Pages

KAPIPI TV

Thursday, October 30, 2014

AMUUA MTOTO WA DADA YAKE KWA KUMKATA MAPANGA-KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

Mgonjwa  wa  akili  Mkazi wa Kijiji cha Kandaga wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma Henry James(19) atapandishwa kizimbani katika  Mahakama ya hakimu mkazi wilayani    hapa kwa kitendo cha kumkatakata mapanga hadi kufa mtoto (2) Deniza Ramadhan.

Akielezea tukio hilo ofisini kwake mbele ya wandishi wa habari  kigoma Ujiji  jana Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Jafari Mohamed alisema Octoba ,25,majira  ya saa 2.00  usiku kijijini hapo, kijana huyo  ambaye pia ni kaka wa mama wa mtoto huyo Frola  James(26) alishtuka kutoka usingizini baada ya  kaka yake kufanya  unyama huo.

“ alifanya mauaji haya baada ya siku mbili tu,kutoka hospitali ya wilaya hiyo na vipimo vinaonyesha ni mgonjwa wa akili  , mtoto alilala kitandani ,akaingia chumba alicholala mtoto akiwa na panga na kuanza kumkatakata shingo na hatimaye kufa papohapo ila ni mwehu ,sheria inajua aina ya uchizi atahukumiwa hivyohivyo” aliabainisha kamanda  Mohamed.

Katika tukio la Pili  KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed amethibitisha tukio la uporaji wa zana za wavuvi zilitokea Octoba ,25,mwaka huu   Ziwa Tanganyika  kijiji cha Kalalangabo Jimbo la kigoma kaskazini  na kudai kuwa ni  njama iliyosukwa na Mwenyekiti wa kijiji  hicho Ramadhan Hamis (46) na mwenzake  Lolinda Mustafa (33) .

 Kamanda Mohamed  alisema  majira  ya saa 5.00 usiku wa octoba 25,mwaka huu watu wasiofahamika wakiwa na silaha za moto tatu walimvamia Kiza Wiliam(44) na kupora mashine mbili  na vitu mbalimbali zenye thamani  ya zaidi ya  sh.milioni 4.5.

Changamoto ya uvamizi ziwani unahusishwa na hujuma miongoni mwa wamiliki wa mitumbwi ambao baadhi yao hushirikikiana na wahalifu kutoka nchi jirani ya DRC-Congo na kuwavamia wavuvi wakiwa kwenye shuighuli hizo na kuiba mashine na vifaa vingine vya uvuvi.
 
Mwenyekiti wa wavuvi  Mkoa wa Kigoma  Sendwe Ibrahimu alisema wananchi walimtilia shaka mwenyekiti huyo kutokana na kukubali ushahidi wa kusimamia hati ya mauziano  ya mashine kwa raia wa wilaya mbili tofauti ,ambapo kisheria kama mashine ni halali muuza na mnunuzi wangeuziana katika kijiji chao .

Aidha pamoja na kukamatwa kwa mwenyekiti wa kijiji  hicho na mwenzake, bado  msako unaendelea ili kubaini wengine waliopo katika mtandao wa kihalifu  wa kuiba zana za wavuvi ziwani kila ifikapo mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka na watapandishwa kizimbani baada ya upelelezi wa awali utakapokamilika.

No comments: