Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu
MKULIMA
na mkazi wa kijiji cha Iyumbu tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi mkoa wa
Singida,Jubulu Mahende,amefariki dunia muda mfupi baada ya kupewa
matibabu na mtu anayedaiwa kuwa ni daktari feki.
Imedaiwa
kuwa Jubulu aliyekuwa akisumbuliwa na kifua, kiuno na mgongo
alizidishiwa dawa kitendo kilichopelekea hali yake kuwa mbaya zaidi.
Daktari
huyo ambaye amekiri hana cheti cha aina yo yote kutoka vyuo vya
afya,Prospa Simson,baada ya kubaini hali ya mteja wake inakuwa
mbaya,alimpa chupa tisa za maji,ili kuokoa maisha yake,lakini hata hivyo
juhudi hizo hazikuzaa matunda.Pia alipatiwa vidonge sita ambavyo hata
hivyo havijafahamika vilikuwa vinatibu maradhi gani.
Imedaiwa kuwa baada ya muda mfupi,Jubulu alipoteza maisha yake katika sebule ya nyumba ya mganga feki, Simson.
Kaimu
mganga mkuu wa wilaya ya Ikungi, Dk.Philip Kitundu alisema tukio hilo
lilitokea Agosti 10 mwaka huu saa nne asubuhi kwenye vyumba maalumu
vilivyotengwa na Simson kwa ajili ya kutolea huduma mbali mbali za
matibabu.
“Tulipata
taarifa ya tukio na agosti11mwaka huu, tulienda kukagua duka la dawa
ambalo lilisadikika lilitibu Jubulu ambaye alifia pale pale
dukani”alifafanua.
Akifafanua
zaidi,alisema walipolikagua duka hilo,waligundua kuwa Simon hakuwa na
leseni kutoka TFDA ya kumruhusu kufanya biashara ya kuuza dawa kwa ajili
ya binadamu.Pia yeye mwenyewe Simon,alikiri kuwa hakuwa na cheti cha
chuo chochote alichosomea utaalamu huo.
“Hata
tulipopekuwa pekua dukani tulikuta madawa ambayo hayaruhusiwi kabisa
kwenye maduka ya dawa muhimu,tulikuta madawa ya sindano,madawa ya
vidonda,alikuwa anafunga vidonda,analaza,anatoa huduma za kujifungua kwa
akina mama wajawazito”alisema Dk.Kitundu.
Aliongeza
kwamba katika ukaguzi huo walikuta pia dawa zilizokwisha muda wake wa
matumizi. Tukio hilo la watu kupoteza maisha yao ni la tatu kutokea kwa
watu waliopatiwa matibabu katika duka hilo isipokuwa matukio mawili
yalitokea nje ya duka hilo.
Kwa
upande wake daktari huyo bandia,Dk.Prospa Simson licha ya kukiri
kumpokea mgonjwa huyo akiwa na hali mbaya na kwamba baada ya kuchukua
historia yake aligundua kuwa alikuwa akisumbuliwa na kifua na kwamba
kabla ya kupelekwa kwake, alianza matibabau kwa waganga wa tiba asilia.
Kwa
upande wake mtoto wa marehemu, Jilala Jibulu, alisema siku ya tukio
asubuhi alikwenda kumsalimia baba yake na kumkuta akiwa na hali mbaya na
ndipo alipoamua kumpeleka kwenye duka hilo la madawa,na muda mfupi
alifariki akipatiwa matibabu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela,amekiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema
kwa sasa wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kama muuza duka hilo la
madawa, ndiye alikuwa akimtibu au alienda dukani hapo kununua dawa
alizoandikiwa na daktari mwingine.
No comments:
Post a Comment