Pages

KAPIPI TV

Sunday, September 14, 2014

WASHINDI TUZO ZA HABARI ZA TANAPA 2013 WAENDELEA KUJIFUNZA MAENEO YA UTALII AFRIKA KUSINI

1Mwanahabari Vedasto Msungu wa ITV (kushoto) na David Rwenyagira (Radio 5) walikuwa miongoni mwa wanahabari waliofika nje ya Jengo la Mahakama Kuu ya Pretoria ambapo ilikuwa siku muhimu ya utoaji hukumu kwa mwanariadha Oscar Pistorius aliyeshitakiwa kwa makosa ya kumuua mpenzi wake kwa silaha. Unayoyaona hapo nyuma ni magari maalum ya urushaji tukio hilo moja kwa moja katika vyombo mbalimbali vya habari duniani(OB Van) na mahema meupe ni Kambi iliyopigwa na wanahabari hao kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo muhimu.
2Wanahabari Vedasto Msungu na David Rwenyagira walipata nafasi ya kumhoji raia huyu wa Afrika Kusini juu ya maoni yake kwa hukumu iliyotarajiwa kutolewa 3Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 waliweza kufika hadi katika Hifadhi ya Taifa ya Pilanesberg ili kujionea wanyama mbalimbali. Kutoka Kushoto ni Mtanzania Peter Masika anayeishi Johannesburg, Vedasto Msungu (ITV), Pascal Shelutete(Meneja Mawasiliano TANAPA) na Gerald Kitabu wa The Guardian 4Wanyama aina ya Nyumbu wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Pilanesberg 5Washindi wa Tuzo za TANAPA 2013 waliweza pia kufika katika Mji wa Sun City kama wanavyoonekana hapa

No comments: