uhaba wa maziwa ,mafuta ya kupakaa,nepi za
kisasa,madawa na usafiri na ghrama za kuwapeleka kliniki watoto walio na shida
kubwa ya afya,hasa mwenye maji kichwani na wenye shida ya kutoboka kwa moyo.
“ nina miaka 19 tangu nianze kulea watoto vichanga,ambao
wengi walitupwa na kufiwa na mama ,ambapo tunalea na ikifika mwaka 1 familia inawajibu
wa kumchukua ,shida familia huwatelekeza hawaji kuwachukua na maofisa ustawi
hutuachia jukumu la kumsomesha ,mfadhili kajitoa “ alibainisha Leonard.
Kwa upande wa mchungaji wa kanisa la Aglikana Fredy Stephano alisema chamgamoto ya ugumu wa maisha
inachangia familia kutelekeza watoto waliovuka umri wa mika miwili washindwe
kuwachukua ,hasa waliofiwa na wazazi wa kike.
Naye ofisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya
kigoma Penina Mbwete alisema awali kituo
cha matyazo kilifadhiliwa na WFP kwa kushirikiana na kanisa la anglikana ,hivi
sasa WFP anafadhili wakimbizi na
wanatarajia katika bajeti ya 2015/16 kituo kitawekewa bajeti ili kuendelea
kutoa huduma husika.
Alisema wanawake waliowengi hivi sasa wanatupa watoto baada
ya kujifungua,ambapo mwanzoni mwa mwaka huu kuna mwanamke mmoja alitundika
mtoto na kondo lake juu ya mti na kuondoka ambapo wananchi wakishirikiana na
ofisa ustawi walimwahisha hospitali ya rufaa na leo ana mwaka 1 na anaitwa
Pamela.
Hali ya kutupa watoto vichakani inachangiwa na wanaume
kuwakana wanawake wanaowapa ujauzito na wanaume wenye ndoa zaidi ya moja
sanjari na michepuko ni chachu ya mimba zenye kutelekeza watoto hatimaye taifa
linakabiliana na watoto waishio katika mazingira hatarishi.
No comments:
Post a Comment