Na Magreth
Magosso,Kigoma
IMEELEZWA
kuwa,Mkoa wa kigoma umefanikiwa kutimiza agizo la Rais Jakaya Kikwete juu ya
kuanzishwa kwa Benki maalum ya matofali kwa ajili ya ujenzi wa majengo
mbalimbali katika sekta ya elimu,Afya na Ulinzi kwa lengo la kuboresha huduma
hizo.
Tamko hilo
limefanikiwa kwa asilimia 65 ya nguvu kazi ya wananchi wa wilaya sita ya
Kigoma,Kakonko,Buhigwe,Uvinza,Kasulu na Kibondo kwa kuweza kuwa na matanuri ya
matofali yapatayo 70 sawa na matofali milioni tatu,ambapo ifikapo mwishoni mwa mwka
huu watakuwa na matofali milioni 5 .
Wakizungumza
kwa nyakati Tofauti baadhi ya wakazi wa mkoa huo Tumain Fredrick na Juma Hassan
walisema wanachi wapo tayari kutoa
nguvu,akili na mali zao katika shuguli za maendeleo ya taifa lao kwa maslai ya
kizazi cha leo na siku za usoni kwa kufuata taratibu husika na kuwaasa viongozi wasimamie kwa dhati ili kufanikisha
malengo mtambukwa.
Kwa upande wa
mwanafunzi wa shule ya sekondari Manyovu
Juma Nyamgenda alisema ujenzi wa maabara ukifanikiwa katika shule zote itasaidia
ufaulu wa masomo michepuo ya sayansi
ambapo watajifunza kwa vitendo , pia
uwepo wa mabweni ni usalama kwa kutokubughudhiwa
na kazi za majumbani na mimba kwa wanafunzi wa kike na kuisihi serikali na jamii watimize ili ndoto zao zitimie.
Akizindua
matanuri hayo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Lt.mstaafu Issa Machibya alisema mradi huo
ni moja ya kupunguza changamoto mbalimbali katika jamii husika,hususani ujenzi
wa maabara,mabweni,nyumba za watumishi idara ya ulinzi,wauguzi na walimu.
Machibya
aliongeza kwa kubainisha kuwa,viongozi wakishirikiana na wananchi katika agizo
hilo ni moja ya kuokoa wanafunzi na matokeoa mabovu ya mtihani wa taifa sanjari
na mimba za utotoni kwa wasichana wanaosoma shule za kutwa ambapo ujenzi wa
mabweni ni tija kwao kuondokana na vishawishi vya uraiani.
Aidha Mpango wa Benki ya Tofali umefikia awamu ya
pili baada ya awamu ya kwanza ulikuwa ni mandalizi ya ufyatuaji wa matofali
ambapo juzi ulizinduliwa rasmi na mkuu wa mkoa huo katika kijiji cha Mwayaya
wilaya ya buhigwe ambapo kupitia wilaya zake sita wamefanikisha agizo la Jakaya
Kikwete kwa maslai ya umma na kuongeza
ufanisi wa huduma kwa jamii husika.
No comments:
Post a Comment