Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif
Shaban Mohamed (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Daftari la
wanachama wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, katika hafla
iliyofanyika leo Ukumbi wa Anautoglo. Anayeshuhudia kulia ni Katibu wa
Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed (kushoto) na Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje wakionesha daftari hilo baada ya kuzinduliwa.
Viongozi
wa meza kuu wakipiga makofi wakati wakiimba wimbo wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kabla ya kuzindua daftari hilo. Kutoka kulia ni Katibu
Msaidizi wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Mavela,
Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Wilaya ya Ilala,Meritius Mangugu,Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje , Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif
Shaban Mohamed, Katibu wa Elimu na Malezi Taifa, Masoud Bwire na Mjumbe
wa Kamati ya Utekelezaji mkoa wa Dar es Salaam, Nicolaus Msemo.
Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Katibu
wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje (kushoto), akiteta
jamba na wajumbe wa kamati ndogondogo zilizoundwa ili kurahisisha
utendaji kazi wa jumuia hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Wilaya ya Ilala,Meritius Mangugu na Angelina Malembeka.
Wajumbe
wa Kamati ya Afya, Maafa na Mangira wakijadiliana jambo, Kutoka kushoto
ni Ali Said, Josephat Kadiya na Dk. Meshack Sabaya.
Wajumbe wakijadiliana jambo, Kutoka kushoto ni Omar Njate, Seleman Kumchaya na Seleman Nduda.
Wajumbe
wa Kamati ya Uhamasishaji, Mapambo na Makazi wakiwa kwenye mkutano huo.
Kutoka kulia ni Janeth Sondoka, Amina Mlewa na Khadija Kingi.
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi, Fedha na Mipango, wakifuatilia uzinduzi huo.
Wajumbe
wa Kamati ya Elimu na Malezi wakifurahia jambo. Kutoka kulia ni Amina
Mtemvu, Levocatus Machage, Maria Ernesti na Galila Ramadhan.
Wajumbe wakiwa katika uzinduzi huo.
……………………………………………………………………
Dotto Mwaibale
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed amewata viongozi wa
jumuia hiyo kuwa wabunifu wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili
kuifanya jumuia hiyo kukua kiuchumi.
Moto huo aliutoa wakati akizindua Daftari la Wanachama wa Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam leo.
“Nawapongezeni kwa kuunda kamati ndogondogo ndani ya jumuia itasaidia kusogeza huduma kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla hivyo kukifanya chama chetu kiendelee kuaminiwa” alisema Mohamed.
JUMUIYA YA WAZAZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) MKOA WA DAR ES SALAAM YAZINDUA DAFTARI LA WANACHAMA WAKE
Alisema kwa mfano katika shule ya jumuia hiyo ya Boza iliyopo mkoani Tanga kuwa ina ardhi ya kutoka lakini haifanyiwi uzarishaji mali wowote.
Mohamed alipongeza Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha daftari hilo kwani litasaidia kuwatambua wanachama wao kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa hivyo kurahisisha shughuli za kisiasa kwa kutambuana katika chaguzi mbalimbali na shughuli za maendeleo.
Katika hatua nyingine Mohamed alisema wanajumuia wote ya wazazi wanaiunga mkono rasimu ya Katiba mpya iliyopendekezwa na Bunge Maalumu na kuwa wao wanautaka muundo wa serikali mbili kwani ndio utalipeleka mbele Taifa la Tanzania.
Alitoa mwito kwa wanachama wote wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kuwachagua viongozi wao kuanzia ngazi za mashina wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika hivi karibuni.
Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje alisema mpango wa kuanzisha daftari hilo ni moja ya mikakati yao ya kuibadilisha jumuia hiyo kiutendaji badala ya kuegemea katika eneo moja la siasa.
“Hii jumuia yetu kwa muda mrefu ilikuwa nyuma kimaendeleo lakini tumedhamiria kuibadilisha na kuwa ya kiutendaji zaidi na ndio maanna tumeanzisha kamati ndogo ndogo za maendeleo na kuwateua watu wenye sifa za kuziongoza yaani wenye taaluma” alisema Cholage
Cholage aliwataka viongozi wote waliochaguliwa kujitambua kuwa wamechaguliwa si kwa bahati mbaya bali ni kwa ajili ya kuleta maendeleo ndani ya jumuia hiyo.

No comments:
Post a Comment