Pages

KAPIPI TV

Sunday, September 14, 2014

KINANA ZIARA YA MKURANGA

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kimanzichana leo wakati alipoanza Ziara yake ya mikoa ya Pwani ,Tanga na Iringa Ikiwa ni kuimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 huku akihimiza wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo katika maeneo yao, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi na leo amefanya shughuli mbalimbali katika ziara hiyo. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MKURANGA -PWANI) 2Mbunge wa jimbo la Mkuruanga na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Adama Malima akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkuranga wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo leo. 3Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akizungumza na wananchi wa kata ya Kimanzichana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapo. 4Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Mh. Mercy Silla akwahutubia wananchi wa kata ya Kimanzichana kwenye mkutano wa hadhara. 5Baadhi ya wananchi wakipunga mikono kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kimanzichana. 6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano mjini Kimanzichana, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkuranga. 8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli ya kufyatua matofali pamoja na wanakikundi wa kikundi cha Mkuranga Youth Development ambapo amekipa kikundi hicho mashine 2 ili kuongeza uwezo wa kikundi hicho. 9Mmoja wa wanakikundi wa kikundi cha Mkuranga Youth Development Bi Faraja Msani akionyesha jinsi wanavhoshiriki shughuli za kujiletea maendeleo. 10Wananchi wakishiriki kukusanya matofali katika shule ya sekondari ya Mwarusembe. 11 12Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli ya ujenzi wa mafarasa katika shule ya sekondari ya Mwarusembe huku wananchi wakiendelea na kazi ya kukusanya matofali. 13Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akishiriki ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Mwarusembe. 15Baadhi ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Pwani kutoka Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi 16Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akionyesha ripoti mbalimbali za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM wakati wa kutano wa ndani na wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Pwani. 17Mmoja wa viongozi wa CCM wilaya ya Mkuranga Bi Agricola akiwa katika mkutano huo

No comments: