VIONGOZI wa serikali za mikoa ya mpakani mwa Burundi na Tanzania wasema mahusiano mema ya nchi hizo kiulinzi uchumi na biashara ni moja ya nguzo muhimu kulinda amani na utulivu baina yq nchi hizo
hayo yamesemwa na wakuu wa mikoa ya Luyigi nchini Burundi na Kigoma nchini Tanzania wakati wa mkutano maalumu wa ujirani mwema unaofanyika Alhamisi hii katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kigoma Tanzania
Mkuu wa mkoa wa Luyigi nchini Burundi ambaye ni mkuu wa msafara huo Bw Nshimilimana Siriyako ameshauri Tanzania kuboresha miundombinu ya Reli ya kati na barabara kwakuwa Burundi inategemea bandari za Dar na kigoma kibiashara.
aidha mkuu wa mkoa wa kigoma luten kanali mstaafu Issa Machibya amesisitiza umuhimu wa nchi hizi kuboresha ulinzi wa mipaka kupunguza uwezekano wa mwingiliano wa waharifu na wahamiaji Haramu ambao mara zote wamekuwa wahusika wakuu wa matukio ya ujambazi wa kutumia silaha kali za kivita
Hata hivyo mwakilishi wa Burundi katika ujumbe huo wa kamati ya ulinzi na usalama kwa mikoa hiyo Bw Nshimirimmana ameipongeza Tanzania nakuhimiza kuendeleza oparesheni ondoa wahamiaji haramu nakwamba ilifanya wakimbizi haramu kurejea nchini kwao na salsa wanajenga nchi yao kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment