Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Juma
Abeid Diwani wa Kata ya Magawa wilayani Mkuranga wakati alipotembelea
shamba la Mikorosho lenye hekari 1000 ambapo mikorosho inayokaribia elfu
20 imeharibika vibaya baada ya kupata ugonjwa unaonyausha mikorosho
hiyo , Diwani huyo amesema wananchi wa kata hiyo wako katika hali mbaya
kwakuwa zaidi ya miaka minne sasa hawajavuna chochote na maisha yao
yanazidi kuwa mabaya, Katibu Mkuu Kinana yuko katika ziara ya mikoa ya
Pwani, Tanga na Iringa akikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM
ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za
maendeleo, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa
NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-
Juma Abeid Diwani wa Kata ya Magawa wilayani Mkuranga akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akikagua shamba hilo leo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa na Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Pwani Mwishehe Mlao jinsi mikorosho hiyo ilivyoharibika kutokana
na kukumbwa na ugonjwa huo, kushoto ni Juma Abeid Diwani wa kata ya
Mgama
Juma Abeid Diwani wa kata ya Mgama akitoa maelezo yake mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi
akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Wilaya ya Rufiji wakati Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili katika mji wa Ikwiriri
kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mh. Nurdin Babu.
Wajumbe wa Harmashauri kuu ya Wilaya wakiwa katika kikao cha ndani kilichofanyika kwenye ukumbi wa FDC mjini Ikwiriri
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Harmashauri kuu ya Wilaya.kilichofanyika kwenye ukumbi wa FDC mjini Ikwiriri
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi kwenye ofisi ya mafundi seremala mjini Utete.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akipokea zawadi ya viti kutoka kwa kikundi cha vijana Maseremala mjini
Utete kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa , Itikadi na Uenezi na
wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo la Rufiji na Waziri wa Afya na
Ustawi wa jamii Mh. Dr. Seif Rashid.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi Ofisi ya CCM wilaya ya Utete Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua jengo la ofisi ya CCM wilaya ya Utete
Mmoja
wa wapiga ngoma wa kikundi cha ngoma cha mjini Utete akipiga ngoma huku
akiwa amebeba mtoto wake mdogo na mtoto wake mwingine akiwa amekaa
pembeni.
Mkuu wa wilaya ya Rufiji Mh. Nurdin Babu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Utete leo
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa , Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi wa Utete katika mkutano uliofanyika leo mjini humo
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa , Itikadi na Uenezi akimuwekea
kipaza sauti mmoja wa wazee waliofika kwenye mkutano ili kumsikiliza
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kuuliza maswali yake
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wana Utete wakati wa mkutano wa hadhara uliofnyika mjini Utete.
Baadhi ya wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi wakila kiapo mara baada ya kupokea kadi zao za uanachama
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa , Itikadi na Uenezi wakinyanyua mikono yao juu wakati wakila kiapo cha utii kwa chama,
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Dr. Onesmo Mambosho Mganga Mfawidhiwa wa kituo cha afya cha Nyamwage.
No comments:
Post a Comment