Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa Ruangwa Likangara tayari kuhutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Wananchi
wa Ruangwa wakionyesha furaha yao wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa
CCM kwenye uwanja wa mkutano Ruangwa Likangara.
Wananchi
wa Ruangwa wakiwa na mabango yaliyobeba ujumbe wakati wa mkutano wa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amekuwa mstari wa
mbele katika kujenga na kukiimarisha chama,Katibu Mkuu wa CCM
ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akihutubia wakazi wa
Ruangwa ambapo aliwaambia CCM inaimarika kutokana na kuwa na sera zenye
kuleta maendeleo kwa Watanzania pamoja na kuthamini amani iliyopo
nchini.(Picha na Adam Mzee)
Umati wa wakazi wa wilaya ya Ruangwa wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wao wa CCM Taifa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa wilaya ya
Ruangwa waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza,Kinana amekuwa Katibu Mkuu
wa kwanza wa CCM kuzunguka nchi nzima ,kushiriki kwenye miradi mbali
mbali ya maendeleo,kukagua ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 pamoja na kutoa
elimu kwa wananchi hasa ya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii.
Mbunge wa Jimbo la Ruangwa
Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wakazi wa Ruangwa ambapo alielezea
katika kipindi chake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge ameshiriki
shughuli mbali mbali za maendeleo jimboni kwake.
Mbunge wa Jimbo la Ruangwa
Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa Ruangwa ambapo
alichukua muda wa kutosha kufafanua kwa wananchi namna alivyotekeleza
wakatoi wa kipindi chake kama Mbunge wa Jimbo wakati wa mkutano wa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anafanya ziara katika
mikoa ya Lindi na Mtwara
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Ruangwa
ambapo alisema uongozi mbovu kwenye vyama vya ushirika ni chanzo cha
kusababisha matatizo kwenye zao la korosho,aliwaambia wananchi hao
hakuna sababu ya msingi ya kuwa na utitiri wa vyama vya ushirika.
Wananchi
wa kijiji cha Mibure wakiwa na furaha wakati wa kumkaribisha Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kijiji chao kilichopo
wilaya ya Ruangwa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha
Mibure ambapo aliwapongeza uamuzi wao wa kujenga Zahanati ya kijiji kwa
kushirikiana na Mbunge wao pamoja na Halmashauri.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha
Mibure ambapo aliwashauri vijana kujiunga vikundi na kufanya shughuli za
ujenzi kwani kuna miradi mingi ambayo vijana wanaweza kupatiwa fursa ya
kuifanya kwa gharama nafuu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua jengo la zahanati ya
kijiji cha Mibure ambacho kinajengwa na mafundi wa kawaida wa kijijini
hapo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wananchi wa kata ya Chienjele wilayani Ruangwa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya
Chienjele wilaya ya Ruangwa ambapo aliwaambia vijana kuwa bado kuna
fursa nzuri nchini katika kuleta maendeleo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCMkata ya Nandagala wilayani Ruangwa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia chanzo cha maji kwenye
mto Ole kijiji cha Ng’au kata ya Mnachu wilaya ya Ruangwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda miti kwa ajili ya kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha
Ng’au Ole wilaya ya Ruangwa ambapo aliwahimiza kutunza mazingira kwa
kutokata miti badala yake wapande miti kutunza vyanzo vya maji.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya
Nandagala ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama mkoa wa
Lindi.
No comments:
Post a Comment